GE2025 Adv. Stephane Byabato ampigia chapuo wananchi Eng. Mutasingwa, Ubunge Bukoba Mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

ADV. STEPHEN BYABATO AMPIGIA CHAPUO KWA WANANCHI ENG. MUTASINGWA, UBUNGE BUKOBA MJINI

Salaam sana ndugu zangu

Naomba tusambaze ujumbe huu

Leo jumatatu ni siku ya tatu tangu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iteue wagombea Ubunge na Bukoba Mjini ikatuletea ndugu yetu Eng Johnston Johansen Mutasingwa, tumempokea kwa mikono miwili kama ilivyo jadi yetu katika Chama chetu.

Wakati wa mchakato kila mtia nia alipata kuungwa mkono na watu kadhaa, mwisho wa mchakato maamuzi ya H/Kuu yametupatia jina moja ambavyo kwa vyovyote ilitakiwa mwisho apatikane mmoja katika wale makada wetu wazuri 5, Mwenyezi Mungu kampa nafasi Eng. Mutasingwa.

Kwa siku mbili hizi kumekuwa na furaha au masikitiko au kuwa kawaida kwa watu mbalimbali kulingana na mapokeo ya uteuzi, hili lazima litokee, lakini halitakiwi kudumu. Kitaalamu wanasema ukiwa na jambo ndani ya moyo inabidi ulitoe ili upone nafsi lakini lisipitilize kiasi na kuleta madhara.

Ni kwa mantiki hiyo, mimi Adv. Stephen Byabato (Mbunge niliyemaliza muda wangu Jimbo la Bukoba Mjini) nawaomba wana CCM na wana Bukoba wote sasa tuungane kumpa ushirikiano mteule wetu ili turudi kazini mapema na kuijenga Bukoba yetu. Kwa sasa naamini kila mtu amepumua na hatujafika kwenye madhara, na tusifike huko na atakayetaka kutupeleka huko tumkatae na tumuone ni adui wa Bukoba yetu na sasa sote tuwe tayari kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha Mgombea kwa tiketi ya CCM anapata ushindi wa kishindo ili Bukoba tuzidi kusonga mbele.

Ninawaomba na kuwasihi wapenzi wa kila upande sasa tuwe wamoja, tuvumiliane, tukubaliane, tushirikiane na ni kwa ajili ya maslahi mapana ya kuleta maendeleo ya Bukoba Mjini.

Asanteni sana. Ndimi kijana wenu

Adv. Stephen Byabato
Bukoba Mjini
25/07/2025

Screenshot 2025-08-25 at 15-35-59 Instagram.png
 
Amefanya vizuri! So far chama kina manafasi mengi kuna moja atapata huyo Byabato
 
Na huu ndip ujinga uliowajaa maccm kusubiri mkono wa binadamu kama fisi.

Yani watoto wao wapendwa hawakatwi kina Ridhiwani, Wanu, Salma Kikwete etc, wewe unakula mkasi halafu unajifanya kuunga mkono upuuzi mtupu.

Pambanieni reforms ili mtu agombee ubunge hata bila kupitia vyama, kama watu wanakupenda watakuchaguwa kama mgombea binafsi.
 
Pole kwa maumivu
 
ADV. STEPHANE BYABATO AMPIGIA CHAPUO KWA WANANCHI ENG. MUTASINGWA, UBUNGE BUKOBA MJINI

Salaam sana ndugu zangu

Naomba tusambaze ujumbe huu

Leo jumatatu ni siku ya tatu tangu Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iteue wagombea Ubunge na Bukoba Mjini ikatuletea ndugu yetu Eng Johnston Johansen Mutasingwa, tumempokea kwa mikono miwili kama ilivyo jadi yetu katika Chama chetu.

Wakati wa mchakato kila mtia nia alipata kuungwa mkono na watu kadhaa, mwisho wa mchakato maamuzi ya H/Kuu yametupatia jina moja ambavyo kwa vyovyote ilitakiwa mwisho apatikane mmoja katika wale makada wetu wazuri 5, Mwenyezi Mungu kampa nafasi Eng. Mutasingwa.

Kwa siku mbili hizi kumekuwa na furaha au masikitiko au kuwa kawaida kwa watu mbalimbali kulingana na mapokeo ya uteuzi, hili lazima litokee, lakini halitakiwi kudumu. Kitaalamu wanasema ukiwa na jambo ndani ya moyo inabidi ulitoe ili upone nafsi lakini lisipitilize kiasi na kuleta madhara.

Ni kwa mantiki hiyo, mimi Adv. Stephen Byabato (Mbunge niliyemaliza muda wangu Jimbo la Bukoba Mjini) nawaomba wana CCM na wana Bukoba wote sasa tuungane kumpa ushirikiano mteule wetu ili turudi kazini mapema na kuijenga Bukoba yetu. Kwa sasa naamini kila mtu amepumua na hatujafika kwenye madhara, na tusifike huko na atakayetaka kutupeleka huko tumkatae na tumuone ni adui wa Bukoba yetu na sasa sote tuwe tayari kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha Mgombea kwa tiketi ya CCM anapata ushindi wa kishindo ili Bukoba tuzidi kusonga mbele.

Ninawaomba na kuwasihi wapenzi wa kila upande sasa tuwe wamoja, tuvumiliane, tukubaliane, tushirikiane na ni kwa ajili ya maslahi mapana ya kuleta maendeleo ya Bukoba Mjini.

Asanteni sana. Ndimi kijana wenu

Adv. Stephen Byabato
Bukoba Mjini
25/07/2025

Akina kamala wana maumivu makali sana byabato amewapiga bao la kisigino
 
Mfyuuuuuu! Wakati akiwa Waziri alikataa kupokea simu za wapiga kura, sasa hivi anajichekesha Jamii Forum
 
Na huu ndip ujinga uliowajaa maccm kusubiri mkono wa binadamu kama fisi.

Yani watoto wao wapendwa hawakatwi kina Ridhiwani, Wanu, Salma Kikwete etc, wewe unakula mkasi halafu unajifanya kuunga mkono upuuzi mtupu.

Pambanieni reforms ili mtu agombee ubunge hata bila kupitia vyama, kama watu wanakupenda watakuchaguwa kama mgombea binafsi.
Mtikila licha ya kuwa na chama lakini alipigania wagombea binafsi bila kupitia chama.
Uhuru wa mbunge unapungua akiogopa kwenda kinyume na msimamo wa chama,japo alichaguliwa na watu wa vyama na wasio na vyama.
 
Back
Top Bottom