Adhabu za wanajeshi

Huyo dogo namjua. Nafikiri utakuwa unamwongelea Bellah.
 
Ila huo ni unyanyasaji na mwanajeshi mwenye akili timamu hawezi kumnyanyasa binadamu mwenzie kwa kosa kama hilo lisilo na miguu Wala kichwa.

Kimsingi mtu wa namna hiyo namuonaga kama hamnazo vile
 
Safi sana kwa elimu mujaaarabu!
Unajua baadhi ya wanajeshi ni wajinga sana. Mwanajeshi mwenye weledi hawezi kufanya mambo kama hayo. Ndo shida ya kuajiri watu waliopata waliopata four ya zero.
 
Wanajeshi wasio na kisomo hawana hakili kabisaaaaaa,Inaelekea watu wanajua mwanajeshi hua hapigwi,
Aloo Kuna wanajeshi wawili walipigwa vibaya sana na washkaji waliokua wakichunga Mbuzi maeneo ya jeshi.
 
Kuna football team ya kambi flani hv ya jeshi, sjui ni ujinga au upumbavuu😲
Wakicheza na team ya kijjn ambapo wanamashart Yao.

1, huruhusiwi kushangilia Kwa kiruka circus au kupiga kelele na kuzomea hovyo ukifanya Hvo utajuta kwann ulifunga goli.

2, Kupiga chenga za sifa na kujiona we ni star kama inonga misifaa kibao hii itakula kwako kwani utajuta kwann unaleta sifa
3, haitakiwi kuifunga hii team kabisa iwe isiwe Bora mtoke draw, na ikitokea mmefunga mtafanya juuchini japo mjifunge tu Ili kuepusha vita ya tatu ya dunia. Sio Kwa hicho kipigo kitakachowakuta.

Hawa jamaa yaani sio poa ila hii ilkua zaman saiv Kwa namna tulivovurugwa aahh kinaumana.
 
 
Ukitaka kuongelea kuhusu sheria basi kajadili huko kwingine na si kuingia eneo la kazi la mwanajeshi. Ukiona mwanajeshi yupo eneo lake la kazi kaa naye mbali sana, kukitokea msala wowote ule kisa raia wewe kwa ujuaji wako anapewa adhabu mbaya kuliko hizo anazokupa. Hao watu tumeishi nao makambini na kama hana zamu ya majukumu utamwona ni mshkaji wako, akiwa na zamu hata urafiki tulikuwa hatuleti. Kuna mmoja alishawahi kuwapiga kuruti ambao ni washkaji zake sana mateke ya uso kabisa kisa kumletea ujinga akiwa zamu.

Kama huyo dereva wa lori hapo, kaziba geti na eneo lake la kazi ni hapo getini ulitaka afanywaje? Wakubwa wakitoka je na wana mambo yao, unafikiri kitakachomkuta kinafikia cha huyo dereva alichomfanyia?

SHERIA PELEKA KWENU USICHEZE NA MTU AKIWA KAZINI NA ANATAKIWA KUIFANYIA KAZI HIYO KWA UFANISI. UTAUMIA
 
Acha kuwafundisha watu uoga na kukubaliki kunyanyasika wakiwa wananyang'anywa haki zao za msingi. Ukianza huo unyonge utapigwa makofi hata na wadogo zako
Kama unajua haki zako za msingi basi tambua na haki zake huyo mwanajeshi pia. Usimletee ujinga na wala usikiuke taratibu zao akiwa yupo eneo lake la kazi. Ujuaji wenu utaumia na cha kufanya huna, kama huyo dereva wa lori aliyeziba geti angemfanya huyo MP apewe adhabu mbaya sana na wakubwa zake. Ulitaka amuache?

Usicheze kwenye kazi ya mtu ambaye aliisotea na hata kuumia hadi kuja kuipata
 
Ila kweli jeshini hakuna kujuanaa, nilishuhudia kabisaa,
 
Ila kweli jeshini hakuna kujuanaa, nilishuhudia kabisaa,
Watu hawajui hilo, kama kule ndani linapokuja suala la kazi hawana mambo ya kujuana. Vipi huko raia uje kumletea ujuaji, yaani wale anaweza kukufanya kiti kibaya hata kama mshkaji wako
 
Watu wanaotakiwa kulinda raia ndio ambao wanaonea raia kwa kuwahukumu badala ya kuwapeleka sehem husika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…