Afadhali ya Magufuli

Afadhali ya Magufuli

Mmeshaanza kutubu wakati mlisema Bora Magufuli afe aje yeyote yule kutakuwa safi .

Ndio maana Kiranga alisema wabongo wanaangalia simple solution kwenye ishu ngumu ambazo hazihitaji shortcut na wengi hawana principlees wanaangalia mtu .
 
Mmeshaanza kutubu wakati mlisema Bora Magufuli afe aje yeyote yule kutakuwa safi .

Ndio maana Kiranga alisema wabongo wanaangalia simple solution kwenye ishu ngumu ambazo hazihitaji shortcut na wengi hawana principlees wanaangalia mtu .
Hawa hawaelewi kuwa kuna mengi yanayoendelea sasa yasingewezekana bila kuwekewa msingi na Magufuli.

Hawaelewi uongozi wa CCM ni kama mbio za kupokezana kijiti, na unachoona kinatokea sasa kisingeweza kutokea hivi bila ya hao wa awali kuweka mazingira ya haya kutokea.

Wananikumbusha kuna wakati nilikaa na rafiki zangu, tukawa tunauchambua uongozi wa Kikwete. Mmoja akasema Kikwete ni rais dhaifu sana, mbovu sana, hatakuja kamwe kutokea rais mbaya kama Kikwete Tanzania.

Mimi nikawaambia tulieni tu, mtaona zaidi.

Nilijua kuwa, ubaya wowote atakaoufanya Kikwete, ataufanya uwe wa kawaida kwa anayemfuatia, na anayemfuatia atafanya ubaya zaidi, kwa sababu Kikwete atakuwa kashashusha standards. Kaweka "the new normal" ya standards za chini zaidi. Ni kama viongozi wanashindana kuharibu.

Na kweli, baada ya Kikwete akaja Magufuli akafanya vilevile nilivyosema. Mpaka watu wakawa wanamtamani Kikwete arudi kipindi cha Magufuli.

The same thing is happenning now. Magufuli kashusha standards, Samia kaziondoa kabisa.

Watu wanamuona Magufuli afadhali, lakini hawaelewi haya madudu ya Samia yasingewezekana kama Magufuli asingeshusha standards.
 
A man hears what he wants to hear and disregards the rest. Paul Simon
 
Magufuli ndiye alianzisha dhuluma ya utekaji, upotezaji, uuaji wa watu wanaompinga.
By comparison, afadhali ya Uovu wa magufuli kuliko wa sasa
Samia huyu hata shetani mwenyewe anamvulia kofia, kuua watu 23,000 kwa siku nne tu hii rekodi ya juu sana, huyu akifa anaenda kuwa kuni za kuwachomea waovu wenzake
 
Huu uongo.
Watu walipigwa mabomu Arusha na kuvunjwa mikono.
Dr. Ulimboka alitekwa na kunyofolewa kucha.
Muandishi wa habari Saed Kubenea alimwagiwa tindikali usoni.
Muandishi na Mhariri Absolom Kibanda alitekwa.
Muandishi wa habari aliuwawa na polisi kwenye maandamano ya CHADEMA mkoani Iringa.
Kiongozi wa vijana waliopitia JKT na kukosa ajira wakanzisha harakati za kudai ajira lilimkuta jambo baya.
Dr.Sengondo Mvungi aliuwawa nyumbani kwake.
Wachimbaji wadogo wa madini toka Mahenge waliokamatwa na kuuwawa mikononi mwa polisi.
Masheikh wa Uhamsho walikuwa wanavamiwa majumbani kwao Hadi usiku na kukamatwa kwa mtindo huu wa sasa wa kutekwa.
Orodha ndefu sana.
Naamini karibu kila awamu kulikuwa na matukio yanayo fanana na haya.
Kutekwa na kutupwa msitu wa Mabwe Pande ilikuwa matukio maarufu sana enzi za Kikwete.
Wanafunzi wa UDSM walipigwa mabomu sababu ya mgomo kudai pesa ya mkopo ya kujikimu (Boom) iongezwe.
 
Hakuna afadhali yoyote tena huyo ndio alikua mkufunzi wa huu ushenzi.
 
Back
Top Bottom