Afisa polisi amdunda hakimu wilaya

Afisa polisi amdunda hakimu wilaya

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
242
Afisa polisi amdunda hakimu wilaya



Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Lushoto Wilson Yona (35), amekiona cha moto kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa kwa kupigwa vibao, mateke na ngumi na Mkuu wa Upelelezi wa wilaya hiyo, wakati akitekeleza wajibu wake kazini.

Tukio hilo la aina yake lilitokea saa 2:16 asubuhi ofisini kwa hakimu huyo, katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakati akiwa anaandika hukumu za washtakiwa wengine.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa Upelelezi mkoa wa Tanga, Azizi Kimatta, alisema hakimu huyo baada ya kupata maumivu alipewa fomu ya PF3 kwa ajili ya matibabu iliyotolewa na polisi Na. 5224 PC Hamis.

Akiongea na NIPASHE Jumapili, kuhusu mkasa huo, hakimu huyo alisema akiwa ofisini kwake Machi 22, mwaka huu, mkuu huyo wa upelelezi alimfuata na kuanza kumshambulia akimtuhumu kuwa hajui kufanya kazi yake vizuri.

Hakimu alidai kuwa pamoja na polisi kukataa kufungua jalada la kesi kwa madai ya kumlinda bosi wao, anakusudia kutumia njia nyingine ya kufungua kesi hiyo.

"Amenishambulia sana kwa ngumi, vibao na mateke utadhani mhalifu eti anadai kuna watuhumiwa nimewapatanisha na walalamikaji wakati suala la kupatanisha ni la jeshi la polisi.

“Nikamwambia sikutambui namfahamu mwendesha mashtaka wako mwambie aje nimfahamishe, na ndipo alipoanza kuniporomoshea kipigo kama mhalifu", alidai hakimu huyo.

NIPASHE Jumapili ilimtafuta mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Jumanne Juke na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantino Massawe bila mafanikio.

Hata hivyo, Afisa Upelelezi, Kimatta aliimbia NIPASHE kuwa suala hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi na polisi.


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Hahaaaa, mafisi wanatafunana wenyewe!
"Pilato" akugawa fungu la rushwa la kutosha kwa mjeda wake nini???!!
Tufyefye!
 
It can only happen under CCM rule and under Policcm force! This poliic force has now become lawless, guideless, it's ready to offer itself to manipulations by CCM politicians -- it avails itself to be dressed down just like a wh**e!
 
Unafanywa uchunguzi gani tena?
Kama hiyo latin maxim umeitoa wewe unachekesha sana kwani inaenda kinyume na post yako.kwanini wasipeleleze kwana Hakimu hawezi kutunga habari ya uongo?Lazima upelelezi wa uhakika ufanyike ndio tuwe na right ya ku condemn
 
Lilianza kwa walimu sasa limehamia mahakamani,siku hizi mtu akipata mafunzo na kuwa na uhakika wa kulindwa basi anaweza fanya lolote,eti wanafanya upelelezi..jamani upi tene kama kufungua jalada tu nongwa?TUTAPIGANA SISI ZAIDI YA RWANDA SIKU NAINGOJA KWA HAMU.
 
Maajabu kweli kwei na ni udhalilishaji uliokubuhu! Naona mhimili wa mahakama ukipoteza sifa na heshima yake!
 
sometimes mahakimu wanakera,
Kuna kipindi nilikamata mwizi na jamaa akamuachia hivi hivi
Wacha adundwe
 
Afisa polisi amdunda hakimu wilaya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Lushoto Wilson Yona (35), amekiona cha moto kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa kwa kupigwa vibao, mateke na ngumi na Mkuu wa Upelelezi wa wilaya hiyo, wakati akitekeleza wajibu wake kazini. Tukio hilo la aina yake lilitokea saa 2:16 asubuhi ofisini kwa hakimu huyo, katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakati akiwa anaandika hukumu za washtakiwa wengine. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa Upelelezi mkoa wa Tanga, Azizi Kimatta, alisema hakimu huyo baada ya kupata maumivu alipewa fomu ya PF3 kwa ajili ya matibabu iliyotolewa na polisi Na. 5224 PC Hamis. Akiongea na NIPASHE Jumapili, kuhusu mkasa huo, hakimu huyo alisema akiwa ofisini kwake Machi 22, mwaka huu, mkuu huyo wa upelelezi alimfuata na kuanza kumshambulia akimtuhumu kuwa hajui kufanya kazi yake vizuri. Hakimu alidai kuwa pamoja na polisi kukataa kufungua jalada la kesi kwa madai ya kumlinda bosi wao, anakusudia kutumia njia nyingine ya kufungua kesi hiyo. "Amenishambulia sana kwa ngumi, vibao na mateke utadhani mhalifu eti anadai kuna watuhumiwa nimewapatanisha na walalamikaji wakati suala la kupatanisha ni la jeshi la polisi. "Nikamwambia sikutambui namfahamu mwendesha mashtaka wako mwambie aje nimfahamishe, na ndipo alipoanza kuniporomoshea kipigo kama mhalifu", alidai hakimu huyo. NIPASHE Jumapili ilimtafuta mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Jumanne Juke na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantino Massawe bila mafanikio. Hata hivyo, Afisa Upelelezi, Kimatta aliimbia NIPASHE kuwa suala hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi na polisi. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Binafsi mie naona hapo Mgao haukuenda sawa, Hakimu anaonekana kamzidi akili Afande! Mambo ya RUSH.WA hayo..... Mko wapi PCC.B?
 
Huu ni ukosefu wa maadili katika utumishi wa uma ,nafikiri kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha watumishi wa uma kupigana katika ofisi ya serikali na ikithibitika chanzo hatua kali za kisheria na kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wahusika wa kadhia hii ili kuendelea kujenga heshima katika utumishi wa uma.
 
Chandejaji.jpg

Chande fanya ziada kulinda usalama wa mahakimu


  • Ni Mkuu wa Upelelezi aliyemnasa vibao, mateke na ngumi akiwa ofisini
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Lushoto Wilson Yona (35), amekiona cha moto kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa kwa kupigwa vibao, mateke na ngumi na Mkuu wa Upelelezi wa wilaya hiyo, wakati akitekeleza wajibu wake kazini. Tukio hilo la aina yake lilitokea saa 2:16 asubuhi ofisini kwa hakimu huyo, katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakati akiwa anaandika hukumu za washtakiwa wengine.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa Upelelezi mkoa wa Tanga, Azizi Kimatta, alisema hakimu huyo baada ya kupata maumivu alipewa fomu ya PF3 kwa ajili ya matibabu iliyotolewa na polisi Na. 5224 PC Hamis. Akiongea na NIPASHE Jumapili, kuhusu mkasa huo, hakimu huyo alisema akiwa ofisini kwake Machi 22, mwaka huu, mkuu huyo wa upelelezi alimfuata na kuanza kumshambulia akimtuhumu kuwa hajui kufanya kazi yake vizuri.


Hakimu alidai kuwa pamoja na polisi kukataa kufungua jalada la kesi kwa madai ya kumlinda bosi wao, anakusudia kutumia njia nyingine ya kufungua kesi hiyo. "Amenishambulia sana kwa ngumi, vibao na mateke utadhani mhalifu eti anadai kuna watuhumiwa nimewapatanisha na walalamikaji wakati suala la kupatanisha ni la jeshi la polisi. “Nikamwambia sikutambui namfahamu mwendesha mashtaka wako mwambie aje nimfahamishe, na ndipo alipoanza kuniporomoshea kipigo kama mhalifu", alidai hakimu huyo.


NIPASHE Jumapili ilimtafuta mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Jumanne Juke na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantino Massawe bila mafanikio. Hata hivyo, Afisa Upelelezi, Kimatta aliimbia NIPASHE kuwa suala hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi na polisi.
 
Na bado tunasubiri ngumi za DPP na Police juu ya kesi ya Lwakatare
 
moja ya maeneo ambayo polisi ni kero ni lushoto,kuna askari mmoja maarufu kwa jina la chituma ama kelvin,huyu jamaa ni janga kubwa kwa wakaz wa lushoto anapenda sana rushwa,ananyanyasa sana waendesha bodaboda na madereva wa hiace,mda mwingine huwa anawachapa vibao.mpaka sasa hv kuna mpango wa chinichini unaofanywa na vijana wa bodaboda wa kumsaka huyu bwana na kumtandika,ikibidi hata kumuua.
 
Na bado tunasubiri ngumi za DPP na Police juu ya kesi ya Lwakatare

Mkuu kibogo
Mi nadhani DPP na boss wa TAKUKURU ndo imebaki nukta tu maana sipati picha siku wawekwe karibu halafu ule mjadala wao wa mashtaka ya ufisadi/rushwa uwekwe mezani. Hapatatosha!
 
Last edited by a moderator:
Serikali yetu bana,mlinda amani ndio amegeuka mvuruga amani,pole muheshimiwa.
 
walichapwa viboko walimu, watoto wamepata sifuri, sasa wanapigwa mahakimu, ngoja tufungwe...
 
"no permanent friend, but permanent interrests"
 
Back
Top Bottom