Africa hatuna la kujifunza toka kwa wazungu

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
8,779
2,000
Ha ha ha e bana eee! kumbe ubepari ni noma, yale mambo ambayo wazungu walikuwa wanawafanyia babu zetu wakati wa ukoloni bado wanaendelea nayo ndani ya nchi zao kwa raia zao. Hakiya nani utumwa bado upo duniani hasa Marekani na Ulaya. Mabepari ndio watawala na ndio wenye njia kuu za uchumi, hivyo serikali imewatengenezea mabepari tu mazingira bora ya kuwanyonya wananchi wao na yeyote yule atakayejipeleka Marekani na Ulaya kichwakichwa. Walichokifanya ni kuimalisha vyombo vyao vya mabavu kama polisi, jeshi, mahakama na magereza ili viweze kuwashughulikia wananchi wao wanaoenda kinyume na sera za kibepari. Mabepari watahakikisha kuwa wanakulipa mshahara ambao utakaourudisha kwao tena wote ili ukaendelee kufanya kazi. Hivyo kama unataka kubaki na pesa kidogo mfukoni kwako ni lazima ufanye kazi kwa masaa 16 hadi 24 kwa siku, ndipo utakapomudu kulipia simu yako, nyumba, maji, umeme, matibabu, chakula na shule za watoto. Ee bana e, usiombe uugue ukiwa Ulaya na Marekani, kama huna bima ya afya lazima utakufa tu, au ushikishwe ukuta, maana hutaweza kununua dawa pharmacy hata kama unaijua jina na matumizi yake hadi uonane na daktari kwanza.

Usishangae kama una ndugu yuko Marekakani au Ulaya asiyekumbuka kutuma chochote nyumbani "hana" usimlaumu. Na kama una ndugu yuko nchi hizo ambaye anajitahidi kuwakumbuka kwa vijisenti nyumbani ujue huyo kijana anafanya kazi zaidi ya moja ama anashikishwa ukuta, wengi wao wana kazi 2 - 3, hivyo wanafanya kazi saa 24 kwa siku. Wengine wanatamani kurudi nyumbani lakini ama wanaona aibu kurudi mikono mitupu ama hawana nauli. huku watu wana discipline ya kukandamizwa sio ya heshima na utashi wao. Waafrica wanakwenda Ulaya na Marekani wakiwa na digree zao lakini wakifika Ulaya na Marekani unawakuta wanauza duka (malls) kwa mshahara wa dola 8 kwa saa. Wengine wanasoma nurse assistant ili wapate kazi ya kutunza wazee majumbani, jamani ulaya ulaya ulaya hakuna cha kukimbilia kusikieni hivyo hivyo. Ulaya na marekani wanawake ni wengi mno kuliko wanaume, kisa wanaume wengi hasa ma-black wako magerezani kwa uhalifu mdogo mdogo na uzururaji bila kazi. Ushoga ni mwingi hapa kwasababu wanaume hawana hela na hawana kazi na maisha ni ghali, kwahiyo unaweza kushikishwa ukuta kwa sahani ya chips mayai. Vijana hawawezi kununua vitu vipya madukani kule Ulaya na Marekani, ama wananunua mitumba (used) au vitu hafifu ama vilivyoisha fasion yake madukani vilivyoshushwa bei 'Clearance'. Watu wamepewa uhuru wa bandia kama unataka kutembea na mbwa ruksa, kama unataka kutembea uchi ruksa, kama unataka kuwa soga ruksa, n.k ili wajione wako huru, lakini sio kweli. Watu wengi ulaya na marekani wamechanganyikiwa, vichaa kibao.

KAMA KUNA kijana anayetafuta VISA ya kwenda Marekani na Ulaya hebu afikirie tena mara mbili kama ni muhimu kufanya hivyo. Ulaya ni kuzuri kwa kusoma tu kisha urudi nyumbani kwenu. Vijana tukifanya kazi kila siku kwa masaa 16-24 hukuhuku Africa pia tutatoka.

Tuzipende nchi zetu, tubaki kwenye nchi zetu, tufanyekazi kama watumwa kwenye nchi zetu na tupambane kwa nguvu zetu zote na viongozi na wanasiasa wanaosababisha tuzichukie nchi zetu na kwenda kuwa watumwa Ulaya na Marekani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom