African Association iliasisiwa mwaka gani na nani waasisi wake?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,972
30,317
AFRICAN ASSOCIATION ILIASISIWA MWAKA GANI NA NANI WAASISI WAKE?

Kuna kijana kaniandikia anaomba maoni yangu kuhusu aliyosoma katika kitabu hicho hapo chini "Muungano wa Tanganyika na Zanzibar:

"Baba naomba nikusumbue.

Naomba usome kuanzia ukurasa wa 20 ''Mchango wa Jumuiya Mbalimbali kwenye harakati za Ukombozi.

Mpaka ukurasa wa 31 kisha naomba unipe maoni yako ni muhimu.''

Katika kitabu hicho imeandikwa kuwa African Association iliasisiwa mwaka wa 1927 kitabu kinasema:

‘’Mwaka 1927 Waafrika wa Tanganyika walianzisha jumuiya ya kimaslahi iliyoitwa African Association (AA), chombo cha kutetea maslahi ya Waafrika na kusaidiana kwenye masuala ya kijamii.’’

Nimemwandikia muulizaji kama ifuatavyo:

''Hapa pana kosa kidogo.

African Association iliasisiwa mwaka wa 1929 na mkutano wa kwanza ulifanyika Mtaa wa Ndanda na Masasi Misheni Kota nyumbani kwa Mwalimu Cecil Matola na waliohudhuria kikao hicho walikuwa: Cecil Matola, Kleist Sykes, Ibrahim Hamisi, Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Cecil Matola alichaguliwa President na Kleist Sykes Secretary.

Historia hii ikaja kuandikwa na Kleist Sykes kabla hajafa mwaka wa 1949.

Unaweza kusoma historia ya African Association katika kitabu alicho hariri John Iliffe kwenye sura aliyoandika Daisy Sykes Buruku: ‘’The Townsman: Kleist Sykes,’ Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114).''

1664210179140.png

1664210217040.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom