Ado Shaibu: Kauli za Rais Magufuli sio za KiUrais, aache

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Wafanyakazi na Wanafunzi Shikamaneni Mdai Haki Zenu

- Kuweka Sawa Ukweli Juu ya Maslahi ya Wafanyakazi, Ushiriki wa Wanavyuo Kwenye 'Siasa', na Ubaguzi Kwenye Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini.

- Mapitio ya Kauli, Miongozo na Taarifa za Rais na Serikali Katika Majuma Mawili ya Mwezi Mei.

Utangulizi:

Kati ya Aprili 30 na Mei 7, 2018, ndugu Rais alifanya ziara ya kikazi kwenye mikoa ya Iringa na Morogoro. Katika kipindi hicho pia alihutubia maadhimisho ya kitaifa ya sikukuu ya Wafanyakazi ulimwenguni, Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa Mkoani Iringa.

Akiwa kwenye ziara hiyo ya wiki moja, ndugu Rais alitoa matamko, misimamo na mitazamo mbalimbali inayoonesha dira na mwelekeo wa Serikali anayoiongoza kwenye maeneo mbalimbali ya Kisera na Kiuongozi nchini.

Kwenye nchi zenye Demokrasia thabiti, pana na hai, matamko na misimamo hii ya Rais huwekwa kwenye mizani, huhojiwa na humulikwa (Scrutinized) kwa sababu ya athari zake kwa umma, kutokana na nguvu ya Taasisi ya Urais kikatiba na ile ya kimabavu iliyotamalaki kwenye nchi nyingi za Kiafrika. Kauli za Rais, hazipaswi kutazamwa kama vichekesho, mzaha au maneno ya kawaida.

Wajibu wa kuzimulika kauli na maelekezo ya Rais na Serikali nzima ni wa Mhimili wa Uwajibikaji (Bunge), Vyama vya Siasa (hasa vya Upinzani), Asasi za Kiraia, pamoja na Umma kwa ujumla. Utaratibu huo wa kumulika na kuhoji kauli na mwenendo wa Rais na Serikali kwa ujumla kwa sasa ni kama haupo nchini. Sisi ACT Wazalendo tumeona tuuanzishe, na ziara hii ya Rais tumeonelea ndio iwe eneo la kuanzia.

Chama chetu kimefuatilia mkutano kwa mkutano na kuchambua hotuba kwa hotuba, kauli kwa kauli, na hata neno kwa neno katika ziara yote ya Rais. Katika uchambuzi huu tutatoa maoni yetu kwenye maeneo matatu yatokanayo na ziara hiyo, pamoja na mwendelezo wa kauli za Serikali kupitia taasisi zake, ambayo tunadhani ni muhimu yamulikwe kwaajili ya umuhimu wake kwa Taifa.

Tutazungumzia maeneo matatu muhimu; Maslahi na haki za wafanyakazi nchini, Ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu kwenye siasa na kudai haki zao, pamoja na Sera za Kibaguzi za Serikali kwenye kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu.

A: Maslahi na Haki za Wafanyakazi Nchini

Tofauti na matarajio ya wafanyakazi ya kupata nafuu kwa kupata nyongeza ya mshahara siku ya Mei Mosi, Rais aliweka bayana msimamo wa Serikali yake wa kutoongeza mshahara mwaka huu, na kuweka msisitizo wa serikali kutotangaza ajira nyingi Kama ilivyotarajiwa.

Kisingizio cha mambo hayo yote mawili ni kile ambacho Rais anakiita matumizi ya fedha nyingi kwenye miradi mikubwa ya miundombinu, hasa reli, usafiri wa anga na barabara. Kwamba badala ya kutumia fedha nyingi kwenye nyongeza ya mishahara, kulipa malimbikizo ya madeni ya wafanyakazi na kuajiri wafanyakazi wapya kwa wingi, ameona ni bora kuelekeza nguvu zake kwenye miradi.

Kwanza, ni lazima tukiri kwamba tunashukuru sasa Rais na Serikali yake wamekiri kinachomfanya washindwe kutoa ajira mpya nyingi zaidi, kuongeza mishahara, pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya wafanyakazi nchini ni uhaba wa fedha (Kama ambavyo ACT tumekuwa tukisisitiza) badala ya kisingizio cha muda mrefu cha uhakiki wa wafanyakazi.

Malengo ya ACT Wazalendo kwa mwaka 2018 ni pamoja na kushirikiana na Vyama vya Wafanyakazi ili kudai haki zao, hivyo tunasema yafuatayo:

1. Ongezeko la mishahara ya Wafanyakazi ni la Kisheria. Si la Utashi wala Hisani ya Rais:

- Kauli za huko nyuma za serikali zinaonyesha hadaa ya serikali juu ya Jambo hili. Awali, serikali iliahidi kuongeza mishahara baada ya kukamilisha uhakiki wa wafanyakazi (ambao ungefanyika ndani ya miezi miwili), kisha pia Serikali ingeendelea kulipa malimbikizo ya madeni ya Wafanyakazi, na kuajiri wafanyakazi wapya. Ahadi hii imetolewa pia bungeni chini ya Waziri Angela Kairuki. Ni miaka mitatu sasa hili halijafanyika.

2. Serikali Inawadharau Wafanyakazi Pamoja na Kuwa wana Mchango Mkubwa:

- Matendo ya Serikali yanaonyesha dharau na hadaa kwa wafanyakazi, pamoja na kuwa wafanyakazi wanalipa mara 2 ya kodi wanayolipa waajiri nchini, lakini wamepuuzwa, madeni yao ya posho na madai ya nyuma hawalipwi, nyongeza ya mishahara hakuna, huku gharama za maisha zikipanda zaidi kwao.

3. 1.5 Trilioni Zilizopotea Zinaweza Kulipa Nyongeza ya 10% ya Mishahara kwa miaka miwili:

- Ripoti ya Mdhbiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 inaonyesha kupotea kwa shilingi 1.5 trilioni zisizojulikana matumizi yake. Serikali imetoa maelezo bungeni juu ya fedha hizo, maelezo ambayo yamepingwa na kuonyeshwa kuwa ni uongo mtupu. Sasa ni dhahiri kuwa fedha hizi zimetafunwa kifisadi na Serikali ya CCM. Katika wakati ambao Serikali hii hii inadai haina fedha za kupandisha mishahara. Gharama ya Mishahara ya Serikali kwa mwezi (wage bill) ni shilingi 650 bilioni, shilingi 1.5 trilioni zilizopotezwa na Serikali zingetosha kupandisha mshahara wa wafanyakazi kwa 10% kwa miaka miwili mfululizo.

RAI ya ACT Wazalendo: Tunarudia rai yetu kwa vyama vya Wafanyakazi, khususan TUCTA, kushikamana kudai haki za wafanyakazi nchini, hasa nyongeza ya mishahara, haki waliyonyimwa kwa miaka mitatu sasa. Tunajua kuwa Haki haiombwi bali hupiganiwa. Sisi ACT Wazalendo tuko tayari kushirikiana nao kupigania haki za Wafanyakazi nchini.

B: Ushiriki wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kwenye 'Siasa' na Utetezi wa Haki Zao.

Akihutubia Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Rais aliweka bayana msimamo wa Serikali yake kuhusu ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu kwenye siasa, akieleza kuwa hatasita kuwafukuza wanafunzi wa chuo chochote watakaogoma kushinikiza upatikanaji wa haki zao (kama kupinga ubaguzi kwenye mikopo ya elimu ya juu nk).

Tunafahamu kwamba shabaha hasa ya kauli hii si kuzuia siasa vyuoni kama inavyosemwa, bali ni kuzika utamaduni wa wanafunzi kuikosoa serikali, kupinga sera na matendo kandamizi na ya ubaguzi wa kielimu, na kuzika vuguvugu la wasomi wa vyuo vikuu dhidi ya Serikali. Ni kauli yenye lengo la kuminya zaidi uhuru wa maoni ya wasomi nchini. Kauli hii inatishia ujenzi wa kizazi cha vijana wenye kuhoji na kujiamini na badala yake kujenga kizazi cha vijana wenye nidhamu ya woga na wasiohoji.

Ni muhimu kumkumbusha Rais na Serikali yake kwamba mbali na kuwa pahala pa kujifunzia taaluma mbalimbali, Chuo kikuu ni Tanuri la kuoka Viongozi wa baadaye, na kujenga kizazi kinachojiamini na chenye uelewa mpaka juu ya wajibu wao wa kiukombozi kwa nchi yetu na kwa Bara la Afrika.

