Adsense payments methods

dumejm

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,180
Reaction score
861
Habari zenu wakuu.
Naomba msaada wenu wakuu ..

Hivi ni njia gani ambayo ni rahisi kupokea google adsense payments kwa hapa nchini kwetu Tanzania. Au ni njia zipi zinatumika kupokea malipo kutoka google adsense kwa hapa Tanzania...

Naombeni msaada wenu wakuu wenye uzoefu na haya mambo.
 
Msaada wenu wakuu
 
JINSI YA KUPOKEA PESA YAKO KUTOKA ADSENSE



Habari na karibu katika ukumbi huu maridhawa kwaajili yako , kutokana na maombi ya baadhi ya wasomaji wangu kuhitaji kufahamu jinsi ya kupokea pesa zao kutoka adsense leo nimeonelea wacha tujuzane kuhusu hili, ispokuwa nitaeleza kwa upande wa bank tu hizi njia nyingine tutaelezana wakati mwingine au hata kwa kupitia maoni.

kwanza fahamu jambo muhimu kuwa adsense wanawatumia pesa zao wateja wake kuanzia dola 100, pia ili kujua jinsi ya kurekebisha mambo mpaka pesa yako itumwe kwenye bank akaunti yako lazima ufikishe dola 10 na google watakutumia (PIN) Kupitia sanduku lako la barua ulilojaza wakati unajiunga nao,

mfano wa PIN utakayotumiwa na google
Ukiingia katika akaunti yako ya adsense kama umeshafikisha dola 10 utaona sehemu wanakuomba ujaze PIN yako waliyokutumia , fanya kama walivyokwambia jaza PIN yako kutoka katika barua hio uliokwenda kupokea posta, ukisha jaza nenda sehemu iliyoandikwa payment setting

Hapo katika setiing kuna vipengele vingi ila sisi tutazungumzia kuhusu kujaza data zako za bank basi, bonyeza new form of payment kisha chagua wire transfer to bank account kisha jaza form utakayopewa ila kabla ya kujaza lazima ujue SWIFF za bank yako kwa hiyo lazima uwasiliane na bank yako ila kama unatumia equity swif zao ni hizi ( $ : EQBLTZTZ, na kwa pesa tofauti na $ ni hii, EQBLKENA)
baada ya kujaza form yao hiyo baasi utakuwa umeshamaliza kila kitu pindi pesa yako itakapotumwa utajulishwa kupitia email yako na kama unatumia sim banking utajulishwa na sms kutoka bank

Share na marafiki kama makala hii itakuwa imekusaidia au kama umeipenda Riyadi Bhai hapa fanya kuniachia maoni yako ili nikusaidie zaidi unaweza kunitumia maombi yako kuwa kitu gani nikifafanue kuhusu Adsense kupitia riyadibhai@gmail.com
 
Hapa TZ kuna njia tatu tu. Ya kwanza ni kwa kutumia Western Union( hii ni njia rahisi kuliko zote haina makato)

Ya pili ni wire transfer na ya tatu ni check unatakayotumiwa kwa posta mail
 
Shukrani sana mkuuu
 
Njia ni mbili aidha kupitia Benki au Western Union mkuu..kwa msaada zaidi nicheki 0653737353 nikuelekeze
 
Kwanza nielekeze hyo Google AdSense ni nini?
Kama hujui hata hiyo google assense ni kitu gani.. ni vyema kuachana kabisa na hii thread maana haita kusaidia kitu...
 
Kama hujui hata hiyo google assense ni kitu gani.. ni vyema kuachana kabisa na hii thread maana haita kusaidia kitu...
[emoji15] [emoji15] [emoji15] .sawa endelea kujua peke yako.maana umezaliwa unajua mwenzangu.
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] .sawa endelea kujua peke yako.maana umezaliwa unajua mwenzangu.
[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…