Serikali ya CCM, Polisi na TIS Tambueni hii Nchi Siyo ile ya Mwaka 1961! Tumechoka Jamani ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya CCM, Polisi na TIS Tambueni hii Nchi Siyo ile ya Mwaka 1961! Tumechoka Jamani !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elly B, Jul 15, 2012.

 1. Elly B

  Elly B JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1,194
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  "Ifikie sehemu watawala waanze kuona kuwa hii siyo nchi ya wajinga waliyoitwaa kwa Waingereza 1961"

  Salaam Aleykum,
  Kwa wale ambao hii nchi hawana uzoefu nayo, na wale ambao siasa za Tanzania wanazihisi kwa kusika kwenye media ambazo nying ni za hao "nguruwe" wasiojali wenzao,pamoja na hizo media nyingine ambazo zimeuza uhuru na kukubali kukiuka miiko (ethics) za taaluma ya habari, watakuwa wameridhika na majibu ya uchunguzi wa kitoto wa jeshi letu la polisi pamoja na wengine waliowasaidia kufanya upelezi huo.
  Ni bahati mbaya tu kuwa kwangu mimi naona walichotangaza ni "MATUSI KWA WATANZANIA" na napenda wajue kuwa wanaongeza machungu kwa watanzania ambao tayari walishawachoka. Vinginevyo haiingii akilini kwa mtu ambaye siyo "Mgonjwa", hasa wa akili, uje uambiwe mtu aliyemteka Dr. Ulimboka ni mgeni, ambaye aliletwaletwa tu na jamaa fulani, akashushiwa katikati ya jiji kwenye hoteli flani tu. Hivi KOVA Haoni kuwa anawaambia Watanzania kuwa mtu aliyemteka Ulimboka ni mgeni ambaye haijui Tanzania? Leo aje amteke Ulimboka ampeke kwenye misitu ambayo hajawahi kuiona then ghafla aje ajisalimishe kanisani! Hapa "Kanisani" napo pana utata ndugu zangu. Napenda mjue kuwa hakuna mchungaji wala Padre wala shekhe yeyote atakayemwitia polisi mtu aliyekuja kutubia madhambi aliyofanya. Vinginevyo wangepelekwa wengi!!!!
  Napenda kuchukua nafasi hii kumfikishia Kova kile watanzania wanachoona kutoka katika polisi hii. Kwa sasa hii polisi haitofautiani na kikosi cha majambazi yanayoiba mchana, kwa nguvu ya dola na dhamana ya kulinda mali na maisha ya Watanzania.
  Mara kadhaa pia nimewahi kukuta kitu flani ambacho polisi wanakiita "mbinu mbadala" Nafafanua kidogo:
  Baada ya polisi kuona Wanachi hawana imani nao, walikuja na utaratibu wa kutumia media kujisafisha. Yaani wakakkubaliana wajitahidi kutangaza operations nyingi ambazo wanafanya na ambazo ni successful, ili watu waone wana polisi yenye nia ya dhati ya kukomesha uhalifu. Kwenye plans za "mbinu mbadala" polisi wakafanya michezo mingi michafu ikiwemo hii ya aina hii;
  1. "mnakwenda kufanya patrol mtaa flani mnamkamata jamaa ambaye anayetembea usiku, mnampakia kwenye Defender then ghafla kamanda wa zoezi anakwambia nyiyi flani na flani ingieni huku sisi tunakwenda huku. Usishangae kesho ukiambiwa kuwa "yule jamaa wa jana yuko mochwari kwa sababu alitaka kukimbia" Technically kinachotokea ni unaambiwa utafunguliwa mashitaka ya kuuza madawa ya kulevya na ukionekana kubisha wanajua itakuwa soo huko mbele. so wanakuuwa then sikia watakachosema kesho kwenye media. "Alitushambulia" na Silaha watakutafutia!!! Lakini ukitafuta The bottom line ni kuwa kuna muuza unga ambaye ni mtu wao wanatafuta jinsi ya kumwachia, ili atoke wanatafuta mtu wa kumbadilishia akipatikana ndiyo hayo ya Mkenya na Ulimboka. SO NAPENDA WATU WAELEWE KUWA SIYO KILA ANACHOSEMA KOVA NI KWELI. HUU NI MKAKATI TU.

