Nadhani jeshi la polisi mnakosea kukamata Bajaji na pikipiki; hawa Watu wanatafuta riziki walishe familia mnapanda chuki

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Jeshi la polisi KAZI mnayofanya Sasa hivi inatia kichefuchefu hasa Kwa mtu anayetambua ugumu wa maisha uliopo. Kukamata pikipiki na Bajaji Katika Hali hii ya ukata nikudhibiti Watu wasitafute riziki.

Mmewanyima vijana ajira ya pikipiki na Bajaji matokeo yake wizi umeshamiri Kwa Kasi kubwa Sana. Lakini tujiulize hizo pikipiki na Bajaji Zina makosa Gani?

Jaribuni kufanya analysis maisha ni magumu sana, msiwasukume vijana kugeuka wezi wakati wameshajiajiri. Tumieni busara, Kama ambavyo mnalipwa mshahara na hautoshi ndivyo hata wengine wanavyoteseka.
 
Ujambazi, udokozi hauna direct association na kukosa ajira ya kuendesha bodaboda, ninaamini kazi zipo mbadala zinazoendana na bodaboda kwa maana ya kipato chake.

Ninachokiona vijana wengi wamejificha kwenye kujifanya bodaboda ni ajira yao lakini wao asilimia kubwa sana ndio wahuni, wachora ramani za vibaka we kuja kukuvamia kwako.

Ninafahamu wapo vijana na ninawajua wamefanikiwa maishani kupitia bodaboda maana mie no mdau wa hiyo biashara Ila asilimia kubwa ni vijana wapuuzi sana uliza mwenye bodaboda kati ya 10 basi 7 au 8 watakuambia hawataki kabisa kusikia hiyo biashara sababu vijana hawana malengo hawaleti hesabu.

Nimemiliki pikipiki name sasa Ila nilipata hasara pikipiki tatu mpaka nikabadili namna ya kufanya biashara na pia nikabahatika kuchukua vijana kutoka mkoani kwa maana ya nyumbani hapo inasaidia Ila wakishajua mji wanaanza ulevi wa kunywa vitoko na kuuza spea

Yaani unanunua shock up ya mbele anakulia timing anauza anaweka mbovu usipokuwa makini unanunua Tena hata engine wanabadilisha washenzi sana .

Nawajua pia vijana Ila wachache wanafanya hiyo kazi na wanajenga na wanalisha familia Ila wao huwa wanafanya kazi kwa simu tu hawashindi vijiweni masaa yote na ikifika saa moja jioni wanaenda kulala hawana mambo mengi ya kuhuni na inawalipa sana wanakiri.

Kati ya vijana 10 basi 7 wanakuwa wanaendesha wamelewa wanakunywa vitoko, diamond, Kvant ya kupima za bukubuku.

Nimekuwa nakaa na vijana sana nawajua, wacha polisi wakomae otherwise tutapoteza hili taifa. Bodaboda anakuwa mwizi sababu alikuwa mwizi na ni mwizi tu wanajuana vijiweni.

Bodaboda anayeamua kuiba no sababu pikipiki haipo na amezoea kulewa masaa yote na kuvuta bangi ( wengi wao) Sasa anakuwa amekosa means ya kupata hivyo anarudia kazi yake ya zamani ya kuiba Ila kazi zipo kibao.

Nawajua vijana waliachana na bodaboda na Sasa wameajiriwa kwenye kampuni fulani walianza Kama utingo aisee Sasa hivi wanasukuma Scania za kokoto.

So usiwalaumu polisi wacha wafanye kazi yao, nadhani dawa ni kushirikiana na polisi ili kukomesha uhalifu jambo ambalo nafahamu ni gumu sana maana mhalifu wa kwanza ni polisi na wanawajua hao vibaka Ila wamekuwa wanawatumia kujipatia fedha haramu.

Polisi ni mwizi mwenyewe hao madogo ni kutia kiberiti tu.
 
Polisi wantia kichefuchefu yaani wao wananeemesha matumbo yao kupitia pikipiki za watu, inafika hatua tunatamani serikali iingilie kati, yaani siku za hivi karibuni askari wamekuwa wasumbufu sana kwa waendesha pikipiki
 
Kujiajiri ni sawa ila ikumbukwe kuwa kila jambo lina sheria na taratibu zake.

Kama ilivyokuwa kwa machinga, hawa nao inabidi wafuate taratibu zilizowekwa.

Taasisi pekee ya kuhakikisha kwamba wanafuata hizo sheria ni polisi.

Acha polisi wafanye kazi zao, muhimu tu wasiwaonee.
 
Polisi wantia kichefuchefu yaani wao wananeemesha matumbo yao kupitia pikipiki za watu, inafika hatua tunatamani serikali iingilie kati, yaani siku za hivi karibuni askari wamekuwa wasumbufu sana kwa waendesha pikipiki
Sometimes ukorofi na nguvu vinahitajika, hao polisi wapigwe tuu
 
Jeshi la polisi KAZI mnayofanya Sasa hivi inatia kichefuchefu hasa Kwa mtu anayetambua ugumu wa maisha uliopo. Kukamata pikipiki na Bajaji Katika Hali hii ya ukata nikudhibiti Watu wasitafute riziki.

Mmewanyima vijana ajira ya pikipiki na Bajaji matokeo yake wizi umeshamiri Kwa Kasi kubwa Sana . Lakini tujiulize hizo pikipiki na Bajaji Zina makosa Gani?

