Ndani ya siku moja iliyopita wazimbabwe wamepata kile walichokua wanakihitaji.
Si kwamba jambo hili lilikua rahisi hapana Bali msimamo mkali na thabiti wa raia wa Zimbabwe usioyumbishwa ndio uliowafikisha hapo ktk mafanikio.
Ikumbukwe kuwa Mugabe ameitawala Zimbabwe kwa muda wa miaka 37 na baadae kugeuka kuwa dikiteta mbaya sana dhidi ya raia wake hadi Jana alipoamua kubwaga manyanga baada ya mbinyo mkali kutoka kwa raia wake.
Kitu walichokifanya Zimbabwe kinaweza kufananishwa na ARAB SPRING.
Arab spring ilianzia Tunisia ambapo raia wake kwa umoja wao bila kujali ukubwa wa jeshi lao walifanikiwa kumtimua madarakani dikiteta wao Bin Ali, moto huo haukiishia ulishika nyasi ktk nchi ya misri ambapo nao walifanikiwa kumtimua dikiteta Hossan Mubarak.
Vuguvugu hilo liliendelea kushika kasi hadi Libya ambapo dikiteta wa muda mrefu kanali Gaddafi nae alipigwa dafurao Kali sana hadi kupoteza maisha.
Moto huo haukuishia hapo Bali ulienda kuzimikia Syria, dikiteta Assad ameponea chupuchupu na awashukuru sana Warusi.
Sasa kwa Africa, kitu kilichofanyika Zimbabwe kiwe funzo, na kilete vuguvugu jipya kwa wananchi DRC, RWANDA, BURUNDI, UGANDA, CAMEROON, TOGO, CONGO BRAZZAVILLE,.
Kama Zimbabwe wameweza je wananchi wa nchi hizo wanashindwa nn.
Ni wakati muafaka wa kuwang'oa viongozi ving'ang'anizi na madikiteta lkn vuguvugu hilo lisishie hapo Bali liendelee pia ktk kuving'oa vyama ving'ang'anizi vya madarakani ambavyo vimedharau democrasia na kujiona kama vile viliundwa ili kutawala milele na hutumia nguvu zozote kung'angania madarakani.
Zimbabwe Spring iwe funzo kwa nchi za zafrika mashariki na kwa nguvu moja tukiamua kilichotokea Zimbabwe hata ktk nchi zetu za afrika mashariki tuna we za, kinachosubiliwa ni cheche tu moto uwake