Afisa Habari Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha asema Waziri Ummy adaiwa atoa tamko la Watanzania kutosaidia saidia watoto njiti hospitali

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Afisa Habari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru, Sirila Kiyanda ameigomea KLABU ya KITAMBI NOMA kutokufanya matendo ya huruma kwa Watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati (NJITI ) ambao wanapewa matibabu katika Hospitali hiyo licha ya wahusika hao kuwa na ruhusa na kibali kutoka Kwa Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo, Dkt. Ernest Alex.

Hayo yametokea leo tarehe 29.3.2024 hospitalini hapo baada ya Kitambi Noma kufika wakiwa wamebeba bidhaa mbalimbali ambazo zinahitajika kwa Watoto hao wadogo ambao ni kama Malaika wa Mungu na Wazazi waliojifungua ambao hawana uwezo lakini Afisa Habari huyo alitoa maelekezo kwa baadhi ya Watumishi waliokuwa zamu kutokutoa ushirikiano kwa Klabu hiyo lenye lengo la kufanya matendo ya huruma.

Kitendo hicho kiliibua hisia za wengi waliyokuwa hosptalini hapo baada kuona watu hao wamekataliwa kupokelewa vifaa vyao na kuamuliwa waviache mapokezi ilihali vifaa hivyo vinatakiwa kutumiwa na watoto wadogo wazazi.

Afisa Habari huyo katika hospital hiyo alisema Waziri alimueleza kutowaruhusu wanahabari kufanya kazi yoyote ndani ya hospitali isipokuwa kazi za Kiserikali tena kwa kuitwa na barua maaalum kutoka Wizara ya Afya, kitu ambacho kinakandamiza taaluma ya habari kwa kuhabarisha umma.

Licha Kitambi Noma kuwa na kibali maalum cha kuwaruhusu wao kufanya matendo ya huruma kutoka kwa Dkt. Alex, Afisa Habari huyo alisema hakitambui na yeye ndiyo mwenye maelekezo yote kutoka Wizara ya Afya na kutoa maelekezo makali kwa Matroni wa zamu kutopokea chochote.

Baada ya mvutano wa zaidi ya Dakika 180 na Sekunde 47, Matroni wa zamu aliamua kuubeba msalaba huo kwa huruma na mapendo na kuwaruhusu Kitambi Noma kutoa msaada huo na kuwashukuru, maana msaada huo umefika wakati muafaka maana Watoto hao wanaouhitaji Mkubwa sana wa maziwa kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati kitendo ambacho mara nyingi maziwa ya wazazi wao yanakuwa bado hayajajitengeneza kwa ajili ya mtoto kunyonya.

Hadi Jarida hili linaenda hewani jamii inajiuliza Je? kuna siri gani kubwa kati ya Afisa Habari huyo SIRILA na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu?.

Je, Rais Samia Suluhu Hassan, mama namba moja wa Taifa na mwenye huruma ametoa fedha nyingi katika maboresho ya Sekta ya Afya ndiyo hataki msaada au Waziri na Sirila wanataka kumkwamisha Rais kwa nia ipi?

Je, Kwa nini Sirila anadharau maelekezo ya Boss wake, Dkt. Alex, nani yupo nyuma yake?

Mbali ya maswali mengi ila sasa tunamwomba Waziri Ummy Mwalimu amuangalie upya Sirila Kindayo na kama wana malengo yao wasione mioyo ya Watanzania haifai kusaidika.

IMG-20240329-WA0006.jpg
 
Mlipomtafuta Waziri Ummy alisemaje?
Wakiharibu utawakuta kizi city .msikitini wamemzunguka kuomba huruma ya ...kiimani asiwaguse kweli zama hizi nasikia mana kizi hatumbui mtu imani yake.....hata afanye nini.....zamu yaoo etiiii mujibu wa machawa wa mana kizi
 
TEacher hatoshi pale afya
Gwaji girl alifaa kabisa kushika usukuni wa afya
Ila ni imani moja na kizingumkuti basi hakuna atakachofanywa ila waziri wa hovyo
 
Back
Top Bottom