Afrika Mashariki yafuta ushuru wa forodha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika Mashariki yafuta ushuru wa forodha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mallaba, Feb 26, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  WAFANYABIASHARA wa nchi sita wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, sasa wako huru kuvuka mipaka na kuuza bidhaa zao bila kulipa ushuru wa forodha katika eneo hilo linalokadiriwa kuwa na zaidi ya watu 120 milioni.

  Hatua hiyo inakuja baada ya kuondolewa kwa vikwazo vilivyokuwa vinasababisha kero katika ama kuzalisha au kuagiza mali ghafi na kusambaza bidhaa katika nchi hizo za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

  Hatua hiyo inalanga katika kuleta ustawi wa kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

  Hali kadhalika, kuboresha biashara, kuwapatia walaji bei nafuu na kuongeza nguvu ya ushindani katika uzalishaji wa bidhaa za ndani dhidi ya wale wa nje ya ukanda wa Afrika Mashariki.

  Mkakati huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na Uzalishaji katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Amantius Msole.

  "Ni nafasi nzuri kwa Watanzania kutumia fursa hii ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa za kilimo na viwanda kwa lengo la kukidhi mahitaji ya Jumuia ya Afrika Mashariki," alisema Msole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema mfanyabiashara yeyote atakayekumbana na vikwazo akiwa anauza bidhaa ndani ya nchi wanachama, anapaswa kutoa taarifa kwa kamati za kitaifa na kikanda, zilizoundwa na jumuia ili apatiwe haki.

  Alisema Itifaki ya Umoja wa Forodha, sasa imepewa nguvu ya kisheria na kwamba tayari jumuiya imeanzisha utaratibu wa kutambua vikwazo visivyo vya kiforodha, ili hatimaye, viondolewe.

  Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,ratiba ya kuondoa vikwazo hivyo imekwishaandaliwa.

  Msole alisema Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, umeweka kanuni mbalimbali zitakazosimamia fursa za kibiashara kwa bidhaa na malighafi zinazozalishwa au kuagizwa ndani na nje ya nchi wanachama.

  Kuhusu bidhaa zinazozalishwa katika nchi za Afrika Mashariki, alisema jumuiya, imeondoa ushuru wa forodha kwa bidhaa zote zinazokidhi vigezo vya kusajiliwa.

  "Kuondolewa kwa ushuru wa forodha, kumevutia na kuchochea uwekezaji wa ndani na nje ya jumuia katika sekta ya viwanda na kilimo na kurahisisha upatikanani wa mali ghafi," alisema Msole.

  Urasimu wa watendaji wa Forodha

  Kwa kufahamu kuwa bado baadhi ya watendaji wa forodha wanaweza kuweka mazingira yatakayosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara, alisema jumuiya imeweka utaratibu wa kisheria wa kupambana na hali hiyo.
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hii itasaidia sana kupunguza gharama zisizokuwa na maana sana.
   
Loading...