Adhabu ya uhaini Tanzania siyo lazima kifo

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
97
Reaction score
1,751
ADHABU YA UHAINI TANZANIA SIO LAZIMA KIFO.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255714047241.

Mahakama kuu na ya Rufaa zinasema kuwa popote katika sheria ambapo limetumika neno "SHALL BE LIABLE ON CONVICTION TO SUFFER DEATH", maana yake ni kuwa sio lazima mtuhumiwa ahukumiwe kifo bali anaweza kuhukumiwa hata kifungo chochote cha miaka kadhaa au maisha.

Neno hili ndilo lililotumika katika kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni za Adhabu RE 2022 kinachoeleza na kutoa adhabu ya uhaini Tanzania.

Tafsiri hii imesemwa katika Rufaa ya Jinai Na.28/2020 ANTHONY EMMANUEL vs Republic.

Pia, Mahakama ya Afrika Mashariki katika kesi ya OPOYA vs UGANDA(1967)EA 752 inasema hivyohivyo ikinukuliwa hapa" The words SHALL BE LIABLE ON CONVICTION TO SUFFER DEATH, provide maximum sentence only, and the courts have discretion to impose sentence of death or imprisonment"

Maneno hayohayo yamerudiwa na Mahakama ya Rufaa iliyokaa Mwanza katika Rufaa ya Jinai Na.114/2019 BAHATI JOHN vs Republic.

Aidha, maneno "SHALL BE LIABLE ON CONVICTION TO SUFFER DEATH(akipatikana na hatia atatakiwa kupata adhabu ya kifo)" katika Uhaini yanatofautishwa na yale ya kwenye makosa ya mauaji ambayo husema "ANY PERSON CONVICTED OF MURDER SHALL BE SENTENCED TO DEATH( mtu yeyote atayepatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia atahukumiwa kifo) kifungu cha 197 Kanuni za Adhabu.

Maneno ".....SHALL BE SENTENCED TO DEATH(atahukumiwa kifo)" kwa mtu aliyeua mahakama inayatafsiri kuwa maana yake hukumu ya kifo ni lazima na sio chaguo(mandatory not discretion) ikiwa muuaji atapatikana na hatia.

Kwahiyo maneno ya kwenye Uhaini adhabu ya kifo sio lazima wakati yale ya kwenye mauaji adhabu ya kifo ni lazima.

Kwa maana hiyo kwenye uhaini ukipatikana na hatia adhabu yaweza kuwa kifo, kifungo cha maisha, au kifungo miaka kadhaa jela.

Je ni kitu gani ama sababu ipi kwenye uhaini huifanya mahakama isitoe adhabu ya kifo na badala yake itoe adhabu ya Kifungo.

Moja ya sababu(on mitigation) ni ikiwa mtuhumiwa ndio kwa mara ya kwanza anapatikana na hatia ya jinai ambapo inachukuliwa kwamba ni mkosaji kwa mara ya kwanza(first time offender) na hivyo anastahili huruma na muda wa kujifunza.

Mtu anaweza kuwa ameshitakiwa mara nyingi zaidi lakini hajawahi kupatikana na hatia, huyu bado anahesabika ni mkosaji kwa mara ya kwanza ikiwa ndio sasa anapatikana hatia. Na kama ni kosa la Uhaini anatakiwa kufaidika na adhabu ndogo ya kosa hilo(less penalty) ambayo ni kifungo badala ya adhabu kubwa ya kosa hilo(maximum penalty) ambayo ni kunyongwa hadi kufa.

NI MATENDO GANI YANAHESABIKA NI UHAINI TANZANIA.

Kifungu cha 39 Kanuni za Adhabu, RE 2022.
1. Kumuua au kujaribu kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2. Kumuumiza,kumteka, ama kumfunga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

3. Kumuondoa au kujaribu kumuondoa Rais wa Jamhuri ya Muungano katika wadhifa wa urais katika namna isiyo ya kisheria.

4. Kuiangusha au kujaribu kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

5. Kulitishia Bunge, Serikali au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano.

6. Kuwasaidia maadui wa Jamhuri ya Muungano kuivamia Jamhuri ya Muungano kwa majeshi.

7. Kutumia silaha kuitishia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

JE WAJUA UHAINI NI SUALA LA MUUNGANO.

Hapo juu unaona kila kosa linairejea au linakuwa dhidi ya "JAMHURI YA MUUNGANO ....". ,

Maana yake ni kuwa hayo juu yakifanyika dhidi ya Rais wa Zanzibar au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar@SMZ haiwezi kuwa Uhaini. Hakuna kosa la Uhaini dhidi ya Rais wa Zanzibar au dola yake.

