Afrika pumbavu

Afrika pumbavu

Ila kuita waafrika na vijana wake wapuuzi na wanaupuuzi ndio solution? Nilijua tu.. wewe ni kijana mdogo.. ambae hata hufai kutumia kauli ya mabinti zetu.. huna binti bado. Jifunze maisha ndio uje kuropoka.
Next viwanja vya vita mfano wake nenda machimboni huko ukaone vijana wenzako wanavyopambana..
Nenda kkoo kaone vijana wanavyochakalika.
Nenda hata huko south ukaone vijana wenzako wanavyopambana ..
Nenda dubai, nenda hapo tu uk kaangalie vijana wakiafrika, wakitanzania wanavyochakarika.
Unakuja kuongelea jamii forum hapa.
Kijana fikiria kabla ya kuropoka.(Narudia tena)
Aisee we jamaa acha nikuwie radhi tu maana nahisi utakuwa mpambanaji.
Ila tatizo tu unataka kuanza kuvunjiana heshima hapa.
 
Na Libya ikiwemo au....?
Libya, tunisia,Misri, Morocco hizi ni nchi za kiafrica za waarabu,au waarabu wa Afrika, tofauti kabisa kimaendeleo na nchi za afrika ya weusi.
Kilichowasaidia ni dini ya kiislamu kwa maana katika uislamu waumini wote ni sawa mbele ya Mola wao,hii imewakaa akilini hata watawala wao hofu ya kutowatendea mabaya wanaowatawala,hata hapa nchini muislamu akishika usukani angalau wananchi wanapumua.
Uislamu umewasaidia kuepuka mambo ya riba,rushwa,ufisadi na ulafi pia.
 
Kila
Na Libya ikiwemo au....?
Kila nchi ina aina za matatizo yake, kati ya niliyoyaainisha hapa. Walau kutokana na Sheria ngumu nchi nyingi za kiafrika zenye wakaazi waarabu zimetulia katika upuuzi huu, ijapokuwa na wao Wana aina zao za matatizo ambayo sisi atuwezi kuyamudu.
 
Nisiwe mnafki sana kuhusu jambo hili, nchi nyingi za kiafrika tunafanana sana Mambo yetu. Yaani unayoyaona hapa nyumbani ndio hayo hayo yapo Burundi, Kenya, Nigeria, South Sudan, Afrika ya kati na hata South Afrika nchi iliyopiga hatua kidogo kwa Afrika.

Aisee ni upumbavu kuona et- watu maarufu nchini ni wachekeshaji, waimbaji, na wapuuzi puuzi tu wenye kufanya maupuuzi huko mitandaoni na unakuta wanapata wafuatiliaji mamilioni kwa mamilioni, wapumbavu hawa wasio jitambua

Sasa unakuta li-kijana limemaliza chuo alafu linalalamika ajira hakuna huku ukiliuliza unaijua hata jamii forum haijui, hana chochote cha zaidi ya kuwa-follow akina juma lokole na kujua ratiba zote za vipindi vya kipuuzi huko median.

Nimechunguza nikagundua kati ya vijana 10 tisa kati yao hawaitumii jamii forum, zaidi ya kukutana nayo hewani wakati wakiwa wame-google kitu flani. Yaani kwa maamuzi yao hii App sio kipaumbele .

Kujirekodi na kuweka status za kipuuzi puuzi ndio fashion. Sasa jitu hili utaliajiri kweli? Huko vyuoni ni upuuzi tu, elimu mbovu ubishololo umetamalaki, kutafunana tu hadi tunaogopa kupeleka mabinti zetu.

Snap chat, Facebook, Instagram, na kuangalia YouTube chanells za udaku ndio habari ya mujini na vijijini kuliko pelekwa umeme kwa kodi zetu na majasho yetu. Angalia Sasa ni nini wanaposti na kuweka umo, Ni ujinga ujinga tu wa viwango vya kimataifa.

Kwakweli tusimtafute mchawi wala kumsingizia mkoloni ua mabebelu, maana ujinga ndani yetu ukiona nchi watu wake maarufu na role model wa watu ni waigizaji, wachekeshaji, machawa, machangu, na waimbaji wa ovyo ovyo basi ujue hakuna kitu hapo.... Ni mzigo kwa Dunia tu.
Leo umecharuka sijui nani amekuudhi.
 
Akina Masanja ndio wanategemewa kuongea siku ya Uhuru wa Tanganyika na makamu wa Rais hana nafasi.
Afrika bado sana
 
Akina Masanja ndio wanategemewa kuongea siku ya Uhuru wa Tanganyika na makamu wa Rais hana nafasi.
Afrika bado sana
Wale wawili walichaguliwa kwa kigezo cha uanaccm, ile ndiyo top cream ya wachekeshaji wa CCM!
 
Back
Top Bottom