GE2025 Ado Shaibu: Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma asimamishe kazi alizonazo ashughulikie tatizo la wafugaji na wakulima

GE2025 Ado Shaibu: Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma asimamishe kazi alizonazo ashughulikie tatizo la wafugaji na wakulima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Wakuu

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu, amemkosoa vikali Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kile alichokiita kupuuzia mauaji yanayoendelea katika mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Tunduru.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Jana October 05,2025 , Ado Shaibu alisema “Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anapaswa kuwajibika kwa kupuuzia roho za Wanatunduru wanaochinjwa kama kuku kwenye mgogoro wa wafugaji na wakulima. Tunamtaka aache anachofanya huko Songea aje kushughulikia tatizo hili kama Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa.”

Kauli hiyo imekuja kufuatia matukio ya uvunjifu wa amani na vifo vinavyoripotiwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tunduru, hali inayozidi kutia hofu wakazi wa eneo hilo.

Matamshi hayo yalitolewa wakati wa kampeni yake ya Kijiji kwa Kijiji, ambayo hadi sasa imefikia vijiji 73 kati ya 92 vya Jimbo la Tunduru Kaskazini

 
Back
Top Bottom