Jaribuni kufanya analysis maisha ni magumu sana, msiwasukume vijana kugeuka wezi wakati wameshajiajiri. Tumieni busara, Kama ambavyo mnalipwa mshahara na hautoshi ndivyo hata wengine wanavyoteseka.
Polisi wanafanya kaz kwa mujib wa sheria vile ni vyombo vya moto vinataratibu zake kama hazikufatwa wew ni mshakiwa.... na utahukumiwa kwa mujib wa sheria
 
Unawatafutia huruma boda wajeuri kwa wananchi..kulisha familia isiwe excuse ya makundi ktk jamii kukiuka sheria zilizopo.na ndio maana ikawepo serikali..hebu chukua tu mfano mdogo; trafiki wakisema wajiweke kando kwny njia za michepuko (roundbout) na kuacha magari na bodaboda wajiongoze, unafikiri patapitika hapo!
 
Kiukweli hali ni mbaya sana barabarani ukiwa na pikipiki? Kuna vijana wa polisi wanaitwa vodafasta hawa ni tatizo kubwa kwani wanadai fedha kwa nguvu ili wakuachie hata kama huna kosa. Sijui ndiyo kula kwa kadiri ya urefu wa kamba?
 
Mjadala mpana sana huu. Inabidi wahusika (polisi na Bodaboda) wakutane ili kumaliza tatizo.

Inawezekena wengi wa bodaboda hawana uelewa wa sheria za barabarani. Makosa ya barabarani kwa bodaboda yawekwe bayana na faini zijulikane.

Vinginevyo tunatengeneza mianya ya rushwa kwa askari na pia kuwapa kiburi bodaboda sio sawa. Usalama wao na abiria ni muhimu zaidi na sheria zifuatwe kwa kila kundi la jamii.
 
Asilimia kubwa ya Bodaboda hawafuati sheria na ni chanzo cha ajali nyingi.
 
Jeshi la polisi KAZI mnayofanya Sasa hivi inatia kichefuchefu hasa Kwa mtu anayetambua ugumu wa maisha uliopo. Kukamata pikipiki na Bajaji Katika Hali hii ya ukata nikudhibiti Watu wasitafute riziki.

Mmewanyima vijana ajira ya pikipiki na Bajaji matokeo yake wizi umeshamiri Kwa Kasi kubwa Sana . Lakini tujiulize hizo pikipiki na Bajaji Zina makosa Gani?

Jaribu kufanya uchambuzi maisha ni magumu sana, msiwasukume vijana kugeuka wezi wakati wameshajiajiri. Tumieni busara, Kama msaada mnalipwa mshahara na hautoshi ndivyo wengine wanavyoteseka.
Kwani ni zao,wakiwa Barbarani wafuate sheria za uendeshaji
 
Nchi hii kila mwenye mamlaka huona fahari kumnyanyasa mwingine agharabu taasisi moja kuihujumu nyingine ni jambo la kawaida.
Mwaka jana mwishoni nilikodi bajaj inipeleke uwanja wa ndege, kufika kwenye gate la kuingilia parking akatoka korokoroni mmoja kainua mabega huku akifoka "Bajaj na pikipiki haziruhusiwi kuingia huku, shusha abiria wako ugeuze mara moja"
Hivi hizi kanuni na miaongizo yetu huwa zinatungwa na watu kutoka nje kwa ajili ya wageni tu?.
 
bodaboda tatizo Kubwa linahitaji udhibiti kabla mambo hayajaharibika.. wizi&ajali nyingi wao ndio chanzo, week Hii natoka job natembea pembeni Ya barabara Ya vumbi mtaani napokaa, akapita bodaboda miguu kwangu speed 120,mtoto wa Kama miaka 17 au 20..ningegeuka au kujitingisha ningekufa
 
Jeshi la polisi KAZI mnayofanya Sasa hivi inatia kichefuchefu hasa Kwa mtu anayetambua ugumu wa maisha uliopo. Kukamata pikipiki na Bajaji Katika Hali hii ya ukata nikudhibiti Watu wasitafute riziki.

Mmewanyima vijana ajira ya pikipiki na Bajaji matokeo yake wizi umeshamiri Kwa Kasi kubwa Sana. Lakini tujiulize hizo pikipiki na Bajaji Zina makosa Gani?

Jaribuni kufanya analysis maisha ni magumu sana, msiwasukume vijana kugeuka wezi wakati wameshajiajiri. Tumieni busara, Kama ambavyo mnalipwa mshahara na hautoshi ndivyo hata wengine wanavyoteseka.
Aheri hata madereva wa bajaj, madereva wa boda wengi wajinga wakubwa, hawafuati alama za barabara, hawana tahadhari na wengi utakuta ni walevi. Tena Serikali ilipaswa ije na utaratibu maalum wa kuzibiti hawa watu, hizi ajali zinasababisha mizigo mikubwa kwa familia husika.
 
Acha polisi wafanye kazi yao. Unakuta dereva bodaboda anaendesha kavaa ndala, pikipiki haina bima, element hajavaa, Bado akikamatwa utasema kaonewa?
Na sasa hata sight mirrors wanazitoa, mimi naona polisi hawajafanya kazi yao vizuri kwa hawa watu.
 
NI mjinga pekeyake anaweza kulaumu operation inayoendelea kwasababu ili maisha yaweze kwenda lazima tufuate sheria vinginevyo itakuwa ni Fujo Tu..
kabla ya kuanza Kwa operations hiyo kumefanyika uchumgizi na kubainika kuwa chanzo cha uhalifu uliopo mtaani ni bodaboda Kwa asilimia 75%

ACha Tu na wao wakutane na mkono WA chuma
 
Back
Top Bottom