Adui wa mpenzi wako ni adui wako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adui wa mpenzi wako ni adui wako?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Sep 12, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hili ni vizuri mkalijadili na pengine kuwasaidia wengine.....

  Huwa inatokea wakati mwingine unaweza kuwa na jirani au jamaa

  ambae ni chui na paka na mpenzi wako......

  Swali ni hili ,kama mtu wewe humpendi kabisa.ni sahihi au sio sahihi...
  Kumtaka mpenzi wako nae awe mbali au asiongee na huyo mtu????????????

  Hivi ikitokea mtu usiempenda ana urafiki na mtu wako inakuwaje??????

  Nimeona hili kwenye mahusiano mengi linasumbua............
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ....................
   
 3. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  conflict of interest hapo. Utakuwa unaongea nini na adui wa rafiki yako? Si ndio unaweza ukapeleka habari bila hata ya kujua kuwa unatoa habari usiyopaswa kutoa. kujibu swali lako, kwa maoni yangu siyo adui yako, bali punguza mazoea naye.
   
 4. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  japo si sahihi kumchagulia mtu marafiki... ni busara kuwa muwazi kwa mwenzi wako kuwa hauelewani na na huyo mbaya wako na hivyo mwenzako awe makini na urafiki naye.... itakuwa balaaa kubwa pale utakaponyamaza kimya afu ukatokea msuguano kati yenu na ukabaini chanzo ni huyo jirani/mtu usie na maelewano nae!! :smile-big:
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhhhhhhh
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mimi adui wa mke wangu ni adui wangu pia. hata kama mke wangu ana kosa, mtu akijaribu kumgusa kwa tusi au kwa lolote, anagusa mboni ya jicho langu. nashukuru Mungu amenijalia kuheshimiwa na watu wote mtaani, na mara nyingine wanashindwa kumfanya lolote my waifu wangu kwasababu wanajua mume wake hana mchezo...kama waifu amekukosea, njoo nishitakie, hakika nitamweka kitimoto, kama ukishindwa kunishitakia, nenda mahakamani. ukona huji kunishitakia, huendi mahakamani etc, nyamaza kimyaaa! jifanye kama hakuna kitu..ukileta za kuleta utapambana ne mimi mwenyewe.

  kuna wanawake fulani hivi nusura watenganishe ndoa yetu mimi na waifu,..wao wanaishi na wanaume bila kuoana, sasa wakawa wamepanga kusingizia maneno ili mimi nimchoke waifu nimtimue kwasababu wao walikuwa wanaona wivu kwa aliyefunga ndoa. ukitokea mnong'ono wowote tu, au uzushi kwa kusemana, kusengenyana au minong'ono ya wanawake, wanasema ni mke wangu afu wote wanakuja juu. mimi niliwaacha tu sikupenda kuingilia mambo ya kike, wakazidi, ikafika kipindi siku moja nimerudi kazini mchana wakaja wanataka kumvamia wafu wangu wampige...waifu ni kamanda kama mimi mwenyewe, bahati yake mbaya alimkamata mmoja wao akarusha kama karatasi ya kaki...wengine wakaogopa...ilibidi nitokee (hawakujua nipo, walijua kaenda kazini)...walilowa kama wamemwagiwa maji ya mchina, sikuwafanya kitu, niliwaita mmoja baada ya mwingine aje kujieleza (sikujali waume wao wala nini), walikuja kujieleza mmoja baada ya mwingine, nikawapa vidonge vyao mmoja baada ya mwingine kuwa mimi sitaki fujo, anayegombana na mke wangu anagombana na mimi...tuache ugomvi, mkiendelea hamtaniweza, nitawamaliza...mkija kwa ngumi mimi ni boxer, mkinikodia majambazi, nitawakamata kwanza niliwaweka kwenye suspects hata mke wangu akirushiwa jiwe tu niliwaambia watakuwa wao na mimi ni mwanasheria....wakienda kiroho kujaribu kuleta mambo ya kiswahili/uchawi nitawalipua na watateketea....nitayarudisha yote wanayonitumia yawakute wao...kwa Jina la Yesu lakini si kwa uchawi..

  kuna mtu mmoja alishawahi kutaka kuniloga, kumbe mimi asubuhi huwa naomba maombi "mashimo watakayonichimbia watumbukie wenyewe, mtego watakao nitegea uwanase wenyewe"..yale yote aliyotaka yanikute yalimkuta yeye mwenyewe moja baada ya lingine....hadi leo hii heshima mbele...
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu yani upo kama mm atujapishana ata kidogo
   
 8. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duh mzee unajisifia utadhani unaiweza dunia yote. Angalia sana avumaye baharini papa kumbe wengine wapo.......Sio lazima ujisifie na stori kibao ili ueleweke. Wewe hata kama ni boxer unadhani ndo utampiga kila mtu bwana. Kapigwa tyson, Muhammad Ali na wengineo itakuwa wewe.
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hahaha, wala mi sio boxer mkuu, nilikuwa najitapa tu, sijawahi kuwa boxer na sitaki kuwa boxer...ulikuwa msisitizo to, hata hivyo hata kupigana huwa sipigani, ni dhambi kwangu, huwa natumia akili zaidi kuliko manguvu..usihofu, usije ukawa unaogopa hewa!
   
 10. MankaM

  MankaM JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2014
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 9,493
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  me namweleza ukweli kuwa huyo rafiki yake simpendi
   
Loading...