Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,833
- 979
CCM ipo sana kwenye hatamu za uongozi wa Tanzania.
Kila baada ya muda flani, CCM hujutafakari na kujiunda upya. Hii ni sifa muhimu sana kwa chama cha siasa. Mnayoyaona yanatokea leo, hayatokei kwa bahati mbaya, ni mipango Mahususi kutoka kwa mabingwa wa siasa.
Tuliahidi kushikisha watu adabu na kuleta mgombea anayekubalika. TUMETEKELEZA kwa vitendo. Wala rushwa waliotaka kukinajisi chama wameshikishwa adabu kwa kukatwa majina yao.
Aidha, ilishasemwa, nami nasisitiza; kushinda kura za maoni sio kushinda uteuzi, ni sehemu ya mchakato. Chama kina macho na masikio mengi na ndio sababu kwenye baadhi ya maeneo wameteuliwa watia nia ambao hawakuongoza. Moja ya sababu ni uwezo binafsi wa mgombea kupambana na mgombea wa upinzani katika Jimbo husika.
Kwa safu hii, CCM inaenda kushinda kwa kishindo. Shime wanaCCM popote mlipo, tuungane kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo wakihistoria. Wapinzani wetu WAMESHATEPETA.