Ni vizuri sisi vijana wa ACT Wazalendo tumkumbushe Rais juu ya mchango wa wa siasa na utetezi wa haki wa wanafunzi nchini kwa matukio yafuatayo ya historia ya Taifa letu:

1. Mwaka 1965, wakati Mwalimu Nyerere akipambana kupinga ukoloni wa Serikali ya Uingereza kule Zimbabwe, Joseph Sinde Warioba, na wanafunzi wenzake, chini ya mwamvuli wa NAUT (Chama cha Wanafunzi Tanganyika) hawakumuachia Baba wa Taifa na TANU wajibu huu peke yao, Walihamasishana na kuandamana hadi Ofisi za Ubalozi wa Uingereza nchini kupinga uhuru bandia uliotolewa chini ya Ian Smith. Tukio hili linaonyesha wajibu wa wanafunzi wa vyuo vikuu wa Tanzania kupinga unyonge popote pale Afrika.

2. Wanafunzi hawakuiunga tu mkono Serikali ya Mwalimu Nyerere, waliipinga pia. Mwaka 1966, mgomo wao mkubwa ulioongozwa na Samuel John Sitta uliifanya Serikali ipunguze mishahara ya Rais na baraza lake la Mawaziri. Baadhi ya wanazuoni wa masuala ya kisiasa nchini, akiwemo Profesa Issa G. Shivji, wanaamini kwamba moja ya masuala yaliyosukuma kutokea kwa Azimio la Arusha ni Mgomo huu wa Wanafunzi. Tukio hili linaonyesha wajibu wa wasomi kuibana Serikali hata kwa mambo yasiyohusu haki zao binafsi, bali manufaa mapana ya umma.

3. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiliitwa “Makkah ya Afrika" kutokana na kuvutia wasomi mashuhuri kuja kufundisha, pamoja na uhuru wa kitaaluma wa walimu na Wanafunzi wake. Rais wa Leo wa Uganda, ndugu Yoweri Kaguta Museveni, Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, ndugu Willy Mutunga, Balozi Liundi, Mama Zakia Meghi, aliyekuwa Kiongozi wa Sudan Kusini, Komredi John Garang kwa kushirikiana na walimu wao kina Haroub Othman na Walter Rodney waliongoza mijadala juu ya itikadi ya ujamaa, na hata mapambano dhidi ya Utekelezaji mbaya wa ujamaa, wakiyafanya hayo chini ya Chama chao cha TYL (TANU Youth League), USARF na jarida lao la Cheche. Tukio hili linaonyesha ushiriki wa wanafunzi wa chuo kikuu kwenye siasa, wakitumia maarifa yao kukosoa, kupinga na kushauri njia nzuri za utekelezaji wa Sera za Serikali.

4. Chuo Kikuu ni Tanuri la kuoka Viongozi, likitoa uzoefu na mafunzo kwa vijana wa kuongoza vijana wenzao. Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia, Kiongozi wa ACT Wazalendo, ndugu Zitto, na wengineo wengi ni zao la harakati za uongozi na utetezi wa haki kwenye vyuo vikuu. Rais hataki vijana wa sasa tupate uzoefu wa uongozi na utetezi wa kudai haki?

RAI ya ACT Wazalendo: Vijana wasipewe vitisho vyuoni, wasifundishwe nidhamu ya woga, huo si msingi wa Elimu ya Juu nchini. Tunawataka wanafunzi wa vyuo vikuu kuendelea kushikamana kudai haki zao na za jamii kwa ujumla, kuikosoa Serikali (kufanya siasa) na kushauri pale inapobidi.

C: Ubaguzi Kwenye Mikopo ya Elimu ya Juu (Hili litazungumzwa na Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo)

Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi
ACT Wazalendo
Mei 13, 2018
Dar es salaam
 
Naunga mkono hoja, mh abadilike yeye ni kiongozi mkubwa kauli nyingi zina umiza na kubomoa umoja wa kitaifa,

Kwa kuwa mh ni raisi msikivu na rais wa wanyonge naamini atasikia maombi haya
 
Wanafunzi wa elimu ya juu leo hii sijui wana nini woga umewajaa, wafanyakazi ndio kabisa hao viongozi wa vyama vya wafanyakazi kama wamepigwa ganzi, risala yao mei mosi ilitaji maslshi yao ikiwa nyongeza ya mshahara, ajabu boss wao mkuu mh rais akakataa ombi hilo tena bila haya,


Ajabu sijaona kiongozi yoyote wa vyama vya wafanyakazi TUGHE, CWT, TUCTA nk akitoa msimamo wao kama wafanyakazi, wala hakuna mwandishi wa habari aliyesubutu kuhoji mambo haya

Yani wafanyakazi wamerudishwa enzi za utumwa nakusahau nini maana ya mei mosi na kwanini sherehe hizo zipo, wanasahau watu walipoteza maisha nk ili kutetea haki zao na ndio maana mei mosi ipo
 
Kwani unaogopa nini kusema ni wewe ndio umeandika na ndio umesema? kwanini una singizia ni Ado wakati kilicho andikwa kiko wazi kabisa kimesemwa na kuandikwa na Zitto?

