Afande Siro, hii ni kudhalilisha jeshi, hawa Polisi waadhibiwe

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,667
30,585
Sikatai muwakamate ila mnapowafuata bajaji na pikipiki mnawaomba docs zote wakiwa vituo vyao wanaonesha, bado mnawaambia waende kwenye defender asiyekuwa na hela anaondoka na polisi, hii sio haki.

Tukio hili liko hapa Kimara Baruti, wapo mpaka sasa defender moja wameshuka 12 wakazunguka bajaji na pikipiki.

Kinachoendelea unakamatwa unapelekwa kwenye defender wanalazimsishwa kutoa hela asiye na hela anaondoka na polisi mpaka Kimara.

Na hawa polisi nahisi ni wa Kimara, naomba hii hali usiikubali kamanda. Jeshi lifike wakati heshima irudi jamani huu ni wakati wa Magufuli.
 
Imekuwa kero kwa kweli,au ni malipizi? Unajua bodaboda wengi walikuwa wakimkubali Lowasa kipindi cha kampeni.Tutamkumbuka tu mzee wa msoga.
 
Mie pia ni mmiliki wa Biashara ya bodaboda.
Tatizo ni kwamba Bodaboda wengi ujanja mwingi,vibali fake kibaooo.Na lazima tukubali kwamba uvunjaji wao wa sheria unatisha.Na nyingi sasa hivi zilizopo roads ni za wizi,watu wamezipiga siku za nyuma kisha wanaziingiza sokoni.
Acha Polisi wafanye kazi yao,Pikipiki za wizi na vibali fake ni vingi sana.Sio kila documents atayoitoa Driver basi Polisi wakubaliane nayo,na ndio maana wanapotilia shaka inabidi waondoke nao.Ukitaka ku balance stroy we fuata kituo wanachokwenda kisha waulize madereva husika na Askari wa kituo,utapata jibu

Dunia ni kijiji,wao kama wanaombwa rushwa kwa mazingira hayo basi watumie sim zao ku record na sio kulalamika.
 
maisha ya mtanzania ni kufa kufaana. hili la vibali ni UONEVU WA HALI YA JUU. polisi wamewageuza waha vijana ni chumio lao.ndo maana wizi unaongezeka . vijana wafanye kazi gani.......? wamejiajiri bado shida hili jeshi halina tofauti na ntarahamwe.
 
Hivi Pdidy siku hizi unaandika vizuri hivi hongera Sana naona master ya UD at work..
 
Mie pia ni mmiliki wa Biashara ya bodaboda.
Tatizo ni kwamba Bodaboda wengi ujanja mwingi,vibali fake kibaooo.Na lazima tukubali kwamba uvunjaji wao wa sheria unatisha.Na nyingi sasa hivi zilizopo roads ni za wizi,watu wamezipiga siku za nyuma kisha wanaziingiza sokoni.
Acha Polisi wafanye kazi yao,Pikipiki za wizi na vibali fake ni vingi sana.Sio kila documents atayoitoa Driver basi Polisi wakubaliane nayo,na ndio maana wanapotilia shaka inabidi waondoke nao.Ukitaka ku balance stroy we fuata kituo wanachokwenda kisha waulize madereva husika na Askari wa kituo,utapata jibu

Dunia ni kijiji,wao kama wanaombwa rushwa kwa mazingira hayo basi watumie sim zao ku record na sio kulalamika.
Kwa hiyo na were ya kwako ni ya wizi? Na ina vibali fake tuanzie hapo kwanza? Usiwe na tabia ya kujihesabia haki itakughalimu siku moja, wanaosumbuliwa na polisi sio lazima wawe waendesha pikpik tu wanaofanya biashara wanasumbuliwa mpka wenye matumizi binafsi sema polisi hawajajipanga wanaoenda wanaoenda kukamata Pikipiki hakuna wanachokijua kwenye vibali fake wala original
 
Hivi huyu ISRAEL wa vyeti feki/kughushi hajafika huko jeshini ili afanye yake? Maana hapa kwenye halmashauri niliyopo kishaingia.
 
maisha ya mtanzania ni kufa kufaana. hili la vibali ni UONEVU WA HALI YA JUU. polisi wamewageuza waha vijana ni chumio lao.ndo maana wizi unaongezeka . vijana wafanye kazi gani.......? wamejiajiri bado shida hili jeshi halina tofauti na ntarahamwe.
Aisee,watake radhi waha wa Kigoma,au ndio mambo ya smart phone
 
Kwa hiyo na were ya kwako ni ya wizi? Na ina vibali fake tuanzie hapo kwanza? Usiwe na tabia ya kujihesabia haki itakughalimu siku moja, wanaosumbuliwa na polisi sio lazima wawe waendesha pikpik tu wanaofanya biashara wanasumbuliwa mpka wenye matumizi binafsi sema polisi hawajajipanga wanaoenda wanaoenda kukamata Pikipiki hakuna wanachokijua kwenye vibali fake wala original
Najua umeandika kwa jazba,hembu kaa tulia tena na kisha soma umechoandika na kinachojadiliwa.

