Afande kova upo?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande kova upo??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,185
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Majambazi yenye silaha yametikisa sehemu ya Jiji la Dar es Salaam jana baada ya kumwaga risasi kadhaa kwenye bar moja na kupora wateja fedha na mali kabla ya kufanya hivyo pia kwenye duka moja na kujeruhi kwa risasi na mapanga.
  Matukio hayo, yametokea usiku wa kuamkia leo pale kwenye maeneo la Tabata Chang'ombe na Tabata Segerea Jijini.
  Katika uvamizi wa maeneo yote hayo, watu kadhaa wamejeruhiwa, akiwemo mmoja ambaye yuko hoi baada ya kupigwa risasi na kisha kukatwa mapanga kadhaa mwilini kabla ya kuporwa pesa na vitu mbalimbali dukani kwake.
  Tukio mojawapo limetokea mishale ya saa 5:00 usiku katika mtaa wa Ugombolwa Machimbo, maeneo ya pale Tabata Segerea Jijini.
  Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, wamesema kuwa usiku wa jana, watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia duka la Jim Marley na kabla ya kumpora, walimpiga risasi mbili begani na kisha kuanza kumkatakata kwa mapanga.
  Shuhuda mmoja ameiambia Alasiri kuwa mbali na Marley kupigwa risasi, pia alikatwa panga lililoondoa kabisa kiganja chake cha mkono wa kulia.
  "Watu hawa hawakuwa na huruma hata kidogo. Ingawa walishampiga risasi, waliendelea kumkatakata mapanga na mbaya zaidi, wameondoa kabisa kiganja chake hicho cha mkono," akasema shuhuda huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
  Akasema wakati wa tukio hilo, watu wote katika eneo hilo walilazimishwa kulala chini, huku wengine wakitimua mbio kutokana na hofu.
  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa lilijiri usiku wa kuamkia leo.
  Akisimulia tukio hilo, Kamanda Shilogile amesema kundi la watu watatu waliokuwa na silaha za jadi ikiwa ni pamoja na mapanga na shoka, huku mmoja wao akiwa na bunduki, walianza kwa kuvamia bar moja iitwayo Machimbo Pub, iliyopo katika maeneo hayo.
  Akasema katika bar hiyo, majambazi hao waliwateka wateja wote waliokuwa wakijichana kwa vilaji, kisha wakaanza kuwapekua na kuwapora mali zao zote, ikiwa ni pamoja na simu na fedha.
  Akasema baada ya hapo, majambazi hayo yalikwenda kwenye kaunta ya bar hiyo na kupora tena fedha, kiasi cha shilingi 70,000 na simu nyingine moja ya mkononi.
  Kamanda Shilogile amesema baada ya majambazi hayo kuondoka kwenye bar hiyo, ndipo yalipokwenda kwenye duka moja lililo jirani na maeneo hayo na kumjeruhi mwenye duka kwa kumpiga risasi na kumkatakata mapanga.
  Hata hivyo, Kamanda Shilogile akasema mali zilizoporwa na majambazi hao ndani ya duka hilo bado hazijajulikana na majeruhi alikimbiziwa katika Hospitali ya Amana ambako hadi sasa anaendelea kupatiwa matibabu.
  Aidha, Kamanda Shilogile amesema Polisi wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo ili waweze kufikishwa mbele ya sheria.
  Hata hivyo, wakati polisi wakiendelea na jitihada za kusaka wahalifu hao, baadhi ya wakazi wa maeneo hayo ya Tabata Segerea na Tabata Chang'ombe, wamesema hivi sasa wamekuwa wakikabiliwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara na kwa wiki nzima sasa yamekuwa yakitokea mfululizo.
  Mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la James, amesema tangu Jumapili iliyopita, hali imekuwa si shwari katika mitaa yao na kwamba hivi sasa, wengine wanaogopa hata kukaa bar na kustarehe kwa amani.
  Akasema Jumapili iliyopita, majambazi walivamia duka moja la jumla maeneo ya Tabata Chang'ombe, lakini kwa bahati nzuri wakakuta limeshafungwa.
  Akasema hata hivyo majambazi hao waliamua kwenda nyumbani kwa mwenye duka, lakini naye hawakumkuta kwa vile alikuwa amekwenda kwenye sherehe za 'kitchen party', hivyo wakaishia kupora vocha za simu nyumbani kwa mfanyabiashara huyo na kisha yakatokomea kusikojulikana.
  Wakati huohuo, majambazi mengine mkoani Singida yameteka gari moja lililokuwa na abiria na kisha kupora fedha, simu na mali nyingine kibao.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Celina Kaluba, amesema tukio hilo limetokea hivi karibuni, mishale ya saa 2:00 usiku, huko katika daraja la Kijiji cha Doroto, barabara ya Itigi - Mgandu wilayani Manyoni.
  Akasema gari hilo lililoporwa, lilikuwa na abiaria sita na namba zake za usajili ni T 701 AYB, aina ya Mitsubishi Fuso, mali ya Mushi Hassan, mkazi wa Kijiji cha Mgandu.
  Akasema gari hilo lilikuwa likitokea kijiji cha Mgandu kwenda Dodoma na lilikuwa likiendeshwa na dereva Omari Rashidi.
  Akasema lilipofika kwenye eneo hilo, gari hilo lililazimika kusimama baada ya kuwekewa kizuizi cha mawe makubwa katikati ya barabara na majambazi, kabla abiria kunyangÂ’anywa simu zao na pesa zinazofikia kaisi cha shilingi 549,100.
  Akasema majambazi hayo yalikuwa na marungu, fimbo, mawe pamoja na mapanga.
  Bado tunaendelea kuwasaka majambazi hao ili waweze kufikishwa mbele ya mkono wa sheria," akasema Kamanda Celina.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  edit bandiko lako weka paragraphs
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  eti bandiko!
   
 4. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kumbe?Au kabandua?Lol...
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  hii hatari sasa kunajika huko?
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Pdidy vipi leo, hili bandiko uliliweka ukiwa unatembea?
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,185
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  kaka nilikuwa na usingizi usiku nikalimwaga kumradhi....
   
 8. J

  Jahom JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 349
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Pamoja na editorial comments, ni vema tukaijadili mada. Polisi wameanza tena syndicate na matukio yanayoongezeka. Kwa hakika kuna waliopiga simu kuwafahamisha kuhusu matukio hasa yale yanayochukua mpaka nusu saa, na mara majambazi wanapokamilisha kazi, ndipo polisi hutokea. Inawezekana ni woga wa kuuawa kwenye mapambano pia. Lakini kwa sasa ukikamatwa na polisi kwa tuhuma yoyote, wengi wao hutumia fulsa hiyo kama mradi kutokana na juhudi za mtuhumiwa kujinasua. Kuna jamaa alikamatwa na askari wenye pikipiki wanaoonekana kama wapiganaji lakini hatujasikia hata shughuli yao yenye akili, kwa kosaa dogo la traffic. Walifanya fujo ya kuanza kubambika makosa hata wasiyoyajua, huku silaha zao za moto zikiwa standby! Walipoona kuwa waliyemkamata ni mbishi, wakaambizana "waache waende hawana hela hawa". Je, inawezekana wamepewa malengo ya makusanyo badala ya kudhibiti uhalifu?
   
Loading...