Adui yako mnunulie bodaboda

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,332
12,631
Wazungu wana msemo wao unaosema adui yako mnunulie pikipiki itampa adhabu inayomstahili. Wakimaanisha kuwa mwendesha bodaboda lazima tu litamkuta jambo baya sana, kama sio leo basi kesho na kesho kutwa.

Madhara wanayopata waendesha bodaboda ni makubwa sana kuliko hela wanayoipata. Pesa nyingi wanayoipata inaishia kwenye kujitibu magonjwa yanayotokana na kuendesha bodaboda, faini za polisi barabarani, matengenezo ya bodaboda na mazishi ya wenzao wanaokufa kwa ajali za bodaboda.

Ili kujua kama pale kuna kituo cha polisi utajulishwa na wingi wa bodaboda zilizorundikana kwenye kituo cha polisi kwa makosa na ajali za madereva w bodaboda. Kwenye hospitali zetu ajali za bodaboda zimejaza vitanda vyote vya hospitali na wengine kulazwa chini.

Waendesha bodaboda ni lile kundi la watu ambao wanaugua sana magonjwa na vifua na mafua, mgongo, uchovu mwingi, msongo wa akili, ukosefu wa nguvu za kiume, majeraha ya mara kwa mara, na upungufu wa maji na lishe mwilini. Vijana hawali, wanashindia vinywaji vya energy (mo, azam, jembe) usiku kucha ili kulinda hesabu ya boss, familia na kodi ya geto.

Na hii ndio maana unasikia vijana wengi siku hizi wakilalamika kuhusu ukosefu wa nguvu za kiume, kutekwa na kuawa, kuporwa, nk. Wako kwenye risk kubwa sana mno kuweza kuiita bodaboda ni ajira.

Asitokee Mwanasiasa atakaejigamba kama ametoa ajira ya bodaboda kwa vijana, huo utakuwa ni uongo. Asilimia 97 ya vijana wanaendesha bodaboda ambazo sio zao wenyewe, wanapeleka "hesabu" kwa mabosi zao wamiliki wa bodaboda hizo.

Wanaofaidika na bodaboda ni wale wenye bodaboda lakini sio wale wanaoendesha bodaboda. Mmiliki wa bodaboda atakwambia bodaboda ni biashara nzuri na ajira lakini kwa mwendesha bodaboda ni hasara na misiba tu.

Taifa litafute ajira sahihi na salama kwa vijana wake.
 
Juzi nilifata mzigo godown huko sokota, ili kukwepa foleni nikapanda boda niwahi kufika, Kwa jinsi jamaa alivyokuwa anajipenyeza katikati ya malori, aisee ule usafiri ni kifo mkononi, mpaka tunafika tulikuwa tumekoswa koswa mara kibao, sa nikajiuliza huyu anaendesha kila sku na kila saa, atakoswa koswa mara ngapi.

Tulipofika nilimchana pale pale nikamwambia daah mkuu hii biashara yenu mnaishi Kwa rehema za Mungu tuu na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom