Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,345
- Thread starter
- #341
Halafu ktk thread hii wale manguli wa ushabiki wa soka siwaoni kabisa,wapi idimi,mentor,balantanda,mfarisayo,bak,pazi,peasant etc!au wote hao ni diaspora?
Hao sio washabiki wa soka, wengi wao ni wapenzi wa televisheni au individual timu na wachezaji. Huwa nashindwa kumuelewa mtu anafunga ndoa na timu za Ulaya ambazo hata kuziona zikicheza live hajawahi, yet anajiita mdau wa soka.
Wanatumia nguvu nyingi, hisia na akili kujadili michezo ya Ulaya na timu za huko ambazo hata haziwatambui wala kuwaheshimu wakati kwetu michezo ikididImia. Sijui nafasi yao ni ipi katika kuinua soka let na michezo mingine iliyo dhoof il hali? Lakini bado wanajiita GT, Greatthinker gani anajiita Chelsea damu wakati kwo Nyarugusu pia kuna timu na hata hajisumbui kiutazama, na yeye akijiita mshabiki damu sijui wale wanaokaa front stand kila wiki wajiitaje?
Mimi hawa siwatofautishi na mateja ambao baada ya kula bwimbwi hujihisi wako New York, au masista duu wa Sinza ambao maisha yao ni kama ya kwenya tamthilia.
#NO HARD FEELINGS