Afrika Kusini: Mzozo kuhusu makampuni ya Mandela

Afrika Kusini: Mzozo kuhusu makampuni ya Mandela

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo ya habari nchini humo.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1
Mmoja wa wasaidizi hao, ambaye pia ni wakili wa Mandela, George Bizos,amekana madai hayo.
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya mapafu.
Mandela alilazwa hospitalini mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jinala Mandela hususan picha alizokuwaanachora akiwa jela.
Makaziwe na Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa bwana Bizo, waziri wa nyumba, bwana Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene, hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings, kulingana na gazeti la Star.
Pesa zinazotokana na makampuni hayo zinapaswa kuwafaidi wanawe Mandela na yeye mwenyewe.
"Bizos, Chuene na Sexwale hawakuwahi kuteuliwa rasmi kama washika dau katika kampuni hiyo.''
Bwana Bizos, wakili anayeheshimikasana na ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa bwana Mandela, alisema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo.
Aliongeza kuwa wanawe Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa .

CHANZO: BBC
 
Back
Top Bottom