Mwamba 777
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 2,683
- 4,304
Wana nini? Kama bunduki hata sisi tunazo Tena Kwa kibali maalum, wakimwaga mboga namwaga ugali, nitahakikisha nakufa na wawili au watatu kama hamza na hawatokaa wanisahau Kwa ushenzi ntakao wafanyiaKaka usimalize maneno... Wako watu watata na wanajua mchezo ya hatari.. Ila ukiyaingia kwa wanajeshi Kua mpole
Nawe utakuwa mwanajeshu,acheni kutishia wananchiUnasema tu
Watu kamaa nyie ndio popo kishenzi.
Utapigwa mpaka usemee mimi ni mwanamke natafuta mme
Hawa Jamaa usiombe uingie kwenye 18 zao, utajuta kuwafahamu.
Siku moja Tulikuwa kwenye foleni ya kuelekea mjini, kuna jamaa wa Lori akaziba geti la kuingilia pale kambi ya Abdallah Twalipo uhasibu. MP akamfuata kistaarabu kabisa "mambo vipi Kaka?" Jamaa akaitikia "Safi kabisa afande". Afande akamuuliza hapa uliposimama si unajua Kama ni getini? Mwamba kwa kujiamini kabisa akaitikia ndiyo afande ila tatizo foleni haitembei, Sina jinsi, samahani sana.
Kama kawaida ya wanajeshi kujifanya wastaarabu kwenye matukio ya aina hii. Afande akamwambia sasa ndugu kwa kuwa foleni haiendi shuka tu hapa upumzike tupige stori, foleni ikitembea utaendelea na safari yako. Dereva wa Lori kwa mbwembwe akafungua mlango ashuke eti apumzike na wanajeshi. Hapo ndiyo 'ntiti' ulipoanza!!
MP akamwambia "kaka sijasema ushuke mlangoni, shukia dirishani" lilikuwa ni tukio la kuchekesha Sana kwa sisi wapita njia ila kwa lililomtokea lilikuwa ni tukio mbaya na la kufedhehesha.
Picha linaanza,gari anayoendesha jamaa ni Scania R 420,Chuma mpya kabisa ya Transit alafu imepanda hewani Kama farasi, imebeba mafuta inaelekea nje. Gari ikisimama dereva unamwona yule kuleee ghorofani. Sasa vuta picha dereva ameambiwa ashuke kupitia dirisha badala ya mlangoni. Sisi wengine wa pembeni Tulicheka Sana maana jamaa kwanza ni bonge alafu ili ashuke kwa kutumia dirisha inabidi ajikusanye awe Kama fungu la nyanya Kisha ndiyo atoe miguu nje. Ilimchukua karibia dakika 15 kushuka. Wakati huo MP alikuwa siriazi hacheki wala haongei. Yeye anamsubiri jamaa tu ashuke wapige stori. Dereva akadondoka chini Kama mzigo wa viazi mbatata vya Mbeya..Tiii!!
Suruali yote imechanika kwenye maungio ya miguu. Aliposhuka huku kijasho kinamtoka mjeda akaanza kupiga nae stori Kama hakuna kilichotokea "naona chuma imeshakunywa wese inasepa?" Dereva kinyonge akajibu yeah inaelekea Ndola, Zambia. Wakapiga stori Mara foleni ikafunguka magari yakaanza kutembea. Afande akamwambia dereva Sasa unaweza kwenda tu maana gari zinatembea. Dereva akatoa shukrani Kisha akaelekea kwenye gari yake asepe.
Cha ajabu wakati dereva anafungua mlango Mjeda akamwambia mzee baba si tulikubaliana tunapitia dirishani? Ahahahhaha kazi ya kupanda dirishani ikaanza tena. Nina uhakika Yule dereva alimtukana mjeda matusi yote ya hapa duniani ila kimoyomoyo.. Ile siku yule dereva hataisahau kamwe maishani.
Unakumbuka kisa chochote Cha wanajeshi na adhabu zao kwa raia pindi raia akijichanganya kwenye anga zao?
Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.
Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Mimi Nina damu ya kiarabu, Nasemeje Kuna haja ya wabongo kuzaa na waarabu na wasomali tupate wapambanaji walio tayari kujitoa muhanga kwaajili ya kutetea haki, wabongo mnaasili ya kauoga, Mimi sipo hivo, Mimi Nina dam ya kiarabu nipo Razi kuvaa bomu nikafe na washenzi buku kuokoa taifaWatu Kama wewe ndiyo mnakuwaga wapole Kama mmemwagiwa maji mkiwaona bakabaka. Ila kwa background mnaandika kishujaa Kama hivi.
Keyboard warrior.
Sahihi.Afande akileta upuuzi huo unamgomea tu, maana ni kinyume cha maadili ya kazi za jeshi. Hawezi kukufanya lolote. Hawezi kukuua na kama Akikudhuru unamfikisha kwa wakubwa wake tu , uone kama kibarua chake hakijaota nyasi.
Tatizo watu hawajui haki zao na wanaogopa magwanda. Lakini nidhamu za kijeshi zinakataza kabisa askari kuonea raia.
Kijana utajaa tu siku moja ndio utajua wajenda ni vichaa zaidi yako. Utanyooshwa na jamaa ukimshtaki afukuzwi kaziMimi sikubaligi upumbavu, huyo mwanajeshi mshamba na njaa Kali angekuja kwangu aone, ningevomjibu dry sitishiwi bunduki Mimi, Wala sitishiwi kifo hata siku moja
Angeenda ailete hata Kambi nzima, siogopagi kufa Mimi, liwalo na liwe na ndo wangejua kweli hii Dunia kuna watu watata, sio Dunia, Tanzania kuna watu watata. Mimi ndio MWAMBA.
Utaumia tu nduguSahihi.
Muache mjuaji huyo akojaa18 atakubali mziki.Tena wewe ndiyo utakuja kuumizwa kabisa ukileta ujinga huo. Kule kuna watu wameshindikana na zaidibya wahuni, ukitaka ukae nao wale kwa amani punguza ujuaji
Nasemaje!, usije kutana na hao watu ukaleta ujuaji, utaumia mzee baba!. Nasema utaumia sababu hakuna atakayeajibishwa kwa wajeshi wa nchi hii. Bro wangu mmoja hivi alikutana na kisanga pale makongo kipindi anasoma pale Tumaini bachelor of laws, alileta ujuaji wa sheria lkn kilichokuja kumpata hatasahau maisha yake yote.Unachokifanya ni kushangilia ujinga wa kutokujua haki zako, Askari wa jeshi lolote haruhusiwi kukushambulia hata kama umevunja sheria ilimradi tu hujakataa kutii amri ikiwa amekuja kukukamata haruhusiwi kukupiga Wala kukudhalilisha kwa adhabu yoyote chombo kinachotoa adhabu ni mahakama anachotakiwa kukifanya ni kukufikisha mbele ya vyombo vya sheria ili ukahukumiwe kwa kosa ulilofanya kama kweli hilo kosa lipo
Akikwambia chuchumaa/kaa chini we kubali ila akikwambia ruka kichura mwambie siwezi kwasababu za kiafya hapo sasa chochote atakacho kufanya ikiwa ni kukushambulia unaruhusiwa kumshitaki utaratibu wa kushtaki ni uleule
Shambulizi lolote atakalo kufanyia ni kosa kama makosa mengine ya shambulio na unaruhusiwa kufungua kesi dhidi yake na akawajibishwa
Huyo dereva alitakiwa akatae kwanzia amri ya kuambiwa ashukie dirishani kwakua siyo amri halali na ni kinyume na utaratibu kwakua ilikua inahatarisha usalama wake
Acha uoga ww jambo lakwanza ww kamata ile number yake kwisha habari yake akikuamrisha chochote kilicho na element ya udhalilishaji usifanye.Nasemaje!, usije kutana na hao watu ukaleta ujuaji, utaumia mzee baba!. Nasema utaumia sababu hakuna atakayeajibishwa kwa wajeshi wa nchi hii. Bro wangu mmoja hivi alikutana na kisanga pale makongo kipindi anasoma pale Tumaini bachelor of laws, alileta ujuaji wa sheria lkn kilichokuja kumpata hatasahau maisha yake yote.
Wale wana wanatumia neno AMRI, zingatia sana hilo neno usije jichanganya aisee...
