plo lumumba jr
Senior Member
- Nov 8, 2014
- 111
- 79
We vipi?? Afande Sele ni mjumbe wa kamati kuu ya ACT-Limited katika zile nafasi 5 alizopewa Kiongozi Mkuu 'kumgawia' yeyote amtakae. Wewe humtaki wakati Kiongozi Mkuu ndio tegemeo lake?! Unamkosea adabu mkuu wa kampuni yenuNai-support ACT lakini suala la afande Sele kugombea jimboni Morogoro mjini nitakuwa upande wa Abood.
Siasa ili iende vizuri inataka uhuru wa kufikiri. Mimi ni wale tunao amini katika mtu na chama kinafuata baadae.
mbunge gani analima mabange uko mlimani
Hivi Afande Sele ndio yule mwanamuziki anayepandisha mzuka wa kuvua suruali jukwaani au ni mwingine Abood akifanikiwa kuchapisha hizo picha na kuzibandika Morogoro Mjini hakika Afande Sele atakuwa amejizika kisiasa.
... tofauti yao nini?
"mimi nimetangaza nia ya kugombea ubunge morogoro mjini, lakini lengo langu ni kutaka kuwaonyesha kwamba ubunge siyo kuvaa suti na kuendesha magari makubwa bali ni kutumikia wananchi" afande sele akihutubia mwanza.
afande sele ni either anawashauri wabaya au katolewa kafara sijui hata kwanini zitto hajaliona hili, Abood kung'olewa ubunge na afande sele ni ngumu sana.
Abood ni ile type ya wabunge wasio ongea sana lakini wananchi wanaona wanachokifanya, kwenye top 20 ya matajiri tanzania Abood hakosekani na anatumia utajiri wake kusaidia sana wananchi jimboni mwake.
itakua ni ajabu jingine kutokea tanzania mtu makini kama Abood kushindwa na Afande sele labda ccm wakosee kutompitisha.
Afande Sele bado anajifunza siasa hivyo issue ya kujenga hoja bungeni au kuwakilisha wana morogoro mjini bungeni ni ngumu pia hii nimeona baada ya kumsikiliza akihutubia.
Mkuu wewe ulitegemea kitu gani + kutoka kwa afande sele?
Tanzania kila kitu kinawezekana Wakati Paul Bomani anaangushwa na Paschal Mabiti pale jimboni Mwanza kila mtu alibaki mdomo wazi, ata mzee wetu John Malecela si alipigwa chini na huyu mropokaji Lusinde ??(I stand to be corrected)