Afurahia kugeuzwa ‘shoga’ mahabusu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afurahia kugeuzwa ‘shoga’ mahabusu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Mar 29, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,180
  Likes Received: 417,601
  Trophy Points: 280
  Afurahia kugeuzwa ‘shoga’ mahabusu

  Imeandikwa na Flora Mwakasala; Tarehe: 28th March 2011 @ 23:05 Imesomwa na watu: 322; Jumla ya maoni: 1


  KATIKA hali isiyo ya kawaida, mshitakiwa katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa akiwa mahabusu anafanyiwa vitendo vya kuingiliwa kinyume cha maumbile.

  Mshtakiwa huyo, Twaha Seif (22) ambaye ni Mbeba mizigo wa Kidongo Chekundu alikiri mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago baada ya mshitakiwa mwenzake, Ayoub Haruna (20) kuiomba Mahakama itenganishe mashitaka kati yake na Seif kutokana na vitendo vyake hivyo.

  Haruna alidai hayo wakati wakisomewa maelezo ya awali katika kesi hiyo namba 512 ya mwaka 2010.

  Alidai hataki kuendelea kusomewa mashitaka na mwenzake Seif kwa kuwa anajihusisha na vitendo vya kuingiliwa kinyume na maumbile vinavyomharibia sifa.

  Alipoulizwa kuwa inamuathiri nini mwenzake kufanya vitendo hivyo, alidai kuwa, anaumia sana kwa sababu mahabusu wenzake wanahisi na yeye anafanya vitendo hivyo kwa kuwa muda mwingi wanakuwa pamoja na hata mahakamani huletwa pamoja.

  “Sifahamiani naye, nimemjua huku huku lakini kwa kawaida mkiwa mnasomewa shitaka moja mnashirikiana na kuwa pamoja kama ndugu hivyo vitendo vyake vinanifanya nionekane nashirikiana naye,” alidai.

  Seif alipoulizwa kama kweli anafanyiwa vitendo hivyo alijibu; “ni kweli afanyiwa…namshangaa mwenzangu kusema hivyo wakati vitendo hivi ni vya kawaida kwa maisha ya mahabusu.”

  Upande wa mashitaka ulipotaka kufahamu kama washitakiwa wanalazishwa kufanyiwa vitendo hivyo, Seif alidai kuwa hawalazimishwi bali wameamua wenyewe kufanyiwa hivyo kwa makubaliano.

  Kutokana na ombi hilo Hakimu Luhwago, alimuagiza Mwendesha Mashitaka Mkuu Naima
  Mwanga aite mashahidi wote wa kesi hiyo ili aisikilize na kuimaliza haraka.

  Upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kesi imeahirishwa hadi Machi 31 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza mashahidi.

  Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Julai 2 mwaka jana saa 5 asubuhi katika mtaa wa Kongo washitakiwa hao waliiba simu yenye thamani ya Sh 40,000 mali ya Farida Ally.

  Kwa mujibu wa Mwanga kabla ya kuiba mali hiyo washitakiwa hao walitumia panga kumtishia Farida ili awape mali hiyo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,180
  Likes Received: 417,601
  Trophy Points: 280
  PHP:
  "Sifahamiani naye, nimemjua huku huku lakini kwa kawaida mkiwa   mnasomewa shitaka moja mnashirikiana na kuwa pamoja kama ndugu hivyo   vitendo vyake vinanifanya nionekane nashirikiana naye," alidai.   
   
  Seif alipoulizwa kama kweli anafanyiwa vitendo hivyo alijibu"ni  kweli  afanyiwa…namshangaa mwenzangu kusema hivyo wakati vitendo hivi ni  vya  kawaida kwa maisha ya mahabusu."  
  OH.............................GOD have mercy on us.....................
   
Loading...