Humu humu kuna uzi unalalamikia wanendesha bodaboda,leo hii Polisi wanatekeleza majukum yao eti watu wanaona tena waendesha bodaboda wanaonewa.

Narejea tena,kama huna vibali halali polisi watakusumbua,mie sina kesi hata moja nimeyoletewa na Drivers wangu.Muhim tu wananikumbusha muda wa ku renew vibali.
Mie sina shaka na pikipiki zangu,maana zote nanunua mpya,ninavibali vyote hadi number za sim za maduka husika.

Acheni polisi wafanye majukum yao,
 
Wakuu mbona polisi tunawafuatafuata sana, kwanza virushwa vyenyewe ni buku tano tu, tupambane kwanza na wakwepa kodi wakubwa
 
Najua umeandika kwa jazba,hembu kaa tulia tena na kisha soma umechoandika na kinachojadiliwa.

Humu humu kuna uzi unalalamikia wanendesha bodaboda,leo hii Polisi wanatekeleza majukum yao eti watu wanaona tena waendesha bodaboda wanaonewa.

Narejea tena,kama huna vibali halali polisi watakusumbua,mie sina kesi hata moja nimeyoletewa na Drivers wangu.Muhim tu wananikumbusha muda wa ku renew vibali.
Mie sina shaka na pikipiki zangu,maana zote nanunua mpya,ninavibali vyote hadi number za sim za maduka husika.

Acheni polisi wafanye majukum yao,
Sina nilichopanic ila kusema zako halali za wengine za wizi inaama wenzako hawawezi kukua mpya ? Ndio kwenye shako napo mambo ya ww na drivers wako wa bodaboda kama na ww bodaboda hayanihusu na issue ni kwamba watu waliopewa kazi ya kufanya hawana ujuzi nayo
 
Kayenga nahisi hujanielewa vizuri,sina maana ya kukwaza mtu
Nimechobase mie ni kwenye ufuatiliaji wa Documents wanazotaka hao jamaa,hata kama umenunua kwa mtu,kuna utaratibu wa kubadilisha documents kufanya transfer kwa mmiliki mpya na documents kuwa safi sawa na alienunua dukani tu.
Nimebase kwamba watu wengi saana waliibiwa bodaboda na wanaibiwa bodaboda na watu kuuza sehem nyingine,na wale wajanja kutengeneza documents fakes,naomba nieleweke hapa sina maana kwamba kila bodaboda ina documents fake,na ndio maana wapo wanaokamatwa na kuachiwa,na wapo wanaotiliwa shaka ambao hupelekwa kituoni.
Mkuu hujawahi kuibiwa bodaboda,uliza waliobiwa ndio watakuambia kamatakamata hii ina faida gani kwao.Watu kibao wamekatwa kwa style hii na bodaboda za kupiga.Na pia vibali hewa.

Unajua ni sawa na Gari,hasa huku Zanzibar,gari ya biashara lazima iwe na jina la mmiliki pale pembeni ya mlango wa driver,ili ikitokea hali kama hii basi wao wanamtrace mmiiliki moja kwa moja.Ili akatokea maelezo kama kuna utata.Ila kama hakuna basi hakuna usumbufu wa kihivyo.
Tuwaache watu wafanye majukum yao,tumejenga tabia ya kwamba kila operation ya Polisi ni uonevu.
 
Halmashauri ipi hyo mkuu ulipo?
Mkuu, nitaiweka kapuni kidogo.

Issue ni kwamba, Rais katoa maagizo kwa Wakuu wa mikoa na wakurugenzi katika halmashauri zote waondoe;
1. Watu wanaolipwa mishahara hewa,
2. Wenye vyeti vya kughushi/mamluki/feki,

Sasa nimeona katibu anatoa taarifa leo, kuwa watumishi wote wapeleke VYETI VYAO kuanzia j3-j5.

Sasa, najua moja ya sekta yenye mamluki wengi ni gershi! Teh!

Na nyie huko, kaeni CHONJO.
 
Back
Top Bottom