  2."Mara flani nimewahi kukumbwa na mkasa wa kuibiwa na vibaka. Nikafungua kesi. Shangaa pale polisi inapokwambia haiwezi kumpta mtuhumiwa!!!! Jiulize CID na intelijensia zote wanaishia Arusha tu? Nikafanya upelelezi mwenyewe, ajabu polisi hawawezi kwenda kumkamata mtuhumiwa kwa sababu.... "leo tuko wachache sana hapa kijana" as if mimi sijaona wako zaidi ya sita achilia mbali Mgambo walioongezwa hapo! Haya basi nipewe pingu na silaha niende......."we tuambie tu aliko tutamkamata kwa utaratibu wetu"... What is this? Baadaye wanataka na mimi niende kushiriki tukio la kumkamata!!!jamani nimekuwa polisi kwani??? Akakamatwa. Sasa afande anataka "hela ya mafuta"...kwani huu utaratibu wa kuchangia huduma uko mpaka polisi??? Making this black and white ni kwamba inabidi mlalamikaji uhonge ili mtuhumiwa ashughulikiwe, na mtuhumiwa inabidi ahonge ili arahisishiwe kesi!! Kwa lugha nyingine ni kuwa kwa sasa uhalifu ni dili kwa polisi!! HAWA NDIYO POLISI JAMANI.

  3.Siku moja nikaenda sehemu flani hapahapa mjini, ni baada ya kustuliwa kuhusu tabia ya hawahawa walinzi wa mali na raia. Nikajionea jinsi ambavyo polisi hawa hawa "wachapa kazi" wanaodhibiti uhalifu kama Kova anavyotangaza, Wanavyotumia magari haya haya ya polisi hihii na silaha hizi walizopewa na Wananchi wawalinde, bila kujali mafuta waliyojaza ambayo kasma yake ni kutoka jasho la vijana, vibabu na vibibi vyetu, bila aibu wanakwenda kuiba Bandarini usiku wa saa nane! Sasa nataka kila mtu mwenye akili ajiulize ni nini kinatokea hapo kama tumetoka umbali wa kuwa Chombo cha dola, walinzi, mpaka kuwa majambazi. Then njoo nishawishi niamini kuwa tuna polisi!!!

  4.Ni polisi hawa hawa ambao kutokana na sababu za kiintelijensia hawakuona shida kuua raia wasio na silaha Arusha na maeneo kibao tunayosikia, kwa visababu vya kuamini kuna fujo itatokea halafu hiyo fujo tusiione!!!

  5.Ni hawa hawa polisi wanaozagaa barabarani na maguo meupe halafu shangaa pale unapotaka mwendesha pikipiki awe anatembea na kadi ya pikipiki! Huku magari mabovu yanachanja mbuga na mazima yanakamatwa kwa makosa yasiyoelekea kuleta athari hivi karibuni! Hivi hampandi daladala nyie? hamuoni ni ngapi hazina hata First Aid Kit na zipo tu? wangekuwa wanajua wanachofanya si wangeangalia hilo kabla ya kudai Motor vehicle licence? MAAFANDE KWANI MNAJARIBU KUMDANGANYA NANI HASA? SHAME ON YOU POLICE! ......KOVA.......hivi un....u.u..na..

  Lilipokuja hili la Ulimboka, niliposika mazingira tu nikasema hii ni serikali, ila wamechemka kuratibu zoezi lao kiufundi kwani hata mgambo wakielekezwa namna ya kufanya utekaji nyara hawatafanya ubege ule! Then inatokea viongozi wa nchi wote wako kimya kama hawajui kukubali na kukanusha! Ila baada ya kuona umma wa Watanzani unawaona wachawi wakakurupuka na kukanusha. Hata TBC na Polisi pamoja wa Usalama hawakusikika kabisa kusema lolote. Mara anakuja Waziri Mkubwa anakomaa uchunguzi wa KINA ufanywe waliohusika wafahamike! Nilisema hapa kuna mtu atabambikw akesi tu. Hebu angalieni haya mazingira:

  1. Watu walikuwa wanaonge na jamaa yake na Ulimboka ambaye anafahamika (dokta anamfahamu) ambaye angalau hata hiyo simu tu aliyotumia imesajiliwa! wamteke Ulimboka, ghafla hata polisi ishindwe kutaka kujua kuwa jamaa yake na ulimboka anatumia simu gani? Msishangae pale ntakapowaambia nimecheki na mitandao yote(except sasatel) hakuna polisi wala nani aliyekwenda na swala hilo!

