Afrika kusini na ajira

Afrika kusini na ajira

kondeni

Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
5
Reaction score
0
Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi zilizoendelea kwa sekta ya viwanda duniani. Kwa ninavyofahamu miaka ya nyuma vijana wengi walikuwa wanakwenda tafuta ajira huko. Naomba uliza je kwa sasa nafasi za ajira iko vipi? Zipo au hazipo,je kuna wanaokwenda tafuta ajira bado ?
 
Wapo wengi wanaokwenda kutafuta ajira S.A ila wanachokipata ni Umauti.....wanauliwa sana na vijana wa S.A wavivu kufanya kazi wakiona mgeni anafanikiwa kwa kuchapa kazi kwa bidii wanampiga chuma!!
 
Sio sehemu nzuri kwenda, nimeishi huko miaka kadhaa nikaona hakuna dili nimerudi bongo mambo tambarare, nakushauri komaa hapa hapa Bongo opportunities zipo nyingi sana mkubwa.
 
Ucjaribu futa mawazo hayo. hakufai hata mchana wanakutoa uhai ukiingia kwenye anga zao.
 
mbona bongo ajira zipo za kutosha tulia kijana na ujitume
 
Kama huko south kuna watu nenda tu,ni rahs kufanikiwa ukiwa nje ya kwenu,utulie tu usiwe mgomvi uyasome mazingira
 
Sio sehemu nzuri kwenda, nimeishi huko miaka kadhaa nikaona hakuna dili nimerudi bongo mambo tambarare, nakushauri komaa hapa hapa Bongo opportunities zipo nyingi sana mkubwa.

hivi kama passport ikiisha muda ili kuongeza muda zaid unaenda wapi
 
hapa kuna machupa kibao watu wanakunywa maji plz hauitaji mtaji wowote wahi asubui okota kufka jion unapata mshiko wa maana huko sauz sio kabisa
 
Back
Top Bottom