mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Taarifa za wazungu zinasema huko Ulaya hususani Uingereza (kwa mujibu wa BBC Kiswahili jana), watu weusi na wenye asili ya Asia eti ndio wanaokufa zaidi na korona kuliko wazungu.
Hii haijakaa vizuri na inabidi Afrika kushtuka mapema!! Hii ni kwa sababu inapingana na uhalisia wa mambo jinsi ulivyo:
1. Kwanza China kwenyewe ambako ugonjwa ulianzia, kuna watu weusi wengi tu. Lakini takwimu zao zinaonyesha kuwa watu weusi hawakuathirika/hawakufa sana kutokana na ugonjwa wa korona. Kinyume chake ni kuwa asilimia kubwa ya watu waliokuwa na korona lakini hawana dalili zozote za ugonjwa ni watu weusi. Hicho ndicho kilichopelekea kuamua kuwapima waafrika kwa lazima. Nadhani wote mnakumbuka sekeseke hilo hadi wakuu wa nchi za Afrika waliilalamikia China rasmi.
2. Pili hapa Afrika idadi ya vifo vya watu weusi ni vichache sana. Sehemu ya Afrika iliyoathirika kidogo ni Algeria, Misri, Tunisia na Morocco. Na wote mnafahamu nchi hizo ni Waafrika wasio weusi.
3. Vifo vya nchi zote za Afrika mpaka sasa hazijafikia hata vifo vya siku mbili tu vya Marekani japo idadi ya Waafrika ni zaidi ya mara tatu ya idadi ya Wamarekani wote.
Baada ya kutoa maelezo haya inawezekana kabisa:
1. Watu weusi wakiugua korona huko Ulaya na Marekani hawapewi huduma inayostahili ndiyo maana wanakufa zaidi. Kwa nini waugue zaidi na wafe ulaya na Marekani tu?
2. Wanaweza kupandikiziwa hata korona hiyo! Kama wamarekani wanaishuku china kwa nini na sisi tusiwashumu wao?
3. Inawezekana tunataka kuaminishwa kuwa waafrika ndio tutakuwa wahanga wakubwa wa corona. Wakifanikiwa kutuaminisha hivyo watakuwa wameandaa mazingira ya kutumaliza baadaye halafu wasingizie corona na kusema si tuliwaambia waafrika ndio wanakufa sana?
4. Kwa mazingira hayo, tujihadhari sana hata na dawa na chanjo za wazungu!! Si mnakumbuka hata wazungu wengine bila aibu walisema chanjo ifanyiwe majaribio kwa waafrika!!
Kwa upande wangu nitasubiri chanjo itakayogunduliwa na waafrika. Na niwaombe wataalam wetu hasa NIMRI waanze mchakato wa kutafuta chanjo ya corona na Serikali iwawezeshe. Wataalam tunao na ninaomba tuwaamini na tuwawezeshe.
Hotuba ya Rais wetu wakati anamwapisha waziri wa sheria ina vitu vizito sana na itupe tahadhari sana. Hii ni vita kubwa!! Wazungu wanatazamia miili ya waafrika isambae mitaani!! Halijatokea hilo na watajitahidi litokee. Tuwe macho!!