Afya na kanuni bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afya na kanuni bora

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  1.LISHE

  1. Badilisha chakula chako kila mlo, lakini usile vyakula vya aina

  nyingi sana katika mlo mmoja. Iweke milo yako na chakula chako
  unachopakua kuwa rahisi.

  2. Tumia zaidi nafaka zisizokobolewa kwa mashine kama mkate wa ngano

  isiyokobolewa na mchele usiokobolewa kwa mashine. Tumia kwa nadra sana
  chakula kilichotayarishwa kutokana na unga mweupe wa ngano na mchele
  mweupe.

  3. Punguza kula vyakula vitamu sana. Utumie kiwango kidogo sana cha

  sukari, chumvi na mafuta ya kila aina. Epukana na viungo vinavyonukia,
  mafuta ya mgando{grease} hasa mafuta ya nguruwe, hamira,
  mgadiyanayotumika kwa kupikia na siki.

  4. Ule kwa wakati uleule uliowekwa kwa milo kila siku, na acha

  anagalau masaa matano yapite kutoka mlo mmoja hadi mwingine. Mfumo wa
  kuyeyusha chakula unafanya kazi yake vizuri sana ukiwekewa ratiba
  linganifu na uile milo usiku sana.

  5.Usile katikati ya milo. Kula katikati ya milo kunapunguza kasi ya

  tumbo kukitoa chakula kilichomo na kusababisha chakula hiki kuchachuka
  kikiwa bado tumbani.

  6. Ule chakula cha kutosha hasa asubuhi. Hicho ndicho kingekuwa mlo

  wako mkubwa kuliko yote kila siku. Ule chakula chako cha jioni angalau
  masaa mawili au matatu hivi kabla ya kwenda kulala.

  7. Ule chakula unachohitajiili kuhifadhi afya yako, nawe ukifurahie

  ila usile chakula kupita kiasi. Kula chakula kingimno huipumbaza
  akili, huleta uchovu, huongeza magonjwa na kupunguza maisha yako.

  8. Kula polepole na kukitafuna chakula chako vyema kutaongeza furaha

  yako na manufaa ya virutubisho vya lishe hiyo mwilini mwako. Wakati wa
  mlo uwe wa furaha na usiharakishwe, usitafune chakula kwa muda mfupi
  sana, usileusile haraka harakr na usiweke chakula kingi mno
  kinywani.

  9 Unywe maji ya kutosha kila siku ili kuufanya mkojo wako kuwa mweupe,

  lakini usinywe maji pamoja na milo yako ama muda mfupi tu kabla au
  baada ya milo yako. Maji au kinywaji kingine chochote kinachonywewa
  wakati wa milo huchelewesha uyeyushaji na utoaji wa chakula
  kilichoyeyushwa tumboni. Kukaa kwa chakula tumboni kwa muda mrefu
  hukichachusha na hiyo ni mojawapo ya sababu za kawaida sana zinazoleta
  vidonda vya tumbo na ugonjwa wa tumbo{gastritis}

  10. Ruka mlo mmoja mpaka mine kila baada ya kipindi Fulani kupita.

  Kufunga ni msaada wa kuidabisha hamu ya kupenda sana kula chakula na
  tena ni mazoezi ya kuitawala nafsi yako. Kufunga ni dawa bora sana ya
  magonjwa mengi sana, hasa kwa watu wale wasiofanya kazi nyingi na
  ngumu za mikono.

  11. katika mlo wako epuka:

  {a} Pilipili kali zote na viungo vinavyonukia{tangawizi, dalasini,
  karafuu, basibasi}
  {b} siki au kitu chochote kilichotengenezwa kwa siki {achali, mchuzi
  wa mayai uliotiwa mafuta na siki [mayonnaise], kachumbari[catsup].
  Haradali na kadhalika}
  {c}Vyakula ambavyo vinachachuka, vinatoa uvundo, ama vinakuwa katika
  hali ya kuoza wakati wa kuvitayarisha, kama vile, mchuzi mchungu wa
  kabeji iliyokatwakatwa kama kachumbari na kutiwa chumvi ya maji ya
  bahari [sauerkraut], jibini, mchuzi wa soya na vitu vingine kama
  hivyo.
  {d} Magadi, hamira na aina zake zote hasa pamoja na mikate myembamba
  migumu, biskuti, maandazi na vitu vingine vilivyopokwa.
  {e} Kafini [kahawa, majani ya chai, vinywaji vya kola] na chokolet

  12. Usile vyakula vizito sana. Hivi ni pamoja na vyakula vyenye sukari

  nyingi, mafuta yaliyosafishwa sana kwa mashine, vitamini na madini
  zilizotengenezwa ama protini [concentrated proteins] nzito kama nyama
  na vitu vingine vitokavyo na wanyama kama maziwa, mayai na kadhalika.

