Nadeclare interest kabla ya kutoa maudhui ya somo hapo juu kuwa binafsi ni mdau wa Elimu na ni mwezeshaji. Adhabu hii ya viboko licha ya kuwekewa sheria na taratibu bado walimu wa shule hasa za msingi hawazifuati sheria hizo wala taratibu zake. Utakuta mwalimu anamchapa mtoto wa chini ya miaka 13 fimbo zaidi ya 12 tofauti ya kiwango kilichokubaliwa kisheria cha fimbo pungufu ya 4.Nalisema hili kwa ushahidi na situngi.
Nilibahatika kuwa shule ya msingi Kinondoni Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam ambapo nilishuhudia wanafunzi wa darasa la sita na la saba wakicharazwa tena na mwalimu mmoja wa kiume kijana hivi zaidi fimbo nane kwa kosa la kushindwa kupata jibu sahihi la hisabati.
Nimeshuhudia wanafunzi wale wakikandwa viganja vya mikono yao na barafu kwani vilivimba sana. Maskini watoto hawa huogopa kuzungumza mambo ya shuleni kwa wazazi wao kwa sababu ya kutokujaliwa na wazazi wao au kupuuswa. Mamlaka zinazohusika waokoeni watoto hawa kabla hawajapata majanga kama yaliyotokea mkoani Tanga. Wapelelezeni watoto wa shule tajwa msikie madhila wanayoyapata na wengine wanawaza kuacha masomo kuepuka adhabu za viboko vitolewavyo shuleni hapo bila utaratibu.
Chukueni hatua ili kuirekebisha hali hiyo.