Afrika Mkwe Anapokuja Dukani Kwako....!

Afrika Mkwe Anapokuja Dukani Kwako....!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu,
Inahusu mila na tamaduni. Unafanyaje unapokuwa na duka na mteja aliye mbele yako ni mama mkwe wako?

Mwalimu, Profesa Mbele ameligusia hili la mila na destruri za Kiafrika kwenye kitabu chake kiitwacho African and Americans; Embracing Cultural Differences.

Kijinini unapokuwa na duka usifikiri tu hesabu za faida ya kibiashara, kuna hesabu za faida za kijamii pia.

Kawaida mama au baba wa mke ulimuoa haji mwenyewe dukani kwako. Atamtuma mtu. Lakini siku ukimwona mkweo amekuja mwenyewe ujue nyumbani mambo hayajakaa sawa.

Atakutajia mahitaji yake. Atajifanya pia yuko tayari kukulipa. Lakini, unachotakiwa kufanya, ni kuchukua mahitaji yote ya mkweo. Kisha utoka kabisa nje ya duka kumkabidhi mwenyewe kwa mikono yako. Naye atajaribu kufungua mkoba wake atoe pesa. Umwombe radhi haraka, kuwa siku hiyo usingependa atoe hata senti tano!

Na usipofanya hivyo, mkwe atakuona kuwa ni mwanamme usie mwelewa wa mila na desturi.

Maana, Afrika mkwe hawezi kuja mwenyewe dukani kwako, na akija, ujue kaishiwa....Usisubiri akwambie!
Ni Neno Fupi La Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz
 
Kwa sisi wengine hela ndo kila kitu, unamsubiria, akitoa unpokea. but akileta story ndo uje tyr kidonda
 
Fasihi nzuri sana ukiielewa. Asante kwa somo.
 
Enzi hizo wakwe walipokuwa na adabu pia,hawa wa siku hizi na mizinga ya kufa mtu wala usiwajaribu!
 
Back
Top Bottom