Pengo
JF-Expert Member
- Oct 15, 2009
- 579
- 10
Habari zilizonifikia punde tuu ni kwamba askari polisi wa kituo cha chuo kikuu cha Dodoma wameleta maafa ya mama mmoja ambaye alikuwa akifanya biashara ya kuuza chakula kwa wafanyakazi wanaojenga moja ya majengo ya chuo kikuu college ya Humanity & social science.Chanzo cha kifo hicho ni amri ya UDOM ya kuwaondoa mama lishe wasiuze chakula hapo kwa madai kuwa wengi wa wanafunzi wa HSS hawataki kununua chakula katika cafeteria za chuo na kuamua kununua chakula kwa mama lishe hao.Inasemekana polisi walifika eneo la tukio majira ya saa 3 asubuhi na kuanza kuvunja mabanda ya mama lishe pamoja na mahanga ya wafanyakazi wajenzi ambao wanayatumia kwa malazi yao ikizingatiwa wafanyakazi wengi wametoka nje ya mkoa wa Dodoma kwavile Dodoma yenyewe haijitoshelezi kwa wafanyakazi.Habari zinasema kuwa walitokea wahandisi wasimamizi wa kazi na kuongea na uongozi wa UDOM na walikubaliana kuwa mahanga ya wafanyakazi wajenzi yasiguswe kwani kwa wao kupata malazi kwa muda mfupi ni vigumu.
Cha kushangaza majira ya saa 9 mchana walifika tena Polisi wakiongozwa na mkuu wao mwenye nyota 3 na kuanza kuchoma majengo yote bila kuangalia kuna nani ndani au kuna kitu gani kitu kilichosababisha marehemu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ndani ya banda kukosa nafasi ya kutoka kwa kuzidiwa na moto.Wafanyakazi wajenzi walimchukua mamalishe huyo na kumpeleka hospitali ya mkoa General Hospital na alifariki mara baada ya kufikishwa hapo hospitali.
Taarifa nilizonazo leo wafanyakazi wajenzi wamegoma kufanyakazi na wameandamana hadi kwa naibu makamu mkuu wa UDOM Profesa wa Kiswahili Mlacha.