  2. Mara serikali inaunda tume ya kuchunguza, wajumbe ni polisi usalama haohao watuhumiwa! Hii ndiyo akili gani ya mtuhumiwa kujichunguza? Kwani hawa viongozi wetu wanaishi kwenye karne ipi????? Aibu!!!
  Halafu hata pale Ulimboka alipotambua sauti ya mtekaji wake na kudai arudishiwe simu yake bado hawakuonekana kuona kuwa hapo kuna haja ya kufanyika gwaride la utambulisho..HAWA POLISI GANI..WAMETOKA CHUO KIPI HICHO WASICHOPATA UWEZO WA KUFIKIRIA KWA UFASAHA HAWA?
  Ghafla Mtu ashikwe tu from nowhere, anakuwa mtekaji wa Ulimboka, na KOVA anaona ni jambo la fahari kulitangaza! AIBU...
  Halafu kibaya zaidi jamani wachungaji wa kanisa la Gwajima wanasema Yule mtu alikwenda na kutaka apelekwe kwa mchungaji mkuu (Gwajima) baada ya kukataliwa akadai ni muhimu amuone kwani ni yeye aliyemteka Ulimboka! Wala huyu hakwenda kutubu. Baada ya hapo wachungaji wale wakamkagua na kumkuta na simu yenye ujumbe "nimefika,bado najaribu kuwazoea" then baada ya kuona hapo kuna jambo wenye kanisa wakampeleka polisi! Ghafla polisi wamepata habari! HUU NDIYO UCHUNGUZI? Mbona Afande Kova hasemi uchunguzi wao ulifikia wapi kabla ya hiyo " Joshua thing"? Nisaidieni Hawa tuwaweke kundi gani?

  Kwa mtazamo wangu Polisi hawa wamekuwa wahuni sana na kwa kila hali wameonekana ni watekelezaji wa maagizo ya serikali iliyo madarakani bila kujali haki iko wapi and so HAWAWEZI KUAMINIKA KABISA.

  Napenda kusema kuwa hiyo danganya toto haikamati. Nataka Mjue kuwa sisi Watanzania tumeshachoka na majambazi wa aina hii na wahuni waliojipatia haki zote kisheria. Kuna siku Mtaelewa nini kinachotokea pale mnapokuwa mnawafanya watu wote ni wajinga except ninyi! Trust me Hapa wajinga wamepungua sana. Napenda kuwakumbusha kauli ya mwenzetu mmoja hivi majuzi. Alisema "Pale ambapo HAKI imekuwa HAISIKIKI,VIMESIKIKA mabomu na risasi. Chonde nyie watu msitufikishe huko. Wala msidhani eti nyie mtakuwa salama ikifikia hali hiyo. Ila kama that is the only price that Tanzanians has to pay to get free and equal, then let it be. ...... KAMA KUSOMA HAMWEZI ANGALIENI PICHA BASI.

  "STOP EMBARRASSING YOURSELVES"
   
 2. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Polisi wengi wanatamani wasingekuwa wanavaa magwanda wasijulikane!!
   
 3. Elly B

  Elly B JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1,194
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nahisi wangetumaliza kabisa hawa
   
 4. Mkasika

  Mkasika JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  It's truly sad because innocent people are now suffering yet they did their part as requested and turned up to vote! Surely it is now time for this Government to go.
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Polisi ya bongo ukienda kumshtaki mtu mwenye pesa kukuzidi unaswekwa wewe ndani,ni mwenye dau kubwa ndo anatambuliwa na sheria zao.Mambo mengine tumeshasema sana tu humu ndani,nadhani wengi wetu walidhani ni porojo,polisi haifai,period!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280

  Kuna jamaa yangu wa karibu walimbambikia kesi ya kufa mtu bahati nzuri Mungu hamtupi mja wake. Aliponea tundu la sindano vinginevyo angefia lupango. Polisi hawa magamba si wa kuamini hata kwa .0000001%
   
 7. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bottom line,
  Kikwete na CCm yake hawatufai
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Ni kama ilivyo issue ya madaktari,wenye kuumia ni wananchi na serikali iko responsible lakini haiwajali wananchi wake.Polisi ni hivyo hivyo,kuingia ni bure na kutoka ni pesa,penda usipende,uwe na kosa ama hata usiwe na kosa.Kisa wanadai hawalipwi vizuri,bottomline mwenye kuteseka ni mwanachi.Mkuu kwa kusema kweli polisi ni genge la wahalifu kabisa mkuu.
   
Loading...