Afisa polisi amdunda hakimu wilaya

Afisa polisi amdunda hakimu wilaya

Good, next time Mwema akampige vibao Chande. Policcm wapo juu ya sharia na mahakimu wakome kujipendekeza kwa serikali ya CCM
 
Tuwaache wafu wazikane na bado tutaona na kusikia mengi kabla ya kufikia mwaka 2015,hawa Police na movies zao hizi ona Mashitaka ya Rwakatare yalivyokaa kiaina hapa pia Police watatwangana maake hawajifahamu ndio maana nikasema Tuwaache wafu wazikane.
 
hawa mapolisi wamezidi sana inapaswa wawe waadilifu ili wakubalike na raia. siku hizi hawa jamaa wanajichukulia sheria mkononi na kuwadhuru watu bila kufuata msingi wa sheria na maadili ya kazi. huku dsm wanasumbua sana bodaboda yaani lazima watoe kitu wanachokiita mpunga vinginevyo hubambikiziwa makosa kibao na kupelekwa kituoni
 
Huwa inashangaza sana ambapo huwa wanasema upelelezi au uchunguzi unaendelea wakati issue zinajieleza kabisa.....no one is above the law!
 
Chandejaji.jpg

Chande fanya ziada kulinda usalama wa mahakimu


  • Ni Mkuu wa Upelelezi aliyemnasa vibao, mateke na ngumi akiwa ofisini
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Lushoto Wilson Yona (35), amekiona cha moto kwa kile kilichodaiwa kushambuliwa kwa kupigwa vibao, mateke na ngumi na Mkuu wa Upelelezi wa wilaya hiyo, wakati akitekeleza wajibu wake kazini. Tukio hilo la aina yake lilitokea saa 2:16 asubuhi ofisini kwa hakimu huyo, katika Mahakama ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakati akiwa anaandika hukumu za washtakiwa wengine.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Afisa Upelelezi mkoa wa Tanga, Azizi Kimatta, alisema hakimu huyo baada ya kupata maumivu alipewa fomu ya PF3 kwa ajili ya matibabu iliyotolewa na polisi Na. 5224 PC Hamis. Akiongea na NIPASHE Jumapili, kuhusu mkasa huo, hakimu huyo alisema akiwa ofisini kwake Machi 22, mwaka huu, mkuu huyo wa upelelezi alimfuata na kuanza kumshambulia akimtuhumu kuwa hajui kufanya kazi yake vizuri.


Hakimu alidai kuwa pamoja na polisi kukataa kufungua jalada la kesi kwa madai ya kumlinda bosi wao, anakusudia kutumia njia nyingine ya kufungua kesi hiyo. "Amenishambulia sana kwa ngumi, vibao na mateke utadhani mhalifu eti anadai kuna watuhumiwa nimewapatanisha na walalamikaji wakati suala la kupatanisha ni la jeshi la polisi. "Nikamwambia sikutambui namfahamu mwendesha mashtaka wako mwambie aje nimfahamishe, na ndipo alipoanza kuniporomoshea kipigo kama mhalifu", alidai hakimu huyo.


NIPASHE Jumapili ilimtafuta mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Jumanne Juke na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantino Massawe bila mafanikio. Hata hivyo, Afisa Upelelezi, Kimatta aliimbia NIPASHE kuwa suala hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi na polisi.

Tanga ni ngumi tu kwa kwenda mbele. Yaani viongozi wako juu ya sheria. Hadi 2015 mbona tutaona na kusikia mengi!!!! TANGA MMEINGILIWA JAMANI. UPOLE WENU UNAMIGHARIMU!!!!
 
Ameingilia mhimili mwingine wa dola huyo anapaswa kuletwa Kisutu apate haki yake
 
Wamalizane wenyewe kwa wenyewe labda sheria zitaanza kufwata mkondo wake....
 
Hapo Hakimu kama kweli alipigwa basi alijitakia kwa sababu huwezi kumwambia mkuu wa upelelezi ambaye ndiye huandikia majalada kuja mahakamani kuwa hamtambui ila mwendesha mashtaka aliyechini ya Mkuu wa upelelezi, hapo kuna ukweli kuwa mrungura ulitembea na huenda alikula na mwendesha mashtaka, hata hayo majibu aliyotoa yanatosha kuonyesha jeuri, kipigo alistahili kwa sababu mahakimu wengi wanaharibu kesi baada ya kupokea rushwa
 
Itakuwa jamaa walibambika kesi sasa hakimu kaiona hiyo na kutenda haki, Huenda Bahati yake jamaa alisahau silaha ofisini otherwise ingekuwa zaidi ya ngumi na mateke.
 
Hilo nalo ni jema! Ukiona mti mbichi unawaka, je kwa mti mkavu itakuwaje? Hivi mahakimu wanavyowapendelea hao maccm na mapoliccm wanadhani wako salama wao?? Lwakatare anasumbuliwa na sheria ziko wazi. Tendeni haki wananchi tunawaona.
 
Hapo Hakimu kama kweli alipigwa basi alijitakia kwa sababu huwezi kumwambia mkuu wa upelelezi ambaye ndiye huandikia majalada kuja mahakamani kuwa hamtambui ila mwendesha mashtaka aliyechini ya Mkuu wa upelelezi, hapo kuna ukweli kuwa mrungura ulitembea na huenda alikula na mwendesha mashtaka, hata hayo majibu aliyotoa yanatosha kuonyesha jeuri, kipigo alistahili kwa sababu mahakimu wengi wanaharibu kesi baada ya kupokea rushwa

unajua hata kesi zinaendaje wewe au unaropoka tu? kwa faida yako; mwendesha mashtaka ndio upande wa pili wa kesi ujiacha mshtakiwa na ndie anaeiwakilisha jamhur, afsa upelelez anaishia kwe upelelez na hawez kuadress mahakama labla akiitwa kama shahid.
Istoshe mhe Wilson ana zaid ya miaka kumi kwe kazi ya uhakimu ana uzoef na kaz yake na ni mmoja wa watu competent kwe sheria.
huyo askar amekosa adabu kama ulivyo askar wengi wa amir jeshi mkuu Jakaya.
 
heri wapigane wenyewe kwa wenyewe
Tanga kuna laana gani.Mara mkuu wa wilaya Korogwe kamtukana Mwanasheria,Mkuu wa wilaya Tanga kapigana,kataka kumuweka ndani Padre, Mkuu wa upelelezi Lushoto kampiga Hakimu.Mkoa wa Tanga unatakiwa kufanyiwa maombi.
 
huyo hakimu shenzi kabisa yaani polisi wahangaike kukamata watuhumiwa halafu yeye anawaachia kiulaiiini!
 
Lilianza kwa walimu sasa limehamia mahakamani,siku hizi mtu akipata mafunzo na kuwa na uhakika wa kulindwa basi anaweza fanya lolote,eti wanafanya upelelezi..jamani upi tene kama kufungua jalada tu nongwa?TUTAPIGANA SISI ZAIDI YA RWANDA SIKU NAINGOJA KWA HAMU.

Acha kupenda shida wewe, vita unaijua au unaisikia? Acha ushabiki uchwara.
 
Habari bandugu,

ajarushwa ngumi isipokuwa hakimu ndo alitaka kumrushia ngumi...ndpo aripoamua Oc cid kurud nyuma kukwepa ugomvi,...magazet yanadanganya
 
Hili tukio ni lakusikitisha na inavyoonyesha huyo Polisi hajui au haelewi kabisa dhana ya Utawala wa sheria, na kwa madaraka aliyonayo alipaswa kuheshimu Uhuru wa Mahakama katika maamuzi yake na kama hakuridhika angepaswa kuyapinga kwa kukata rufaa ktk mahakama ya juu. Maana ya uhuru wa mahakama ni kuwa na mahakama ambazo zinafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria bila ya hofu, ushawishi au shinikizo la aina yoyote ile. Kwamba inapotokea haki ya mtu binafsi imeingiliwa, inaingiliwa au inaelekea kuingiliwa hata kama Serikali, basi
mahakama iwe huru kuamua kesi hiyo bila upendeleo.
 
Back
Top Bottom