Adui wa Samia siyo Lissu wala Chadema.

Adui wa Samia siyo Lissu wala Chadema.

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,167
Reaction score
14,515
Nalizungumza suala hili kwa mara nyingine tena, niliwahi kulisema hili miaka 3 nyuma. Adui wa Samia na CCM yake kwa ujumla siyo Lissu wala Chadema bali ni wanachama wa chama cha Mapinduzi wenyewe. Kinachotokea sasa ni mwangwi wa mshindo mkubwa ambao umeshatolewa. Chama cha Mapinduzi kinaishia kwa namna ya ajabu sana na hakitaki kubadirika. Wakati wa Uanzishwaji wa mfumo wa vyama vingi chama kwa kauli moja kilikataa mapendekezo ya kuruhusu watu wawe na vyama mbadala vya kisiasa. Nyerere kwa kujua wakati ni ukuta akasema hapana lazima tujue adui wa ndani ni mbaya kuliko wa nje na hii ikamfanya aamue kuweka pembeni mambo ya chama na kuruhusu hekima ifanye kazi kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi. Miaka 20 baadae CCM kwa kujaa kiburi na majivuno wanakataa tena mfumo wa vyama vingi kwa kulazimisha udikteta kwa kimfumo. China hawana upumbavu kama huu japo ni marafiki wa CCM, Cuba wanaheshimu utu wa watu, venezuela wanalinda misingi ya utu. CCM wametengeneza uasi kwa kisingizio cha kulinda amani hata kwa kuua wapinzani wao... Hii hata miaka 1000 mbele bado itawaletea shida tena kubwa kwenye vizazi vyenu. CCM achaneni na siasa za kihuni kubalini kurudi kwenye mfumo wa haki ili kila mmoja afurahie kuishi hapa nchni.
 
Back
Top Bottom