Zitto subiri kichanga chako kikue ukielimishe kikagome hata kikifukuzwa ukipeleke ulaya...Usiwasawishi watoto wa wenzie wapigane na wasio wawezi mwisho wa siku wana baki peke yao.....Leo hii Nondo amebaki peke yake ulijifanya ooooh naongozana nae oooh nitakwenda nae...yuko wapi sasa? Mzazi na ndugu zake ndio wana hangaika na yeye chuo kasimamishwa.....

Zaeni wakwenu muwatume wakagome sio kutumia watoto wa wenzenu kutafuta umaarufu na msiwafundishe jinsi ya kudai haki ...hao ni watu wazima waacheni watumie njia wanazo ona zinafaa........

Zaeni wakwenu mkawafundishe kugoma
 
Kiukweli katka mambo muhm ktk Taifa hl ni kuwasaidia vjana kutambua mambo mhm ktk maendeleo ya taifa le2 bado hata wanavyuo wengi ni waoga Sana bado vjana kna jambo kwao lnahtajka
 
Sio tu kwamba kauli zake sio za ki-urais, yeye mwenyewe hajakaa ki-urais
(Siyo presidential material)

Sijui ilikuwaje yani???
 
"Kwanza, ni lazima tukiri kwamba tunashukuru sasa Rais na Serikali yake wamekiri kinachomfanya washindwe kutoa ajira mpya nyingi zaidi, kuongeza mishahara, pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya wafanyakazi nchini ni uhaba wa fedha (Kama ambavyo ACT tumekuwa tukisisitiza) "

Haya maneno yako yameondoa hata hoja yako ya kuwambia wafanyakazi wadai maslahi zaidi.

Umesema serikali haina pesa halafu unawaambia tena wadai maslahi zaidi. You can't have your cake and eat it!

Suala 1.5T lilishabuma baada ya waelewa kugundua ulitaka kuwalisha "tango pori" ndio maana wameachana na hoja hiyo baada ya ukweli kuwafikia. Kumbuka uwongo hupanda lift wakati ukweli hutumia ngazi!

Hakuna mtu aliyekataza siasa vyuoni. Wafanyasiasa vyuoni lazima waelewe athari zitokanazo na wao kujiingiza kwenye siasa vyuoni. Kusomea siasa ni tofauti na kufanya siasa. Mtu anaweza kusoma siasa na asiwe mwanasiasa.

Inafurahisha kuwa kwa sasa Zitto ni Mweza hazina wa ACT, Katibu Mwenezi, Kiongozi Mkuu, Mkuu wa kitengo cha Mambo ya nje ACT na Mbunge! The man is all over the place!

ACT is becoming one man political party as time went by!
 
Wanafunzi wa elimu ya juu leo hii sijui wana nini woga umewajaa, wafanyakazi ndio kabisa hao viongozi wa vyama vya wafanyakazi kama wamepigwa ganzi, risala yao mei mosi ilitaji maslshi yao ikiwa nyongeza ya mshahara, ajabu boss wao mkuu mh rais akakataa ombi hilo tena bila haya,


Ajabu sijaona kiongozi yoyote wa vyama vya wafanyakazi TUGHE, CWT, TUCTA nk akitoa msimamo wao kama wafanyakazi, wala hakuna mwandishi wa habari aliyesubutu kuhoji mambo haya

Yani wafanyakazi wamerudishwa enzi za utumwa nakusahau nini maana ya mei mosi na kwanini sherehe hizo zipo, wanasahau watu walipoteza maisha nk ili kutetea haki zao na ndio maana mei mosi ipo
Wote wametiwa mfukoni!

Ova
 
Naona unazidi kujianika hapa Kwa ujinga wenu.
Elimu mtaisikia ahera
Wewe elimu yako imekusaidia nini?ungekuwa na elimu ungelilia kubembelezwa?hao wenye elimu kama mnalialia nini sasa,ziongozeni elimu zenu hapa mtaongozwa tu
 
Back
Top Bottom