Afrika imekubali kutukanwa?

Afrika imekubali kutukanwa?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,646
Reaction score
10,859
Afrika ni ara zuri. Limebarikiwa rasimali kede kede, lakini haziwanufaishi wananchi wake.

Afrika ni bara kubwa. Lina mchango mkubwa sana kwa mataifa mengi ya Magharibi, hasa katika suala zima la malighafi na nguvu kazi.

Katika miaka ya hivi karibu, kumeibuka baadhi ya watu walioonesha dharau za wazi kwa bara la Afrika.

Madhalani, mwaka 2018, aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, alizitukana nchi za Kiafrika kwa kuziita SHITHOLE COUNTRIES.

AU ilielezea kuchukizwa na hilo na kumtaka Trump kuomba msamaha. Sijui kama "agizo" lao lilitekelezwa au lilichochea matusi zaidi.

Kwa tusi hilo, Afrika haikuwa na uwezo wa kuchukua hatua zaidi ili kuonesha ulimwengu kuwa siyo Shithole countries kama Trump alivyoudanganya ulimwengu?

Kioja kingine ni kile kilichofanywa na Mwafrika kutokea nchini Ghana mnamo mwaka 2022. Mfanyabiashara huyomaarufu, Dr. Kofi Asamoah, "alizua" taharuki kwa kumshauri Elon Musk alinunue bara la Afrika na kisha "kuwadelete" viongozi wake wote.

Sikusikia kama AU ilitoa tamko kumkemea Dr. Kofi, au hata nchi yake "kumshikisha" adabu.

Inamaana kwamba Afrika ilishindwa "kumshughulikia" hata raia wake aliyeikejeli? Au tuseme alichosema huyo mfanyabiashara tajiri kina "kaukweli" ndani yake?

Afrika ilishadharauliwa na Wazungu, lakini ni sawa na Waafrika nao kujidharau? Hizo dharau mpaka lini?
 
NGOZI NYEUSI Ina LAANA....

ANGALIA Kongo hizo vita za wenyewe kwa wenyewe ni LAANA.

Wanachinjana kubakana , kuuana kama WANYAMA.


Tumejilaani wenyewe.
 
Kuhusu kauli ya Africa kua na shithole countries, mi naona ni ukweli mtupu. Nchi inauza bandari yake, madini na rasilimali nyingine kwa deals za rushwa, inaachaje kua shithole?

Kuhusu kauli ya Elon Musk kuinunua Africa then awadelete viongozi wote, napinga kuinunua Africa, ila naunga mkono kuwadelete viongozi.
 
Mwafrika alinuimwa rasilimali adhimu na muhimu sana ambayo ni akili na hili lisha wahi semwa na watu weupe muda mrefu sana hasa kaburu Botha.
 
Back
Top Bottom