Hii pia ni kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama ya Rufaa iliyokaa Zanzibar katika Maombi Na.8/2020 kati ya SMZ dhidi ya MACHANO KHAMIS ALI na wengine 18( Maarufu kama kesi ya uhaini Zanzibar ya Maalim Seif na Juma Duni Haji) ambapo mahakama ilisema haiwezekani kuwepo Uhaini dhidi ya Zanzibar au Tanganyika kwasababu hakuna dola ya Zanzibar wala Tanganyika bali ipo dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo inayoweza kutendewa uhaini.

Na ikasisitiza kuwa kwakuwa Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano na Uhaini ni kosa dhidi ya Ulinzi na Usalama basi pia Uhaini ni suala la Muungano.

KESI NYINGINE YA UHAINI TANZANIA.

Ukiacha hiyo Na 8/2020 ya wakina Maalim Seif na Duni Haji ipo pia kesi ya Jinai Na.32/1971 kati ya GRAY LIKUNGU MATTAKA na wengine VS JAMHURI.

Washitakiwa .
Oscar Kambona(Waziri wa Serikali za Mitaa mstaafu na msiri wa Mwalim Nyerere), Bibi Titi Mohammed(mwenyekiti mstaafu wa umoja wa wanawake Tanzania), Michael Marshall Kamaliza(Waziri wa Kazi Mstaafu), William Makori Chacha(askari jeshi mstaafu), Grey Likungu Mattaka(mhariri mstaafu wa gazeti la serikali), Eliya Dunstan Chipaka(captain wa jeshi mstaafu), Alfred Phillip Millinga(askari jeshi).

Kesi Yao.
Ilikuwa ni kupanga, kuratibu mipango ya kuiondoa madarakani isivyo halali serikali ya Mwalim Julius Nyerere.

Mawakili wa Serikali.
Mark Bomani
Nathaniel King(raia wa Trinidad).

Majaji.
Philip Telfer Georges(raia wa Trinidad).

Hukumu.
Walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha Maisha jela isipokuwa Oscar Kambona ambaye hakuwa ndani ya nchi.

WATU AMBAO HAWAWEZI KUHUKUMIWA KUNYONGWA KWA UHAINI TANZANIA.

Kifungu cha 26 Kanuni za Adhabu.

Iwe ni hatia ya Uhaini au Mauaji ya kawaida, mtu ambaye hajafikisha miaka 18 wakati akitenda kosa na mama mjamzito hawawezi kuhukumiwa kunyongwa hata wakipatikana na hatia.

Adhabu yao itabadilishwa na kuwa kifungo.

DHAMANA YA UHAINI.
Kosa la uhaini halina dhamana.

Makosa mengine ambayo hayana dhamana Tanzania ni Kuua kwa kukusudia(mada), wizi wa kutumia silaha,Ulawiti, Usafirishaji dawa za kulevya kutegemea kiwango na thamani, Ugaidi, Utakatishaji fedha, na Usafirishaji haramu wa binadamu.


Pia soma:
~ Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025
~
Tundu Lissu ahojiwa kwa makosa ya uhaini na kutoa taarifa za uongo, agoma kutoa maelezo Polisi
~ Meseji ya Heche kwa wananchi kuwa "Wanataka Kumnyonga Lissu" Inasababisha wananchi wapay attention zaidi kwa ishu ya Lissu kufunguliwa kesi ya Uhaini
 
Uhaini na kutaka kuliondoa ccm on power kwa maandamano ya amani, wapi na wapi?
 
mbowe anasemaje kwani yupo kimya sana mwamba?
 
DPP atasema hana nia ya kuendelea na hii kesi.
 
Uhaini na kutaka kuliondoa ccm on power kwa maandamano ya amani, wapi na wapi?
Kitendo cha kudai uchaguzi ulio huru na wa haki, kwa namna ccm ilivyo jizoesha kinaonekana ni UHAINI kwakua ukifanyika uchaguzi huru na haki ni wazi serikali ya ccm itaondoka madarakani.

Kwahiyo, yeyote anayetaka uchaguzi huru na haki anaonekana ni mhaini anataka kuiondoa serikali madarakani kinyume cha sheria.

Kwa ccm haramu ndio halali na halali ndio haramu
 
Kabisa....
 

..lakini TL amependekeza mara kadhaa kwamba serikali hii iongezewe muda madarakani, uchaguzi usogezwe mbele, ili kutoa nafasi ya kufanya mabadiliko. Sasa mtu mwenye maoni kama hayo eti leo anashtakiwa kwa kutaka kupindua serikali, uhaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…