SoC02 Afya ya akili na uchumi wa vijana

Stories of Change - 2022 Competition

Celectn

New Member
Aug 8, 2022
1
0
AFYA YA AKILI NA UCHUMI WA VIJANA

Nusu ya magonjwa yote ya akili duniani yanaanza kati ya umri wa miaka 14, na mengi hayabainiki wala kutibiwa, suala linaloweka mustakabali wa vijana wengi njia panda. Imesewa na “Shirika la afya Duniani WHO”

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO, Hadi mwaka 2020 watu bilioni moja, walikua wanaishi na magonjwa ya akili na wengi waliohatarini ni wale wenye umri wa miaka 15 – 39. Kati ya asilimia 75 -95 ya watu wanaokabiliwa na mtatizo ya afya ya akili ni katika nchi zenye uchumi wa chini na wa wastani, na hawawezi kupata huduma kabisa.

Vijana ndio chahchu ya mendeleo ya jamii yoyote ile. Katika nchi za Afrika kumekuwa na mwitikio hafifu wa kujadili matatizo ya afya ya akili kwa vijana. Kumekua na sera nyingi za elimu, ujasiriamali, warsa wezeshi lakina matunda ya kazi hizi zote nzuri si kadri ya makisio. Vijana ni kundi pekee ktik jamii lenye nguvukazi kubwa, Sasa swali tunalotakiwa kujiuliza Je, Tunapata matokeo chanya au hasi kwa nguvukazi hii?

Ni ukweli usiopingika kua mtu ambaye ana matatizo ya afya akili hawezi kuzalisha kwa wastani unaohitajika. Changamoto inayotukabili ni matatizo haya hayaonekani kwa macho kama mgonjwa mengine. Hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuangalia suala hili katika uwanda mpana.

VYANZO VYA MATATIZO YA UGONJWA WA AKILI

  • Msongo wa mawazo, hofu na wasiwasi.
  • Mazingira hasi ya malezi ya Watoto
  • Unyanyasaji wa Watoto
  • Migogoro ya kifamilia
  • Pombe na madawa ya kulevya
  • Upweke na Kujitenga
Kupelekea ongezeko la ugonjwa huu katika kundi la vijana, limepelekea changamoto mbalimbali katika ukuaji wa uchumi wa vijana.

Ubunifu hafifu katika shughuli za kiuchumi.

  • Vijana wengi wanaamini kua vyeti vyao vitawapatia kazi nzuri na mshahara mzuri, hivyo kupelekea kukosa ubunifu katika soko la ajira, na wale ambao wapo kwenye ajira wanashindwa kua wabunifu katika kuongeza ujuzi na maarifa kitu kinachopelekea kupunguzwa kazini au kukosa kupandishwa cheo.
  • Vijana hasa wenye elimu hawataki kusikia shughuli za uchumi nje ya soko la ajira, mf. Ukimuambia muhitimu kuwa kuna fursa kwenye kilimo hawezi kuhamasika sababu haamini kua alisoma mpaka chuo ili aje kua mkulima.

Kutokuishi kulingana na uhalisia
  • Leo hii unakuta kijana anamiliki simu nzuri yenye thamani ya Zaidi ya milioni moja, halafu anakuambia kua hana mtaji wa kufaanya biashara. Vijana wanavaa kiumaridadi, wanasuka nywele za laki tatu lakini wanakosa maarifa ya kutengeza kipato. Ukitafakari kwa kina hoja hii utagundua jinsi gani vijana walivyo na tatizo la akili, maana kama uko sawa huwezi kumiliki simu ya gharama isiyo na tija kwa uchumi wako binafsi.
Ushiriki hafifu katika shughuli za kijamii
  • Kupitia shughuli za kijamii kama mikutano ya serikali za mitaa, vijana wanaweza kutoa changamoto zao na zikapata ufumbuzi kwa urahisi kuliko kusubiri matamko ya mawaziri.
Ongezeko la matendo machafu katika jamii
  • Kuna wakati simu ya mkononi aina ya iphone 13 ilipotolewa, mitandao ya kijamii ilikumbwa na taarifa nyingi za vijana wa kike na kiume kua tayari kufanya mapenzi na watu wenye pesa ili wapewe zawadi ya simu hiyo. Tukio hili linadhirishwa na ongozeko kubwa la biashara ya ngono. Na wanaofanya biashara hii ni vijana na kati yao kuna wanfunzi wa vyuo vikuu.

