PreGE2025 Ado Shaibu: Hakuna mwenye haki miliki ya kugombea ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amesema watasimamia Demokrasia kwa vitendo katika mchakato mzima wa kuwapata wawakilishi wa nafasi mbalimbali watakaoenda kushindana na wanachama wa vyama vingine katika Uchaguzi mkuu ujao wa Rais Waubnge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu

Ndugu Ado ametoa kauli hiyo kwenye tukio la Songwe Day lililowakutanisha watiania wa nafasi za Ubunge na Udiwani kutoka Majimbo yote ya Mkoa wa Songwe ambapo jumla watia nia wanane wa ubunge walijitokeza na kuchukua fomu katika mkoa huo kwa ajili ya kuomba ridhaa ya Chama.

Hadi sasa katika Mkoa wa Songwe waliochukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama ni Peter Kayuni (Vwawa), Michael Nyilawila (Songwe), Himid Siwale (Momba) na Ezekia Zambi, Nestory, Viniwa Arusha, Emanuel Kalinga (Mbozi).

Ndugu Ado amesema kwa mujibu wa taratibu za Chama cha ACT Wazalendo wanachama wote wana haki sawa katika kugombea nafasi yoyote kwenye Uchaguzi Mkuu 2025.

"Sisi tunaamini kuwa kama unahubiri Demokrasia unapaswa kuionesha ndani ya Chama kabla ya kwenda kuipigania nje. Kwenye Chama chetu, kwa nafasi zote za Urais, Ubunge, Ubunge Viti Maalum, Udiwani na Udiwani Viti Maalum kila mwanachama mwenye sifa ana haki ya kugombea" amesema Ndugu Ado.

Alitumia mkutano huo wa Songwe Day kutoa Onyo kwa Katibu yeyote wa Kata au Jimbo atayeweka vikwazo kwa mgombea yeyote kuchukua fomu akisisitiza kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Katika hatua nyingine Ndugu Ado amesema ACT Wazalendo inaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2025, sambamba na kupigania mageuzi ya msingi katika mfumo wa uchaguzi na kuyataja maeneo sita wanayopigania kuwa, kuhakikisha Wakurugenzi wa Halmashauri wasisimamie uchaguzi, Wajumbe wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi wateuliwe kwa utaratibu uliowekwa kwenye sheria ya Tume Huru, kusiwe na kura feki, wagombea wasienguliwe hovyo, vyombo vya ulinzi na usalama visishiriki hujuma kwenye uchaguzi na mawakala wa vyama wasibugudhiwe vituoni.

Leo Mei 16 2025, Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Mbeya ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye tukio la Mbeya Day litakalowakutanisha watiania wa Ubunge na Udiwani kutoka majimbo yote ya Mkoa wa Mbeya.
 
Attachments

CCM wanawazoom tu ..................
Tieni Nia weeeeee, wenzenu wanawandalia bao la Mkono
Ndio mtajua hamjui
 
Back
Top Bottom