Dogo acha ujinga we na huyo bro wako wazazi walipoteza ada wakapeleka ng'ombe shuleni unatoa mfano wa bro wakati mimi binafsi nimeshawaonya hao wanajeshi kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na maadili ya jeshi na kuvunja sheria? Hivi unajua kosa lolote la jinai ikiwepo kumshambulia mtu ni kosa la kufukuzwa kazi kwenye majeshi ya ulinzi?Nasemaje!, usije kutana na hao watu ukaleta ujuaji, utaumia mzee baba!. Nasema utaumia sababu hakuna atakayeajibishwa kwa wajeshi wa nchi hii. Bro wangu mmoja hivi alikutana na kisanga pale makongo kipindi anasoma pale Tumaini bachelor of laws, alileta ujuaji wa sheria lkn kilichokuja kumpata hatasahau maisha yake yote.
Wale wana wanatumia neno AMRI, zingatia sana hilo neno usije jichanganya aisee...
Rejea hiyo story yangu kisha mengine jiongeze. Huyo bro wangu alifanya kila ujanja, kilichomtokea hakisimuliki ww.Acha uoga ww jambo lakwanza ww kamata ile number yake kwisha habari yake akikuamrisha chochote kilicho na element ya udhalilishaji usifanye.
Ukiwa ndezi,ndo utazidi kuumia zaidiTena wewe ndiyo utakuja kuumizwa kabisa ukileta ujinga huo. Kule kuna watu wameshindikana na zaidibya wahuni, ukitaka ukae nao wale kwa amani punguza ujuaji
Rest in peace classmate
Sina cha kukujibu kaka mkubwa maana naona tutadhalilishana tuDogo acha ujinga we na huyo bro wako wazazi walipoteza ada wakapeleka ng'ombe shuleni unatoa mfano wa bro wakati mimi binafsi nimeshawaonya hao wanajeshi kufanya vitendo ambavyo viko kinyume na maadili ya jeshi na kuvunja sheria? Hivi unajua kosa lolote la jinai ikiwepo kumshambulia mtu ni kosa la kufukuzwa kazi kwenye majeshi ya ulinzi?
Sasa kawatishe wajinga wenzako mtaani usituletee utoto hapa
Kwenye pitapita zangu nikaingia kwenye eneo la Jeshi kukata majani ya kulisha ng'ombe. Mbele yangu kulikuwa na maembe dodo yanatamanisha sana. Sasa mimi sikujua kama ni eneo la jeshi.
Nikaenda chini ya embe dodo nikaanza kuyapopoa maembe.
Muda kidogo naona pale nilipoacha mkokoteni wa kubebea majani kuna mtu amekaa na magwanda, huku anazuga anaongea na simu.
Oya, siisahau ile siku.
Hakuna mtu ambaye Yuko juu ya Sheria. Panda mbele mahakamani kafungue kesi,Rejea hiyo story yangu kisha mengine jiongeze. Huyo bro wangu alifanya kila ujanja, kilichomtokea hakisimuliki ww.
Jamaa baada ya kwenda kwa viongozi kaongezewa adhabu nyingine.
Haya mambo tuyaache tu
Alitakiwa apande juu zaidi baada ya aliekwenda kumshatakia kutomsikiliza lao lilikuwa mojaRejea hiyo story yangu kisha mengine jiongeze. Huyo bro wangu alifanya kila ujanja, kilichomtokea hakisimuliki ww.
Jamaa baada ya kwenda kwa viongozi kaongezewa adhabu nyingine.
Haya mambo tuyaache tu
Jaribu uende kuleta ujuaji wako, utasimulia hadi wajukuu kitakachokupata. Wanajeshi epuka sana akiwa yupo eneo la kazi na hapo ulimkuta alipangiwa jukumu fulani, kazi ikiharibika anaadhibiwa na kuliko litokee hilo ndiyo anakuzingua. Kama huyo wa lori aliyekutana na MP, wale kituo chao cha kazi ni hapo getini kama angekutwa na wakubwa geti limezibwa hivyo angezinguliwa na ndiyo hapo aliamua kumzingua yeye.Ukiwa ndezi,ndo utazidi kuumia zaidi