Afisa wa Wanyama Pori TANAPA auawa kwa kuchinjwa kinyama

Kisamo namfahamu vizuri huyu bwana alikuwa hana ugomvi na mtu ni mtaratibu aliyekuwa anajitoa sana kanisani. Tumempoteza mtu mwema mcha Mungu. Ndoa yake haina hata miaka 4. Damu yake itamlilia Mungu daima na haitapotea bure. We will Miss you Emmily
 
Huu ni upotoshahiji mkubwa kwa nchi yetu bado criminal act nyingi ni primitive, uchunguzi ake hauhitaji hat uwe na degree kungamuaa kuwa ni rahisi kuwapata watuhumiwa.
mfano kwenye hili, hivi unashindwa vipi kupata alama za vidole ? unashindw avipi kupata DNA trace, uanshindwa vipi kupata simu za mononi zilizokuwa around tukio kwa usiku huo na ukachambua na kupata muuaji wako?

tubadilike tuache kutetea jeshi dhaifu la polisi unless wawe wnafanya makusdi kitu ambacho wanchi tumekuwa tukiamini sikuzote.

by the way inakuingia akilini eti gari ikutwe kitaa then apigiwe simu mke wake alete funguo wa akiba?
walijuaje kuna funguo w akiba?
kwanini hawakuvunja mapema hilo gari na iuangalia kuna nini?

Mkuu nakuunga mkono....kuna vitu vingi vinafumbiwa macho hapo....eti hata gari imechukuliwa na polisi, imekokotwa kutwa nzima iko kituoni polisi hawajajua kuna mwilii wa mtu aliechinjwa ndaNI ya gari! Kuku tu akichinjwa anaharufu... sembuse binadamu??
 
Kupitia kifo cha afisa huyu iwe chachu ya kukomesha mauaji kama haya ....afisa mkubwa kama huyu anauawa alafu mpaka sasa hakuna aliyekamatwa? Idara zetu za usalama zinaogopesha sana namna wanavyoshughulikia matukio mazito kama haya ....
 
Inasikitisha kuona watu wanakwenda kumuua binadamu mwenzao kama kuchinja myama.Damu ya mwanadamu haitaenda chini Bure Mungu awalinde familia awape nguvu kipindi hiki kigumu.na wale wote waliohusika watakwenda kupatikana kwa jina la Yesu hii damu ya marehemu itawasumbua sana
 
Acheni kuwasingizia polisi kwa kila baya linalitokea maana huyo anatakiwa kulindwa na askari wao na wala sio polisi


Wakati Mangu anapinga vikundi vya ulinzi vya makundi ya watu kujilinda alisema ulinzi wowote binafsi hauruhusiwi kwa kuwa ni kuingilia kazi ya jeshi la polisi. Akasema Ulinzi wa raia na mali zao ni kazi ya polisi waachiwe wao maana ndiyo wenye dhamana hiyo, wwe ulimsikia labda sehemu akisema " ULINZI WA RAIA NA MALI ZAO WAACHIWE POLISI ISIPOKUWA TU AFISA WA TANAPA!"

Ni vizuri ukiongea kitu uwe na kumbukubmu ya kuonanisha na maswala mengine kuliko uropokaji wa kiccm ccm. Hapa ni mahala pa Great Thinkers. Au la sivyo. nenda fb.
 
TANAPA inayofahamika...... watamkamata tu muuaji wa bosi wao. si ajabu hata tayari wameshamkamata. Hawataki tu kutangaza. Polisi watapelekewa tu mtu. Hawa jamaa intelijensia yao ni ya juu sana.

Kupitia kifo cha afisa huyu iwe chachu ya kukomesha mauaji kama haya ....afisa mkubwa kama huyu anauawa alafu mpaka sasa hakuna aliyekamatwa? Idara zetu za usalama zinaogopesha sana namna wanavyoshughulikia matukio mazito kama haya ....
 
