Adam TV tunaomba ufafanuzi

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
657
Wadau wa soka hasa ligi kuu Tanzania bara na michuano mingine ya kimataifa wanapenda kujua sababu hasa zinazofanya Azam tv washindwe kuweka alama ya neno LIVE.

Yapo maandishi kadhaa ambayo huonekana kuanzia mwanzo wa mechi hadi mwisho kama vile majina ya timu zinazopambana.

Hatuelewi huu ugumu wa kuandika hilo neno lenye herufi nne tu tena zinakaa pembeni unatoka wapi.

Je, hilo neno la live pengine lina sumu au kirusi ambapo likiandikwa tu TV yote ya Azam inaungua au inapata shoti mbaya.

Ni kawaida Kwa uongozi wa Azam kupuuza na kudharau malalamiko ya wateja wao ambao ni watoto wadogo lakini wakubwa kama mawaziri, wabunge,nk malalamiko yao hujibiwa mara moja.

Tunaomba majibu neno LIVE lina matatizo gani.
 
Nimefunguwa faster uzi huu kutaka kujua Adam TV ipo wapi, kumbe ni Azam TV. .
 
Kwani ikiwa neno live limakuongezea nini
Mkuu swali lako ni sawa na kwenda kumuuliza mkeo usipovaa sidiria kinapungua nini?

Anyway neno live tafsiri yake (iliyo hai),BAKITA wanasema mubashara, ni muhimu kwa mtazamaji kwani humfahamisha kwamba anachoangalia ni tukio halisi linaloendelea katika muda huo anaotazama ukilinganisha na tukio lililorekodiwa.
 
Wewe hujui faida ya kuvaa sidiria? Huoni umuhimu wa kuhifadhi kandambili za mkeo.
 
Back
Top Bottom