African Sports ya Tanga

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253
AFRICAN SPORTS YA TANGA

Jana mtaani pangu nimesikia washabiki wa Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club wakiwatupia madongo mazito mazito washabiki wa Yanga kwa kufungwa goli moja na African Sports.

Club hizi mbili ni ndugu kama zilivyo Coastal Union na Simba lakini zinapokutana ushindani unakuwa mkali.

Nimefurahi Yanga kufungwa.

Nimefurahi kwa sababu kwa muda nitapumzika na shari ya rafiki yangu Kambi Kilago.

Somo yangu Mohamed Bhinda anaelewa maudhi ya huyu Yanga mwenzake.

Basi kwa furaha hii ya kufungwa Yanga nimeingia Maktaba kutafuta kama nina kitu kuhusu Wanakimanumanu nizidi kumkera Kambi.

Nimekuta picha hiyo hapo chini ya African Sports katika "scrap book," yangu ya mwaka 1978.

Nimekuta picha ya Sports iliyokuwa ndani ya Daily News la tarehe 9 February, 1989.

Picha hii inawaonyesha African Sports wako Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kabla ya kupanda ndege kwenda Manzini Swaziland kucheza mechi yao ya kwanza na Mbambane Highlanders, Africa Clubs Cup Championship.

Wakati ule Secretary General wa African Sports alikuwa Ahmed Keya ambae imesadifu ni rafiki yangu.

Kabla ya kuingia ndani ya ndege wachezaji na viongozi wa African Sports walisali rakaa mbili kumuomba Allah awape safari ya kheri.

Hii ni miaka mingi iliyopita, miaka 32 sasa na Sports wakawa wamepotea hadi jana nilipowasikia wamewafunga Yanga.
20210207_164458.jpg
 
Back
Top Bottom