  13. Matunda na mboga za majani visiliwe katika mlo uleule mmoja na

  usile matunda mabichi sana ama yaliyoiva sana.

  14. Vyakula visiliwe vikiwa bado ni vya moto sana ama vya baridi sana

  na visiliwe mapema zaidi kabla masaa yaliyopangwa kufika.[masaa matano
  kati ya milo]


  2.MAZOEZI YA VIUNGO


  KANUNI ZA MAZOEZI YALETAYO AFYA

  1. Mazoezi lazima yawe ya kuendelea [ya kila siku] ili yaweze kuleta
  manufaa mwilini angalau zitumike dakika 30 kwa siku.

  2. Mazoezi ya viungo hayana budi kuwa mepesi na yasiwe ya kutumia

  nguvu nyingi [kupita kiasi].

  3. Mazoezi ya viungo shart yawe ya aina mbalimbali[kama vile kulima

  bustani] ili misuli yote ya mwili ipate kutumika vizuri.

  4. Mazoezi ya viungo hayana budi fufurahiwa ili yaweze kuleta manufaa

  ya kutosha mwilini.

  FAIDA YA MAZOEZI YA VIUNGO

  1. Mazoezi ya viungo huimarisha mifupa na misuli.


  2. Mazoezi ya viungo yanaharakisha MZUNGUKO wa damu kwenda katika

  sehemu zote za nyama ya mwili wetu

  3. Mazoezi ya viungo huoneza utendaji bora wa moyo


  4. Mazoezi ya viungo huongeza utendaji bora wa mishipa ya damu.


  5. Mazoezi ya viungo yanasaidia kudhibiti ugonjwa wa shinikizo la damu

  [blood pressure]

  6. Mazoezi ya viungo yanasaidia uyeyushaji wa chakula wakati mtu

  anapotembea mara tu baada yam lo akiwa ameinua kichwa chake juu na
  kuyaweka mabega yake nyuma

  7. Mazoezi ya viungo yanachelewesha kuzeeka


  8. Mazoezi ya viungo yanausaidia mwili kuwa na uzito wake unaofaa si

  mnene kupita kiasi wala mwembamba kupita kiasi

  9. Mazoezi ya viungo yanapunguza msongo[stress] unaoleta

  unyong`onyevu[depression] au magonjwa ya akili. Yanamfanya mtu
  ajisikie ameburudika

  10. Mazoezi ya viungo yanauimarisha mfumo mzima wa kujikinga na

  maradhi kwa njia hiyo kuusaidia mwili kutopatwa na magonjwa ya
  kuambukiza pamoja na mafua

  11. Mazoezi ya viungo yanaboresha utendaji wa akili na kukuza fikra

  safi


  3. MAJI
  Mwili unahitaji theluthi zaidi ya majiyanayohitajika wakati wa kiu.
  Utaratibu wa kudumu ufuatao utakusaidia kukidhi mahataji ya maji

  mwilini. Kunywa maji bilauri 2 za maji mara tu unapoamka asubuhi,

  bilauri 2 kati ya asubuhi na adhuhuri na bilauri 2 kati ya masaa ya

  mchana. Unywe maji mengi ya kutosha kuufanya mkojo wako ufanane na

  maji safi. Kumbuka kwamba hali zinazosababisha kupotea kwa maji mengi
  mwilini zinahitaji kufidiwa kwa kunywa maji mengi sana .

