Afrika Kusini niijuavyo mimi

Afrika Kusini niijuavyo mimi

Untold story: Safari yangu kurudi South 1998
Hiki kipande ni kirefu na sijawahi kukisimulia .. Naona leo nitafanya hivyo.. Get ready
Wengine wakati tunanyonya wengine tayari mshaanza safari ya kuacha simulizi🥲
 
Naendelea sasa..!
Mwaka 1998 nilirudi Tz likizo kwa mara ya kwanza.. Ile kumaliza likizo nikaugua malaria na kulazwa siku moja kabla ya safari.. Hivyo shirika la ndege Alliance airline bythen wakakata almost 40% ya ticket na kunidushia pesa iliyobaki

Baada ya kupona nikawa sina nauli ya kutosha kupanda ndege hivyo nikaondoka na treni mpaka Kapiri Mposhi Zambia (hii safari ikawa na vituko vyake vingi sitavisimuia hapa)

Tuliondoka Dar Ijumaa jioni pale Tazara na kufika salama Zambia Mji wa Kapiri Mposhi Jumapili asubuhi
Pale nikachukua basi mpaka Lusaka na kufika mchana.. Nilipata hotel nikalala mpaka kesho yake siku ya Jumatatu

Nilienda stand na kufanikiwa kupata basi la South kupitia Zimmbwe.. Nikiwa ndani ya bus nikakutana na jamaa yangu mkenya naye katoka likizo.. Safari ikaanza
Tulisafiri mchana kutwa mpaka jioni tukafika mpakani mwa Zambia na Zimbabwe
 
Naendelea sasa..!
Mwaka 1998 nilirudi Tz likizo kwa mara ya kwanza.. Ile kumaliza likizo nikaugua malaria na kulazwa siku moja kabla ya safari.. Hivyo shirika la ndege Alliance airline bythen wakakata almost 40% ya ticket na kunidushia pesa iliyobaki

Baada ya kupona nikawa sina nauli ya kutosha kupanda ndege hivyo nikaondoka na treni mpaka Kapiri Mposhi Zambia (hii safari ikawa na vituko vyake vingi sitavisimuia hapa)

Tuliondoka Dar Ijumaa jioni pale Tazara na kufika salama Zambia Mji wa Kapiri Mposhi Jumapili asubuhi
Pale nikachukua basi mpaka Lusaka na kufika mchana.. Nilipata hotel nikalala mpaka kesho yake siku ya Jumatatu

Nilienda stand na kufanikiwa kupata basi la South kupitia Zimmbwe.. Nikiwa ndani ya bus nikakutana na jamaa yangu mkenya naye katoka likizo.. Safari ikaanza
Tulisafiri mchana kutwa mpaka jioni tukafika mpakani mwa Zambia na Zimbabwe
Enheee..! 👂
 
Naendelea..
Pale mpakani Chirundu ukaguzi wa mizigo na nyaraka za safari ukaanza kwa abiria wote
Sasa tukiwa kwenye bus kabla ya kufika boda yule jamaa yangu alinitambulisha kwa kijana mwingine mkenya akasema tuko naye safari moja

Sasa tukiwa kwenye foleni ya ukaguzi nyuma yangu alikuwa yule mkenya mwingine na jamaa yangu akawa kama mtu WS a tano nyuma

Kwenye ukaguzi nikakutwa na kanda 5 za kaseti za mziki... Kea kipindi hicho ukiwa na kitu ambacho unaingia nacho Zimbabwe on transit unakilipia ushuru kabisa na ukitoka nacho kuingia South unarudishiwa prsa yako

Enzi hizo zawadi kubwa ya kuwapelekea wabongo south ni kanda za mziki wa Kongo.. Bongo fleva haikuwepo.. Kama huna hela ya kulipia vitu unaviacha boda
Vilevile kulikuwa na sharti la kuwa na pesa ya Zimbabwe Zimdollar 50+.. Yule mkenya nyuma yangu akawa kapungukiwa 30 akaniomba nimuongezee tukifika South atanirudishia... Nilimpatia lakini lilikuwa bonge la kosa!