Ongezeko la visa va mauaji
  • Kwa kipindi cha hivi karibu kumekua na matukio ya mauaji yanayo chochezwa na wivu na migororo ya kimapenzi. Imetokea Zaidi ya mara mbili mume kumuua mke na yeye kujiua. Tunaweza kusemaa chanzo ni wivu ila ukweli ni matatizo ya afya ya akili. Mauaji haya yanaa athaari mojakwamoja kwa uchumi wa vijana, maana wanaojiua wanaaacha watoto na jamii inakua imepoteza nguvu kazi.

Ongezeko la vitendo vya ubakaji na ulawiti wa Watoto wadogo.
  • Kumekua na mtitiririko wa matukio ya ubakaji na ulawiti wa Watoto wadogo. Matukio haya yamekua yakifanywa na ndugu wa karibu, waalimu, na majirani. Vitendo hivi vichafu ni dhahiri mtupu afya ya akili imekua duni sana, maana watendao uchafu huu ni vijana. Matokeo vijana wanaishia jela na jamii inapoteza nguvukazi.
NAFASI YA SERIKALI KATIKA KUBORESHA UCHUMI WA VIJANA.
  • Kuhusisha masuala ya vijana katika sera zote.
  • Elimu mafunzo ya mendeleo ya ujuzi wa vijana kujiajiri.
  • Utoaji wa elimu wa afya ya akili kwa vijana na jamii kwa ujumla.
  • Kuboresha mazingira ya ubunifu, sanaa na michezo.
  • Kutoa nafasi kwa vijana kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi.
  • Kuhamasisha vijana kujikita na shughuli za kilimo
  • Kuhamsisha vijana kuelewa fursa za tecknolojia ya habari na mawasiliano.
CHANGAMOTO YA SERIKALI KATIKA KUBORESHA AFYA YA AKILI
  • Upungufu wa wataalamu wa masuala ya vijana
  • Sekta ya vijana bado haina watendaji wenye taaluma ya vijana, kutokana na watendaji wengi kukosa taaluma, serikali imekua ikitumia watendaji wenye taaluma maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii.
  • Watumishi wenye taaluma ya vijana wanahitajika ili kuweza kutekeleza hoja zilizopo kwenye mfumo wa kisheria wa kushughulikia masula ya vijana.
  • Upungufu wa wataalamu wa masuala ya Afya ya akili
  • Upungufu wa wataalamu ni janga la kidunia, ndio maana takwimu zinaonesha zaidi asilimia sabini na tano ya waathirika wa matatizo ya afya ya akili hukosa huduma. Serilikali inatakiwa iwekeze katika kuzalisha wataalamu ambao ndio watakua chachu ya kupambana na tatizo hili.

MAONI

Dunia ya sayansi na tecknolojia imeleta fursa kedekede kwa vijana, lakini katika upande wa pili imeleta matatizo pia. Utandawazi umekua na athari sana kwa jamii pale ambapo umekua ukitumika vibaya. Mashindano ya kutaka kufanikiwa na kuonekana imeongeza chachu kwa vijana wengi kupata misongo ya mawazo. Kama jamii kunatakiwa kua na mipango ya kimkakati ya kunusuru vijana katika jaanga hili.

Jitahada zinazotumika kuhamasisha vijana kuchukua fursa katika maendelo ya sayansi na tecknolojia, zitumike vivyohivyo katika kupambana na athari za sayansi na tecknolojia kwa kuhakikisha vijana wanakua na afya bora ya akili. Hapo ndio fursa zitatumika vizuri na uchumi wa vijana na taifa utakua kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom