Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Taarifa za ndani zinadokeza kuwa afisa mmoja wa NSSF (Bw. Kinunda) amejeruhiwa na kulazwa hospitali ya Aga Khan baada ya kupigwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka huko anakoishi Kimara. Kwa muda sasa wakazi wa maeneo ya Kimara wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi hasa baada ya kuongezeka kwa wimbi la vitendo vya ujambazi.
Kwa mujibu wa vyanzo vyangu vya kuaminika Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama vimejikuta vikiziwa ujanja na makundi ya vibaka na majambazi na kuwaweka katika hali ya kushindwa kujibu mashambulizi ya uhakika huku ukusanyaji wa habari za kiintelijensia ukiwa duni katika maeneo mengi ya Jiji la Dar.
Hadi hivi sasa haielweki kama vyombo hivyo vina uwezo wa kupambana na vibaka hawa ambao wanaoekana kujenga vibanda katika maeneo mbalimbali nchini. Kama hali hii inaendelea wananchi wanaweza kuanza kuhusisha usalama wa mitaa yao na wale walioko madarakani au wale wanaotaka kuchaguliwa.