Afande Sele Aingia CHADEMA Rasmi Morogoro

Afande Sele Aingia CHADEMA Rasmi Morogoro

huyo ata akienda bagamoyo kugombea ubunge atakuwa mbunge si morogoro tu, kabeba ufalme wa rymes akiwa moro sembuse ubunge.
Kuna viongozi wanahama, wanakufa, wanachoka nk. Inapobidi nafasi hujazwa. Hii inahitaji akili ndogo sana kujua. Mwenyekiti wa kata ya Mafiga alihama, na Afande Sele amekula Bingo. Nakuomba usimuonee wivu, mtie moyo.
 
Ninakumbuka siasa za Jamaica, Bob alisumbua sana. Sijui Morogoro, maana huyu jamaa ni kichwa.
 
Sio kila mwanamziki, ni mbumbumbu, Huyu ukimsikiliza kwa makini kawazidi wabunge wengi sana wa CCM.
 
Karibu JF kwa ID yako rasmi
Ah sitaki kuwa karibu na watu wenye matusi makali, angalia matusi yako "kichwa chako kimejaa kinyesi! Una dementia wewe nenda kwa FaizaFoxy akufanyie massage uanze kupata ndoto za mabikra wa peponi" mimi nakuogopa. Lakini poa.
 
wednesday, Nov 20th 2013

8:55 AM








Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana katika picha. kwa upande mwingine wapenzi wa CCM walionekana kuwa nahofu na uchungu, na walihisi sasa mambo yanazidi kuwa magumu sana kwao.

Kata ya mafiga wa upande wake ilionekana kutekwa kabisa na CHADEMA, huku katika mkutano wa Ndani Afande Sele alichaguliwa kushika nafasi ya Uenyekiti wa kata hiyo, katika kipindi hiki cha kushusha chama kwa wananchi (Program ya Chadema ni msingi), ambayo imekuwa mwiba mkali kwa CCM.





source dj.sek blog
 
Bado Roma pale Tanga kwani kwenye safari ya ukombozi kila mtu aliyetayari kujiunga na harakati anahitajika!! Hongera Afande,boresha busara zaidi
 
Da hila kumtoa yule mbunge wa moro mjini kazI hIPO.
 
Afande Sele karibu sana chadema tuwakimbize wajingawajinga wa ccm..
 
Hongera sana kamanda! Karibu home Chadema.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
...karibu afande,huku wote ni makamanda na tuko mstari wa mbele kuliangamiza dudu moja baya la maccm lililotafuna nchi kwa miaka zaidi ya 50. Vaa gwanda tuchape kazi...
 
...karibu afande,huku wote ni makamanda na tuko mstari wa mbele kuliangamiza dudu moja baya la maccm lililotafuna nchi kwa miaka zaidi ya 50. Vaa gwanda tuchape kazi...
bila shaka atahimili maana alishapitia ligwalide pia..
 
ni swala la kumshukuru mungu,kwani waTanzania wanaanza kumsikia mwenyezi Mungu mwenyewe,kwani ndo aliyeumba tawala zote,duniani na mbinguni kwa nia njema ya kuongoza wanadamu,wahishi vizuri duniani na baadaye mbinguni.CCM imeasi katika ilo,imetufisadi na kutusababishia mahisha Magumu.Nasasa mungu kaichagua CDM kuwaongoza watu wake,kuwapa matumaini mapya na neema tele.Haya sasa ni kazi yetu wanadamu kutii sauti ya Mungu na Kujiunga na hatimaye kuichagua CDM itupeleke kwenye neema.Amen
 
Huyu jamaa ni kichwa, nilimsikiliza kidogo tu, na mikakati aliyonayo, huwezi amini, ni msikivu, muelewa na ana busara. Ila itabidi aachane na baadhi ya mambo, ili kuwatia moyo wafuasi wa CDM. So far so Good.
 
Back
Top Bottom