African Union na EAC wana mpango gani juu ya Maafa?


M

Mchili

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2009
Messages
727
Likes
6
Points
35
M

Mchili

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2009
727 6 35
Duniani kumekuwepo na majanga ya aina mbalimbali kila mwaka. Tumesikia matukio ya tsunami, matetemeko ya ardhi huko Hait na Chile hivi karibuni, maporomoko ya Same na Uganda na mafuriko huko kilosa kwa uchache tu. Kila yanapotokea haya majanga yanasababisha vifo vya watu wengi, uharibifu wa mali na miundo mbinu na gharama kubwa za uokoaji na misaada ya dharura ya kuwahifadhi walionusurika.

Kwenye suala la uokoaji na misaada imekua ni tatizo kubwa hasa kwenye hizi nchi maskini misada kidokidogo inawafikia walengwa ikiwa imechelewa kiasi kwamba hata wale ambao wangenusurika wanakufa kwa kukosa misaada. Kutokana na umaskini wetu Waafrica, tungekusanya nguvu kupitia jumuiya zetu za ushirikiano kama East African Union na African Unioni kikaundwa kikosi cha uokoaji chenye zana na vifaa kama helkopta, mawasiliano, wataalamu wa uokoaji n.k tungeweza kupunguza maafa ya majanga haya kwa kiasi kikubwa.

Hili linawezekana na nchi wanachama wana uwezo wa kuweka badget ya kutosha. Cha ajabu hawa viongozi wetu hamna anaeongelea sula linaloumiza raia wao. Wameweka kipaumbile kwenye siasa na mambo wanayoona yanawajenga. Je huu ushirikiano ni wa dhati au nao ni usanii tu?
 

Forum statistics

Threads 1,249,747
Members 481,045
Posts 29,710,275