Aflatoxin kwenye Unga wa Dona

Aflatoxin kwenye Unga wa Dona

Tembomtata

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
266
Reaction score
427
Imezoeleka kuona mtu akila unga wa dona mweusi na mchungu kama ndio chakula bora. Ni kweli mahindi yaliosagwa moja kwa moja na mahindi yaliokobolewa yakasagwa yanautofauti kwenye nutrients, lakini si kweli kwamba kadri weusi wa unga wa dona unavyokuwa ndivyo nutrients zinavyoongezeka.

Weusi mwingi katika mahindi husababishwa na vitu vingi moja ya vitu hivyo ni fungi wanaotengeneza toxin inayoitwa Aflatoxin. Aflatoxin ni sumu inayoua utafiti uliofanywa na TFDA na CDC uligundua kuna high level ya Aflatoxin kwenye sample 52 kati ya 115 see the link (usiseme nimetunga) Tanzania: TFDA Tests Find Higher Aflatoxin Levels in Cereals, Maize Flour.

Hivi ninavyo andika gazeti la leo tar 3.08.2017 la gurdian ukurasa wa 5 limeandika kuhusu vifo vya watoto wa nne waliokufa kutokana na aflatoxin huko Dodoma na cases nyingine mbili za mwaka huu. Ukisoma Link hiyo ya juu hapo utaona mpaka mwaka jana mwezi July kulikuwa na vifo 14. Kuna mtu alikuwa ananiambia Arusha mbwa wanakufa sana kwasababu watu wanawasagia mahindi mabovu kama chakula chao.

Lakin issue sio vifo issue ni matatizo ambayo inaleta kwenye ini (liver). Nilikuwa nasoma case ya Kenya ya 2004 between January na June watu 317 walirepotiwa kuwa na matatizo ya ini yaliyotokana na aflatoxin kati ya hao 125 walikufa Liver Cancer and Aflatoxin: New Information from the Kenyan Outbreak.

Tumezoea kula unga wa mahindi ambao hatujui umetoka wapi tena kumeibuka wajasiria mali ambao ungawao si dhani kama umetest wa TFDA.
Now you know its up to you to chose. Unaweza kugoogle kujifunza zaidi
 
MMMh mara kidudu mtu ,mara mayai feki,mchele feki sasa kama vyakula vyote vya asili mnavipiga vita cancer mtaiepukaje kwa vyakula vya kusundikwa?

Babu zetu enzi hizo hawakua na stress kama hizi na waliishi miaka mingi,kula kulingana na urefu wa mfuko wako sio kisa kuna tetesi fulan basi nawe uache kula chakula fulani
 
MMMh mara kidudu mtu ,mara mayai feki,mchele feki sasa kama vyakula vyote vya asili mnavipiga vita cancer mtaiepukaje kwa vyakula vya kusundikwa?

Babu zetu enzi hizo hawakua na stress kama hizi na waliishi miaka mingi,kula kulingana na urefu wa mfuko wako sio kisa kuna tetesi fulan basi nawe uache kula chakula fulani
Umeongea vyema kwa mtazamo wako...kunatofauti kati ya tetesi na ukweli. Kuna tofauti kati ya kudhani na kudhibitishwa pia. Soma hizo link na soma gazeti la leo. Babu zetu hawakuishi siku nyingi kwa vile walikula vitu vya asili tu, waliishi kwa vile walijishughulisha na kazi zilizokuwa hitaji kuushughulisha mwili. Kama unadhani waliishi kwa kula vitu vya asili tu kula na wew uone kama utaishi muda mwingi. Hypothesis ulioitengeneza hapo ni kwamba kila anae kula vitu vya asili anaishi muda mwingi na asie kula vitu vya asili hufa mapema which is very wrong kwa vile wazungu ndio wana life expectancy ndefu kuliko wajomba zetu walioko vijijini wanaokula vyakula vya asili
 
8760ce9fcf79d9d553ebfaaa1549b316.jpg
 
H
Tfda ifumuliwe
Tbs ifumuliwe
Tutaisha
Utafukuza kila mtu kwenye hii nchi... wewe mwenyewe hufuatilii hivi vitu leo ndo unaona kwenye jamii forum issue ya mwaka janaaaa ushakula dona mara ngapi?
natania tu mkuu usikasirike 😀😀😀😀
 
Watakuja watafiti wengine watakuambia hayo mate nayo ukiyameza yana sumu
Hivi vitu vyakupuuzia utafiti huwa vinatu cost sana hasa wa africa na watanzania.........Kituo cha mwendo kasi cha Jangwani waliambiwa wako kwenye mkondo wa maji wakakataa kata kata yanayowakuta wanayajua wenyewe.....
 
Aflatoxin inasababishwa na utunzaji mbovu wa mahindi hivyo ukijua mahindi yako yametoka wapi na yalitunzwaje hakuna shida.....Tatizo hawa wanaosaga na kuuza wao wanununua mahindi popote tuu hawayakagui wanasaga tuu na kufunga na kuuza unga wa dona.
 
kiukweli food industry iko loose sana hapa TZ. kuna mashine za kukoboa na kusaga nyingi zinafanya mpaka packing ya unga mifuko kuanzia kilo tano na kuendelea na kuna vigari vina distribute huo unga madukani lakini huoni popote wanakaguliwa. Thats why kila siku magonjwa ua ajabu ajabu yanaibuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi napoga dona ninayo iandaa mwenyewe na kwa Siku ninatembea km 2 hiyo kwangu naita nimeushughulisha mwili nyie kuleni dona ya kuatengenezewa halafu hamfanyi mazoezi majibu mtayapata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kwao wanaonunua dona ,linasagwa tu na mahindi yoyote tu hayasafishwi vzr!

Ili kuepuka hayo ,nunua mahindi mwnyew yaoshe km sio masafi andaa vzr saga,ht huo uchungu kwnye unga hutausikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka dona safi! Nunua mahindi kasage mwenyewe hao wengine wanatulisha mapumba

......
 
Nina jamaa aliwahi kupoteza biashara sababu ya hii Aflatoxin. Alifanikiwa kupata mnunuzi wa Korosho iliyobanguliwa sasa wenzetu wako serious kwenye mambo ya chakula akaambiwa apeleke samples za korosho kwenye maabara mbili tofauti majibu kutoka, asilimia ya aflatoxin ikawa kubwa kuliko kiwango kinachoruhusiwa katika hiyo nchi.......utunzaji wetu wa nafaka(mahindi, karanga, korosho, etc) bado sio mzuri elimu bado inatakiwa kwenye ujenzi wa maghala na utunzaji!
 
Ukitaka dona safi! Nunua mahindi kasage mwenyewe hao wengine wanatulisha mapumba

......


Aflatoxin haina maana ni kusaga mwenyewe, ni utaratibu Wa Usalama Wa chakula kwa ujumla wake kuanzia shambani mpaka mezani.
 
Back
Top Bottom