Sisi tukavuka lakini jamaa yangu akapata shida
Kwanza alitaka kuwahonga maafisa ili apitishe mzigo wake bila kulipa ushuru .. Alikuwa na kanda kama 20 hivi
Pili hakuwa na Zimdollar za kutosha kuonesha pale boda..

Walimruhusu kupita hivyohivyo lakini kumbe ulikuwa ni mtego kwani tulipofika boda ya kuingia South alikamatwa na police tukamuacha hapo

Sasa ndio nikaja kujua yule mkenya mwinginen hiyo ndio ilikuwa safari yake ya kwanza kwenda South na alikuwa boonge la mbutika.. Hata Nairobi kafika wakati anakuja South

Kutoka Zimbabwe sasa kwenda South nikakaa naye siti moja. Alikuwa anashangaa almost kila kitu.. Mbutika.. ! Mbutika kweli😂 mpaka kiswahili chake cha msukuma kinasubiri.😀🙌🏿

Tulisafiri siku nzima mpaka usiku wa saa moja ndio tunaingia Pretoria. Mimi ilikuwa nishukie hapo lakini nikashindwa kwakuwa huyu mbutika nilikuwa namdai na amesema tukifika ndugu yake anayekuja kumpokea atanirejeshea pesa yangu

Mwendo wa kama nususaa hivi tukaingia Johannesburg kitongoji cha Hillbrow ilipo stand ya mwisho!

Hillbrow ndio ilikuwa inaongoza duniani kwa usalama mdogo.. Yaani kila aina ya ubaya iko hapo
Ujambazi
Wizi
Uporaji
Utapeli
Umalaya
Ushoga
Mauaji
Nknk..
Nitaendelea..
 
Naendelea....
Pale ndani ya basi tukatangaziwa kwamba Ndio tunafika mwisho wa safari na kama ndio mara ya kwanza kufika South makinika kwa kila kitu
Basi tukashuka hapo Hillbrow ni mtaa kama pale Buguruni kasoro magorofa barabara nzuri na manfhari tofauti Ila palikuwa busy na nyomi ya watu
Kwa mshangao wangu yule mkenya alikuwa na begi refu limejaa mavitu kama yale mabegi ya watalii.. Nikamuuliza umebeba nini humo akasema ni nguo😂
Kwa haraka nikaangalia sehemu yenye nafuu ya usalama nikaona jengo refu lenye mataa ya rangi mbele limeandikwa Egoli hotel.. Nikakimbilia hapo

Nilikimbilia hapo kwakuwa wakati huo ITV kulikuwa na tamthilia maarufu ya Egoli😀
Tukaingia mpaka veranda penye sehemu za kupigia simu

Mimi na briefcase ndogo mwenzangu na libegi lake.. Tulionekana ni wageni kwa asilimia 1000
Sasa kwa pembeni yake ndio palikuwa na geti la vyuma na mabounsa.. Hapo ndio unapita kwenda juu kwenye bar, casino na nyumbani
Ulinzi na ukaksi uliokuwepo pale getini unatosha kabisa kukwambia hapo mahali pakoje

Watu waliokuwa wanaingia pale wote ni watu wa kazi wa jinsia zote.. Sasa wakati tunahangaika kufanya mawasiliano na watu wa kuja kutupokea, yule mkenya akawa hampati mwenyeji wake! 🙆🏿‍♂

Hakuna watu waliingia pale wakaacha kutushangaa. . yule mkenya ndio alikuwa anashangaa zaidi. Imagine wanawake wa ki South na mishepu yao halafu wote wamevaa nusu uchi

Basi kuna mabinti wawili waliingia wakaenda mpaka getini wakaingia ndani lakini muda kidogo wakatoka na kutufuata pale tulipo sehemu ya kupigia simu

Yule mmoja akazuga kama katuzimia na kutukumbatia kushoto na kulia akatusogeza pembeni na kuongea haraka na kwa sauti ya chini

Akasema nyie ni wageni hapa na tayari mnaliwa timing muibiwe kila kitu.. Mimi ni mrundi sio msouth sitaki mpate shida nilizopata.. Je mtahitaji msaada wangu!?

Kwa haraka mimi nikamwambia niko sawa kasoro huyu mwenzangu... Basi akataja jina lake na kusema yeye anatangulia juu baada ya dakika kumi amfuate

Jamaa baada ya dakika 8 hivi akaenda pale getini na kuingizwa ndani na libegi lake! Sijui alimkuta wapi huyo dada, casino au bar? Lakini kwangu hiyo ndio ilikuwa mara ya mwisho kumuona🥺🙇🏿‍♂
 
Naendelea...
Baada ya jamaa kutokomea juu kulikokuwa na kelele nyingi na mziki nzito Mimi nikatoka kwenda kununua vocha maana ya kwanza ilikuwa imeisha.. Briefcase yangu niliwapa pale geti Kali wanichungie

Vocha zilikuwa zinauzwa hatua 20 hivi kutoka pale hotelini.. Hulk nje kote ilikuwa na watu na vibiashara vya sigara njugu bazoka nknk
Nikiwa hatua kama tano hivi wakati narudi nikashuhudia kwa macho yangu kuna muuza sigara anakula bomba! Risasi mbili za kifuani na kuanguka chini
Chap watu wakatawanyika na kumuacha marehemu anamalizia kukata roho
Nilitimua mbio mpaka pale hotelini nikiwa nimejaa kihoro

Baadae kuja kuuliza sababu ya jamaa kuuliwa nikaambiwa muuaji aliomba sigara akapewa moja wakati yeye alitaka apewe pakti nzima.. Yule muuzaji alipogoma akala chuma jamaa akachua pakti akasepa.. Nikaambiwa hayo ni matukio ya kawaida Sana pale hill brow.. Nilichoka kabisa!
 
Endelea mkuu...hizi story za kusafiri zinanimalizia sana mabando yangu kule youtube....nazipenda sana yan
 
Naendelea sasa..!
Mwaka 1998 nilirudi Tz likizo kwa mara ya kwanza.. Ile kumaliza likizo nikaugua malaria na kulazwa siku moja kabla ya safari.. Hivyo shirika la ndege Alliance airline bythen wakakata almost 40% ya ticket na kunidushia pesa iliyobaki

Niongoze ilipoendelea ya pili
 
Endelea mkuu...hizi story za kusafiri zinanimalizia sana mabando yangu kule youtube....nazipenda sana yan
Basi nikiwa bado na kihoro cha lile tukio nikaendelea kuwasiliana na mtu aliyekuwa anakuja kunipokea ..Alikuwa ni raia wa nje

Akanieleza kwamba hapo nilipo ndio palikuwa kitovu cha matukio yote mabaya na ya kutisha, hivyo tukapeana muda kwamba exactly baada ya dk 10 nikamate briefcase yangu nitoke nje
Hapo atakuwa amefika, then nitapanda na tutaondoka! Pale kwenye simu upande wa pili kwenye kona walikuwepo watu wawili, ni kama walikuwa wananilia radar hivi
Basi dakika 9 na nusu nilikamata briefcase na kutoka nje kwa kasi.. Nafika nje kuna VW Jetta inasimama
Nilifungua mlango nikaingia kwa kasi na dereva akaamsha kwa spidi
Ninachokumbuka ni kuwaona wale jamaa wameshafika mlangoni mwa ile hotel na kubali kuninyooshea vidole huku wakitikisa vichwa😂

Mwenyeji wangu alikuwa mwanamke mwenye stamina nzuri na usukani. Akaniambia mumewe ana mwezi tangu auliwe viunga vya huo mji

Akaniambia mtu mwingine asingejaribu kufika pale nilipokuwa tens usiku kakini yeye alijitoa mhanga ili kuokoa maisha yangu kwakuwa pale nilipokuwa nisingepona

Tulifika kwake salama nikapata huduma zote muhimu nikalala vizuri na kesho yake akanipeleka chuoni

Yule Mkenya classmate wangu hakuwahi tena kufika south bali baada ya kumalizana na uhamiaji walimrudisha boda akarudi Kenya lakini baadae alijilopua tens na kukimbilia Sweden anapoishi mpaka Leo

Yule niliyemuacha pale hotelini sijawahi kujua chochote tena kumhusu..!
Sasa hiyo ilikuwa 1998 imagine sasa hivi South pakoje!
 
Back
Top Bottom