Adhabu za shule kama hizi, zimepitwa na wakati

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
Kama Wewe Ndio Mzazi Unakwenda Shuleni Unamkuta Mwanao Anapewa Adhabu Kama Hii..Utachukua Hatua Gani Ya Haraka....!!

Adhabu za shule.jpg
 
Ndio maana bara la Afrika bado tuko nyuma kila uchwao!! Wenzetu wanalinda haki za watoto na kujitahidi kuwapa Mazingira rafiki zaidi ya kujifunzia sisi bado tumeng'ang'ana na mifumo ya kikoloni ya uendeshaji wa taasisi zetu za elimu! Jambo la kusikitisha ni kwamba hili (picha juu) ni jambo la kawaida kabisa katika shule zetu kayumba.. Alafu bado kuna kundi kubwa tu la walimu wanahisi ni haki yao kabisa kufanya hivi..
 
Katika kipindi nilichofanya kazi ya Ualimu kabla ya kutoa adhabu nililazimika kuwaita wazazi shuleni.Makosa mengi ya Wanafunzi mashuleni chanzo ni Wazazi wao.Ukitathmini mtazamo wa mzazi basi kuna wanafunzi utagundua hawahitaji adhabu bali ni maombi.
 
Ndomaana baada ya kuhitimu shule tulipoenda JKT tuliishikwa raha mustarehe, tena ilikuwa mwaka mzima na bado tuliona ni muda mfupi mno. haya sasa hawa washuleshule wa kileo, kizazi cha tom and jeri, wakapewa miezi sita wakaona karne, nasikia sasa wamepewa miezi mitatu lakini bado tu hoi.
 
Back
Top Bottom