  MATUMIZI YA MAJI NDANI YA MWILI

  Mwili uanapendelea maji ya moto kidogo kuliko yale ya uvuguvugu.maji

  yakiwa ya baridi sana yanasimamisha kazi ya kuyeyusha chakula
  tumboni[kama yamenywewa wakati wa mlo] na tena yanazipunguza ishara

  zilizomo mwilini mwetu zinazotujulisha tunapokuwa na kiu. Wakati bora

  wa kunywa maji na ule ulio katikati ya milo. Epuka kunywa maji katika
  dakika 30 kabla ya mlo na saa 1-2 baada kumaliza mlo. Kunywa maji

  pamoja na milo hupunguza nguvu ya uyeyushaji chakula mwilini [enzymes]

  na kuchelewesha uyeyushaji wa chakula hicho. Kama mwili unapungukiwa
  na maji basi mkondo wake wa damu utakwenda polepole na mwili wote
  utaadhirika. Nmatumizi mengine ya maji ni kama ifuatavyo:

  1. Hutengeneza mate kinywani


  2. Hutengeneza machozi katika macho


  3. Hurekebisha joto la mwili kuwa katika kiwango kinacholeta afya

  mwilini na yanasaidia kutelemsha homa

  4. Hulainisha viungo vya mwili[joints] pamoja na misuli


  5. Huzuia na kupunguza uchovu wa mwili

  6. Huzuia na kupunguza uchovu na unyong`onyevu wa mwili

  Vilevile kuoga kila siku na maji ya uvuguvugu au yaliyopoa kuna
  manufaa yafuatayo kiafya:


  1. Kunauimarisha mwili ili uweze kujikinga na mafua na magonjwa

  mengineyo
  2.Kunauboresha mzunguko wa damu mwilini
  3.Kunaburudisha na kuutia nguvu mwili
  4. Kunatia nguvu ubongo, kunauchangamsha akili na kuzituliza neva
  5. Kunaongeza uwezo wa misuli kunyumbuka
  6. Kunavisaidia viungo vinavyoyeyusha chakula [tumbo la chakula, ini
  na matumbo]

  4. MWANGA WA JUA


  FAIDA ZA MWANGA WA JUA

  1. Unaongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini

  2. Unaongeza wingi wa damu inayotoka Moroni


  3. Unaongeza uwezo wa damu kusafirisha oxgen


  4. unasaidia kuratibisha mwilini shinikizo la damu [blood

  pressure] kubakia pale kinapohitajiwa

  5. unaongeza idadi ya chembechembe nyeupe za damu na uwezo wao

  wa kupigana na maambukizo

  6. unaongeza protini iitwayo 'gamma globulin' inayosaidia mwili

  kupigana na maambukizo

  7. unaongeza utendaji kazi wa ini na kuriharikisha kutengeneza

  dawa ya kuyeyusha chakula. Pia inaongeza uwezo wa mtu kustahimili
  mazingira yasiyo safi

  8. unaimarisha viwango vya sukari katika damu mwilini.

  9. unapunguza kiwango cha mafuta katika damu. Mwanza wa jua
  unaweza kupunguza kiwango cha kolestero kwa zaidi ya asilimia 30

  10. Mwanga wa jua unaigeuza kolestero na egestero katika ngozi kuwa

  vitamina D

  11. unaongeza nguvu ya misuli na kuiwezesha kudumu


  12. unaongeza uyeyushaji wa chakula mwilini


  13. ni tiba inayofaa kwa ugonjwa wa manzano wa ngozi na macho

  unaowapata watoto wachanga

  14. unaboresha mtizamo wa kiakili na afya mwilini. Unasaidia kuzuia au

  kuufanya unyong`onyefu wa akili kuwa nafuu zaidi

  15. unapunguza msongo [stress] kwa kufanya kazi kupitia katika neva

  zinazopokea ambazo zimo katika ngozi ya mwili wetu na pia kupitia
  katika mambo ya kisaikolojia yanayochangia

  16. unaendeleza uponyaji. Elekeza sehemu za mwili zilizoambukizwa

  kwenye Mwanza wa jua. Kuota jua kwa muda mfupi mara cada kwa situ
  kunaweza kuua vijidududu vya magonjwa na kusaidia kupona kwa majeraha

  17. unasaidia kuviondoa vijidudu viletavyo magonjwa katika nyumba

  zetu.