Head of intelligence wa TANAPA, anauwawa kwa kuchinywa within weeks of kuuwawa kwa faru wawili serengeti. Hapa hatuhitaji degree ya criminology kuona uhusiano uliopo. Kwa ulinzi wa faru wa jk hakuna shaka kuwa baadhi ya park rangers wa serengeti wanahusika kwa karibu ktk kuuwawa kwa faru, na huenda mkuu wao wa intelligence alifahamu hilo na kuwa mkali na kuwatishia kuwa mwisho wao umewadia. Maskini hakujua mtandao huo unanguvu kiasi gani. Pembe ya faru ni about Tsh. 300,000,000/=, kwa kiasi hiki mtu muovu atafanya lolote kujilinda. RIP BROTHER, WE WILL ALWAYS MISS YOU AT MARANGU.
....aseee nimekuelewa
 
Kumtuhumu mtu direct kwa jambo kama hili bila ya kuwa na ushaidi ujue likikuchwea utalikimbia
Nadhani hii sheria ya mitandao haipo kabisa,Haiweekani mtu anakurupuka kama amekunywa maji machafu na kumtaja mtu katika jinai kubwa kama hii bila hata chembe ya ushahidi.
 
attachment.php

Kumbe ni full manyota. Haikubaliki wana JF. Msaada wa hali na mali unahitajika ili wauaji wapatikane. Ushauri pia ni msaada.
 

Attachments

  • kisamo .jpg
    kisamo .jpg
    15.3 KB · Views: 798
Inasikitisha saana..Pole kwa familia ya marehemu...Naomba hii iwe barua ya wazi kwa Mh. Rais JPM kwani matukio kama haya na mengine yamekuwa yakitokea saana kwa awamu zilizopita na yakipita kimya kimya na kusahaulika

Kwakuwa kasi yako na utendaji wako ni wa pekee na kwakuwa serikali ina mikono na macho mengi nina hakika wahusika wa tukio hili wanatambulika kwa uwezo na umakini wa watendaji ndani ya serikali yako basi tunaomba uonyeshe UPEKEE wa SERIKALI yako ili uwe mfano kwa MAFIA wote wanaolingia kuvunja sheria bila ya kuchukuliwa hatua zozote stahiki.
 
Times FM Tz

POLISI mkoani Arusha imewatia mbaroni watu wawili wanaohusishwa na tukio la kuuawa kinyama kwa kuchinjwa shingo kwa Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Ulinzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA). Stephen Kisamo.

Kifo cha Kisamo kinahusishwa na mambo mengi yakiwemo vita ya kupambana na ujangili, ikielezwa mkuu huyo alikuwa na siri nzito juu ya watu wanaojihusisha na ujangili wakiwemo wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya Arusha, watumishi wa serikali na wanasiasa.

Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Arusha zilieleza tayari imewatia ndani watu wawili ambao ni marafiki wakubwa wa Kisamo na wanajua siri nzito kutokana na kunaswa kwa mawasiliano ya simu ya kiganjani kati ya marehemu na watu fulani muda mfupi kabla ya mauti kumfika ambao polisi inawachunguza kwa karibu.

?Wasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas sisi tumeshakamata watu wawili wa karibu na marehemu na sms na mawasiliano yanatia shaka, lakini ukweli utajulikana muda si mrefu,? kilieleza chanzo chetu cha habari ndani ya Jeshi la Polisi.Kamanda Sabas alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Desemba 18, mwaka huu asubuhi katika eneo la Kikwakwaru jijini Arusha muda mfupi baada ya Kisamo kutoka nyumbani kwake akiwa na gari aina ya Mazda.
 
(GAZETI LA MTANZANIA DEC. 21/2015)
MAUAJI YA KACHERO GIZANI

NA JANETH MUSHI, ARUSHA
SIKU tatu tangu Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Emily Kisamo, kuuawa kwa kuchinjwa na kichwa kutengenishwa na kiwiliwili, giza bado limetanda juu ya sababu za mauaji hayo.

Mwili wa marehemu Kisamo uliokotwa juzi katika eneo la Kikwarukwaru, Kata ya Lemara jijini hapa ukiwa umefichwa ndani ya gari lake.
Juzi Kamanda Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotafutwa kwa njia ya simu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alisema Desemba 18 mwaka huu Kisamo aliondoka nyumbani kwake saa mbili asubuhi na hakurudi tena mpaka mwili wake ulipookotwa.
Sabas alisema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wa eneo hilo la Kikwarukwaru kuwa kuna gari limeegeshwa eneo hilo kati ya majira ya saa tatu na nne asubuhi, mpaka saa moja jioni.
Alisema polisi baada ya kupata taarifa hizo, walilazimika kwenda kulichukua gari hilo kwa ‘break down' na kulipeleka kituo cha polisi.
Alisema baada ya kwenda kulichukua gari hilo lililokuwa limetelekezwa katika eneo hilo, waliliweka kituoni hapo baadae walipokea taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa tangu juzi mumewe aliondoka nyumbani hajarudi na simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
"Wakati tunaendelea na uchugunguzi juzi asubuhi tulilazimika kufungua gari lile na kukuta mwili wa marehemu ukiwa nyuma kwenye buti ya gari huku ukiwa na jeraha nyuma ya shingo"alisema Sabas.
MTANZANIA lilimtafuta Kamanda Sabas jana Jumapili ili kujua upelelezi na juhudi za kuwasaka watuhuniwa hao zilikuwa zimefikia wapi.
Hata hivyo pamoja na kufanikiwa kumpata Kamanda Sabas kwa njia ya simu alidai kwamba alikuwa njiani akiendesha gari na kisha alikata simu.

