Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,896
- 3,206
Afrika ni bara tajiri sana duniani.
Lina rasilimali za kila aina kuanzia ardhi nzuri inayofaa kulima mazao ya kila aina, maji, hali nzuri ya hewa, uoto wa asili ikiwemo misitu, madini, mafuta, gesi n.k.
Viwanda vingi duniani vinaendeshwa na raw-materials toka Afrika.
Cha kustaajabisha, nchi nyingi za bara hili, hasa zile za kusini mwa jangwa la Sahara, wananchi wake wanaishi katika umaskini uliokithiri!
Hali hii ya umaskini kwa wananchi wa nchi hizi za Afrika, kwa sehemu kubwa zimechagizwa na viongozi.
Viongozi wengi wa bara hili wakishachaguliwa, kwanza huanza kujinufaisha wao na watu wao wa karibu na kuwasahau wananchi waliowaweka pale.
Wengi wa viongozi wetu, ni matajiri wa kutupwa duniani pamoja na kwamba wengi wao, huficha fedha katika nchi zilizoendelea kama vile Ulaya, Amerika Kaskazini, na kwa sasa Asia (Dubai, Singapore n.k).
Kama kweli viongozi wote wa Bara hili wangekuwa wazalendo kwa nchi zao, basi ingetuchukua tu miaka 20 kuzibadilisha nchi zetu hizi toka hapa tulipo hadi kufikia angalau uchumi wa kati.
Lakini jambo la kushukuru ni kwamba nchi nyingi za Kiafrika, vijana wameanza kuamka na kuwakataa viongozi mafisadi.
Hili vuguvugu limeanzia huko Guinea, Mali, Burkina Faso, Niger na tusishangae kuliona likisambaa sehemu mbalimbali za Bara hili zenye viongozi washenzi ambao wako kimaslahi yao badala ya kuwatumikia wananchi wao.
Mungu libariki bara letu pendwa la Afrika.
Tusaidie pia kwa kutuondolea viongozi wa hovyo wasiowapenda watu wao na nchi zao;
Amiin.