Kabla ya haya mambo ya smartphone, vijana wa kipindi hicho wapenda mambo ya siasa na mambo ya dunia tulikuwa hatubanduki DW Swahili, BBC Swahili na VOA.
Nakumbuka Jumamosi moja hivi miaka ya 2000-2005 (Nimesahau mwaka kamili, nakumbuka tu nilikuwa sekondari).
Siku hiyo nilikuwa nasikiliza dira ya dunia DW Swahili kupitia Radio Free Afrika saa saba mchana. Kulikuwa na makala ilikuwa inaelezea jitihada za maendeleo Afrika. Mtangazaji akamtaja mchumi mmoja wa kizungu akisema kuwa, Afrika angalau itakuwa na maendeleo kama Ulaya ikifikia mwaka 2070.
Kumbuka ilikuwa imebaki kama miaka 65, yaani kutoka 2005-2070. Nimejaribu kui-google hiyo habari angalau nipate huyo mchumi lakini sijaipata.
Vipi unaonaje jitihada zetu Afrika, hasa kusini mwa jangwa la sahara? Je, juhudi zinafanyika na kufikia utabiri wa mchumi yule? Kumbuka imebaki miaka 45 kutoka sasa ili ifike mwaka 2070!
Kwenu wataalamu wa uchumi!