(GAZETI LA HABARI LEO DEC. 21/2015)
MKUU WA UPELELEZI TANAPA ACHINJWA
IMEANDIKWA NA JOHN MHALA, ARUSHA

POLISI mkoani Arusha imewatia mbaroni watu wawili wanaohusishwa na tukio la kuuawa kinyama kwa kuchinjwa shingo kwa Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Ulinzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Stephen Kisamo.
Kifo cha Kisamo kinahusishwa na mambo mengi yakiwemo vita ya kupambana na ujangili, ikielezwa mkuu huyo alikuwa na siri nzito juu ya watu wanaojihusisha na ujangili wakiwemo wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya Arusha, watumishi wa serikali na wanasiasa.
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Arusha zilieleza tayari imewatia ndani watu wawili ambao ni marafiki wakubwa wa Kisamo na wanajua siri nzito kutokana na kunaswa kwa mawasiliano ya simu ya kiganjani kati ya marehemu na watu fulani muda mfupi kabla ya mauti kumfika ambao polisi inawachunguza kwa karibu.
"Wasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas sisi tumeshakamata watu wawili wa karibu na marehemu na sms na mawasiliano yanatia shaka, lakini ukweli utajulikana muda si mrefu," kilieleza chanzo chetu cha habari ndani ya Jeshi la Polisi.
Kamanda Sabas alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Desemba 18, mwaka huu asubuhi katika eneo la Kikwakwaru jijini Arusha muda mfupi baada ya Kisamo kutoka nyumbani kwake akiwa na gari aina ya Mazda.
Hata hivyo, jana hakupatikana kuelezea kukamatwa kwa watu hao wawili baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila ya mafanikio, lakini mwandishi wa gazeti alithibitishiwa na maofisa wa Polisi Arusha kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa, lakini wao si wasemaji wa jeshi hilo Arusha.
Awali, Sabas alisema siku hiyo hiyo jioni alifika kituoni hapo mke wa marehemu na kueleza juu ya kutoweka kwa mumewe ambapo mara moja polisi walianza kufuatilia jambo hilo bila mafanikio.
Kamanda Sabas alisema usiku, Polisi ilipokea taarifa kutoka kwa raia wema wa eneo hilo la Kikwakwaru kuhusu kuonekana kwa gari hilo likiwa limeegeshwa maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuonekana mtu yeyote ambapo walifika na kulikuta gari hilo, lililovutwa hadi katika Kituo Kikuu cha Polisi usiku huo na baadaye lilitambuliwa na mke wa Kisamo.
Baadaye walirejea eneo la tukio kwa lengo la kutafuta mwili wa marehemu huyo, lakini hawakufanikiwa kuupata mwili wala kumuona kachero huyo ambapo walilazimika kuomba ruhusa ya kupekua gari hilo.
Alisema baada ya kuomba ruhusa hiyo, mke wa marehemu alipowasilisha ufunguo wa akiba wa gari na Polisi walipofungua na kuanza upekuzi walikuta mwili wa marehemu ukiwa umekunjwa kwenye buti, huku shingo yake ikiwa imechinjwa eneo la nyuma ya shingo yake.
Aidha, Kamanda Sabas alisema kwa mujibu wa maelezo ya mkewe, mumewe alikuwa mgonjwa na alikuwa akijiandaa kwa safari ya India kwa matibabu, hivyo kabla ya tukio walidhani alitekeleza gari baada ya kuzidiwa na ugonjwa.
Mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.




 
Willy Gamba angekuwa hajastaafu jumatano wangekuwa wako nguvuni washenzi wote hao. Kwani huko Arusha wakishakunywa damu za ng,ombe wanawehuka kutaka za binadamu!
 
Back
Top Bottom