GE2025 Adeni Mwakyonde ajitosa tena Ubunge Tunduma, aichangamkia fomu kupambana na David Silinde

GE2025 Adeni Mwakyonde ajitosa tena Ubunge Tunduma, aichangamkia fomu kupambana na David Silinde

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Songwe Adeni Mwakyonde amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania ubunge katika Jimbo la Tunduma.

Mwakyonde amechukua fomu hiyo tayari kuchuana na Mbunge wa Jimbo hilo na Naibu Waziri wa Kilimo anayaliza muda wake David Silinde.

1751262960030.png
Katika mchakato wa kura za maoni kwenye uchaguzi wa ndani kumpata mgombea ubunge mwaka 2020 Adeni Mwankyonde alimshinda mbunge wa sasa David Silinde ambaye ndiye aliteuliwa na Chama hicho kupeperusha bendera ya nafasi ya ubunge.

Mwakyonde amekabidhiwa fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Tunduma Leo Juni 28,2025 na katibu wa Chama hicho wilaya ya Momba Katana Sukulu.

Akizungumza baada y kuchukua fomu hiyo Mwakyonde amesema ana nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Tunduma na kwamba kilichobaki kwa sasa ni kusubiri mchakato wa ndani ya chama juu ya uteuzi wa majina matatu.

Wanachama wengine waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge kwenye Jimbo la Momba ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba Mathew Chikoti, na kada wa chama hicho Ombeni Nanyaro ambapo Jimbo la Momba linaongozwa na Condesta Sichalwe
 
Back
Top Bottom