Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,619
- Thread starter
- #41
Kada Chilla.Huu mfumo ni wa Dunia nzima...
Hakuna nchi iliyo salama na haya mambo... hakuna binadamu mkamilifu
Tumeona mengi sana kuanzia huko kwa nchi za asia, nchi za ulaya na marekani
Mifano ni mingi sana... Juzi sakata linalo endelea ni kumuondoa mwana mama wa umoja wa ulaya kwa kula rushwa kutoka uarabuni huko
Wakina Platin na Blatter wameondolewa kwa kashfa kama hizo
Wakina messi, neymer nk wamekutwa na makosa yanayo fanana na hayo
PSG imevunja sheria mbalimbali za financial lakini kwa nguvu ya pesa imeweza kukwepa lungu...
Korea na japan wamekutwa na mambo kama haya sana, huko amerika ya kusini ndio balaa...
Urusi tume jionea kwa vipindi tofauti vya kiutawala kwa kurejeshana madarakani kishikaji ili kuendelea kula nchi...
Na nchi zingine za western europe...
Rais na councellor schortz wa ujerumani wana chunguzwa kwa viashiria kama hivi, hasa bwana schortz kipindi alikuwa kiongozi pale hamburg...
Familia za kifalme kuanzia uingereza, spain, uholanzi nk zina pigwa vita na wananchi wao sababu ni hizi za kujilimbikizia mali na madaraka...
Huko marekani kuanzia CIA mpaka ikulu ni majanga matupu... mabosi kadhaa wa CIA walisha wahi kukutwa na tuhuma kama hizo, na marais kadhaa walitumia vyeo vyao vibaya kama huyu ndugu Trump kukwepa kodi nk...
Haya mambo ni dunia nzima... sema wengine wana shindwa kucheza karata zao vyema ndio maana wanakutwa na majanga kama wakina
Al bashir kakutwa na mapesa ndani
Wakina gadaf
Huko misri tunisia na kwa mfalme wa morocco ni yaleyale kama ya nchi zingine na urusi juzi walivyo kuta pesa za tani kadhaa kwenye shangazi kaja...
Waafrika tuna jizalau sana... dunia ni hii hii haina yofauti, yofauti ni jinsi ya kujilemba lakini ndani huko takataka ni zilezile, mavi, mikojo, kamasi, mate nk
Huko kwa wakoloni wetu haya yapo:-
1. Wasio na kazi wanalipwa.
2. Wazee hawaelemei watoto wao, wanalelewa na serikali na mashirika binafsi.
3. Hakuna njaa huko.
4. Kuna uhuru wa habari na maoni.
5. Matokeo ya kura za urais yanahojiwa na kupingwa ILI WAPATIKANE WATU SAHIHI WA KUCHAGIZA MABADILIKO UNAYOSEMA.
6. Huwezi kutuhumiwa ukaendelea kukaa kwy dhamana yako.
7. Kodi zinaogopwa zaidi ya sadaka zinavyoogopwa.
8. Hawakopikopi kama Afrika.
9. Ubelgiji ni kama Rwanda kwa ukubwa, ina rasilimali kidogo kulinganisha na Afrika ambayo pekee ina nusu ya rasilimali za sayari nzima lakini GDP ya Ubelgiji pekee ni zaidi ya GDPs za nchi zote 55 za Afrika ukiweka pamoja.
NB.
Afrika tuanze kuamini kuwa dhambi za Mzungu kwa Mungu ni afadhali (zinamnukia kama waridi) kuliko sadaka za Mwafrika. Mzungu mmoja aliwahi kunikebehi akasema sisi kwy Kiswahili tunawaita wao Mzungu, akaniambia ebu sasa ondoa herufi z kwenye neno Mzungu alafu ulisome.
Afrika tumelogwa na nani?