  JINSI YA KUYAEPUKA MADHARA YA JUA

  1. pata jua kwa kiwango kidogo kinachoongezeka taratibu. Epuka

  kuunguzwa na jua kama unavyoepuka sumu

  2. punguza kujianika juani wakati wa kiangazi hadi wakati wa

  adhuhuri[ saa4 hadi saa 9]

  3. unapokuwa nje vaa nguo zinazokuhifadhi na kofia pana, nguo

  nyepesi zinaweza kunyonya baadhi ya mionzi ya jua

  5. KIASI

  Kiasi au kujinyima maana yake ni kujikana nafsi, kutumia kwa kiasi

  [sio kupita kiasi kile ambacho ni kizuri na kutotumia kabisa kile

  kinacholeta madhara mwilini. Kiasi kiwe mazoea katika maisha yetu ya

  kila siku :lishe, kazi, kulala usingizi, kujifunza, na kuvaa vizuri.

  Epukana kabisa na nyma iliyo najisi na vitu vyote vinavyoleta madhara

  mwilini kama alkoholi, tumbako[sigara] na vitu vyote vilivyo na

  kafini[caffeine] kama majani ya chai, kahawa na vinywaji vya kola.

  Kuvunja kanuni hii ya afya kuna athari kubwa sana. Kutokuwa na kiasi
  ndio msingi wa maovu yote katika ulimwengu wetu.

  6. HEWA SAFI

  Mwanadamu angeweza kuishi majuma 5 mpaka 6 pasipo kula chakula siku

  chache bila kunywa maji lakini kwa dakika chache tu bila hewa. Hewa

  safi inaburudisha mwili na akili. Mwili unanufaika zaidi kutokana na

  mazoezi yanayofamyika nje ya nyumba kuliko ndani ya nyumba. Hewa safi
  kotoka nje inanufaisha mwili na akili kwa njia zifuatazo:

  1. inafanya damu kuzunguka mwilini na kuleta afya


  2. inaburudisha mwili—inasaidia kuwa na nguvu na afya


  3. inazituliza neva—inafanya akili itulie na kuwa na ukunjufu


  4. inaamsha hamu ya kula chakula na kukisaidia chakula kuyeyushwa

  kikamilifu

  5. inaleta usingizi mzito na mtamu


  KUVUTA PUMZI IPASAVYO

  1. jizoeze kusimama au kukaa vizuri. Simama na kukaa wima na kwa
  urefu. Weak mabega yako nyuma na kuyaelekeza chini. Mitulinga iytakuwa
  imevutwa karibu pamoja jambo ambalo hukisaidia kiwambo cha moyo
  [diaphragm] kufanya kazi yake kwa uhuru

  2. kusoma kwa sauti kubwa humsaidia mtu kuitoa hewa nje ipasavyo


  3. kupanda ngazi za nyumba au vilima humsaidia mtu kuvuta pumzi. Vuta

  hewa ndani kwa hatua mbili, kasha itoe nje kwa hatua mbili zinazofuata
  na kadhalika

  7 PUMZIKO
  Pumzio ni la muhimu kabisa katika maisha yetu- kwa afya ya mwili na
  akili. Badala ya kupumzika na kuacha kazi zote badiliko katika aina ya

  kazi linaweza kuleta manufaa katika afya ya mtu. Kwa mfano kuacha kazi

  ya kutumia akili kwenda kazi ya kutumia mikono inweza kuwa na manufaa
  kwa mwanafunzi. Karibu theluthi ya maisha yetu inatumika kwa kulala

  usingizi. Wakati wa kulala nguvu zaakili hurejeshwa upya. Usingizi

  unaofaa sana ni ule unaopatikana kabla ya usiku wa manane. Kwa
  usingizi bora saa ya kwenda kulala isiwe baada ya saa 4 usiku.

  Tumalala vizuri sana kama tumbo letu pia linaweza kupumzika kutopkana

  na kazi yake ya kuyeyusha chakula angalau masaa 3 baada ya kula

  chakula. Usingizi unaoleta pumziko la mwili unasaidiwa na:

  • chumba kitulivu, cha giza, chenye hewa ya kutosha wakati wote
  • tumbo tupu [angalau saa 3 baada ya kula chakula]
  • kufanya shughuli za mwili za wastani kabla ya kwenda kulala
  • dhamiri safi—moyo ulio na amani na Mungu.
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  I see, elimu kubwa mno bila malipo. Thanks...
   
Loading...